Tetesi: Rwanda nyuma ya kufukuzwa Shyrose!

jMali

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
8,379
4,899
Shyrose ndio aliyezima jaribio la Rwanda kutumia bunge la EAC kwa maslahi ya utawala wao wa kidikteta, ikiwemo kuongoza wabunge kupinga kupinduliwa kwa spika aliyekataa hoja ya Rwanda kutengeneza historia batili ya genocide ambayo ingekuwa endorsed na bunge hilo. Shyrose pia alikuwa mstari wa mbele kupinga ardhi yetu kuwa ya cha wote ndani ya EAC, kinyume na matakwa ya Rwanda. Hilo ndio kosa lake.

Bahati mbaya mkuu wa sasa ni "rafiki" (mwenzao?) wa utawala wa kidikteta wa Rwanda, hili liko wazi. Sera yetu juu ya Rwanda kisiasa tuliyokuwa nayo toka tuwasuluhishe 1994 imepinduliwa chini juu! Hii ndio sababu haijawahi kutokea mtu anakatwa jina na mwenyekiti kimabavu bila kikao kuelezwa chochote kile!

Kashfa hizi zinazorudiwa rudiwa kuhusu ulevi na kupigana etc, zilishathibitika kuwa ni fitna za vyombo vya habari vya serikali ya Rwanda humu humu JF kitambo sana. (threads ziko chini). Jamani, bunge la EAC linaendeshwa kwa sheria, mbunge akikosea anafukuzwa kama ilivyo bunge lingine. Ukweli ni kuwa baada ya vyombo vya serikali ya Rwanda kueneza propaganda juu ya Shyrose, HAKUNA SHITAKA HATA MOJA ambalo shyrose alipewa kutokana na huo uzushi wa Rwanda! Na mtu akifanya fujo kwenye ndege pia hukamatwa immediately akitua huko anakokwenda. Vyombo pekee vya habari vilivyoandika habari hizi ni vya serikali ya Rwanda!
In fact SERIKALI YETU WENYEWE pia ilisimama kifua mbele kwa kumtetea shyrose! (thread hapa: Serikali: Shy-Rose hakupigana Kenya), leo hii mkuu wa serikali anamkata Shyrose kwa tuhuma zipi tena?

Shyrose so far ndio mbunge mwenye mchango mkubwa EAC kuliko wengine, lets be objective hapa, ni mchango gani wabunge wengine wote wa TZ wametoa bungeni EAC kumzidi shyrose? Kwa nini hoja isiwe kiwango cha kazi yake na badala yake tunajikita kwenye mfumo dume kuhoji masuala ya ndoa yake? Huu ni unafiki just because she is a woman!

Hatari tuliyonayo sasa ni kuendeshwa na Rwanda. Hii ndio system yao duniani kote, unapoingia utawala rafiki na wao, wale maadui zao wote wa zamani huwa "wanasomeshwa" namba kama anavyofanyiwa Shyrose. Msishangae kashfa mbalimbali zikaanza kuibuka dhidi ya Membe, Kikwete, Kamanda kibolwa na wengineo wote.

Na tusishangae sasa tukaanza endorsement ya historia ya genocide according to Kagame, ingawa nchi yetu ilikuwapo na ilishuhudia what happened, tayari amri za ma DC kuwatoa wafugaji haramu maporini kule Kagera, zinatenguliwa na "ngazi za juu" kwa upuuzi eti "hatuna pa kuwaweka wanyama"! Sasa tusishangae serikali yetu ikiridhia kuwa ardhi yetu ni iwe ni free for all kwa EAC wote n.k
Kwa tunaoelewa geopolitics, shyrose will always be a heroine!

Past theads:
1. Shy-Rose Bhanji Ajitetea
2. Sakata la Shyrose Bhanji na agenda ya Wanyarwanda kumng'oa Spika wa Bunge la Afrika Mashariki
3. Aibu: Shyrose Bhanji azua tafrani ziara ya EALA
 
Jamani hakuna alo wahi kuwa mbunge milele, mbona mwenzie Nape ametolewa uwaziri juzi na akaishia kushukuru tu!? Ndio maisha hayo huwez kuwa sehemu moja milele, she should get over with it, and move on. Nothing is permanent in this world.
Shy hakuzaliwa akiwa mbunge atulie sasa ubunge umeisha na ni wa muda tu
 
Watu waliojitokeza kuomba ubunge ni zaidi ya 400 halafu mtu mmoja anadhani ni haki yake pekee kuwa mbunge.

Uongozi ni kupokezana vijiti. Muda wa uongozi wake ndani ya bunge la EAC umefika kikomo kwa tiketi ya CCM. Kulia lia hakusaidii chochote. Just shake the dust and move on!

Unadai hakuna mtu aliyekatwa jina kwenye vikao vya CCM bila kutolewa maelezo. Are you kidding me? Kamuulize Edward Lowassa atakupa jibu sahihi.
 
Toba kumbe kuna mtu kazaa a shemejiwe

Hili povu la Shyrose kwa mwenyekiti aliyemkata kimabavu linaichana CCM vipande-vipande hadi raha.
 
Back
Top Bottom