Rwanda military trained Burundi rebels to oust Nkurunziza – UN Report reveals

meningitis

JF-Expert Member
Nov 17, 2010
8,394
4,748
Ripoti ya siri katika baraza la usalama la Umoja wa Mataifa inaishtumu Rwanda kwa kuwasajili na kuwapa mafunzo wakimbizi wa Burundi kwa lengo la kumpindua rais wa Burundi Pierre Nkurunziza.

Kulingana na chombo cha habari cha Reuters,ripoti hiyo ya wataalam wa Umoja wa Mataifa ambao hufuatilia vikwazo dhidi ya taifa la DR Congo inadai kwamba mafunzo yalifanywa katika kambi moja ya msituni nchini Rwanda,kwa mujibu wa Reuters.

Wataalam hao wamesema katika ripoti hiyo kwamba walizungumza na wapiganaji 18 wa Burundi mashariki mwa mkoa wa kusini wa Kivu nchini DRC,kulingana na chombo hicho cha habari.

''Wote waliliambia kundi hilo kwamba wamesajiliwa katika kambi ya wakimbizi ya Mahama mashariki mwa Rwanda mnamo mwezi Mei na Juni mwaka 2015 na walipatiwa miezi miwili ya mafunzo ya kijeshi na walimu wao,ambao walishirikisha wanajeshi wa Rwanda'',Reuters imenukuu ripoti hiyo ikisema.

Akijibu madai hayo, waziri wa maswala ya kigeni nchini Rwanda Louise Mushikiwabo amesema kuwa mgogoro huo wa Burundi ni mzito na wa kujitakia miongoni mwa viongozi wa taifa hilo na kwamba jamii ya kimataifa inafaa kuuangazia na kuwacha kutafuta sababu za kuuepuka.

''Ni Muhimu kuelewa kwamba usimamizi wa wakimbizi wa taifa jirani ni swala gumu,hivyobasi Serikali ya Rwanda imelazimika kuweka sheria kali dhidi ya wakimbizi wa Burundi''.

Mushikiwabo amesema kuwa madai hayo yanatokana na hatua ya Rwanda kuwahifadhi wakimbizi wa Burundi ambao wanadaiwa kuwa wapinzani wa serikali.

Waziri huyo ameongezea:Hatuwezi kuwarudisha wakimbizi hao hadi pale kutakapokuwa na mfumo ambao utalinda maisha yao nchini Burundi.

Burundi imekabiliwa na machafuko tangu mwezi Aprili,wakati rais Pierre Nkurunziza alipotangaza kwamba atawania muhula wa tatu wa urais,ambao alishinda.

Alinusurika jaribio la mapinduzi mnamo mwezi Mei,na majenerali wake wanne wamehukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kupanga kumpindua.

=======
A United Nations report has accused Rwanda of recruiting and training refugees from Burundi to oust President Pierre Nkurunziza, according to a Reuters news agency report.

Rebel fighters told the UN panel of experts who monitored sanctions on the Democratic Republic of Congo, that the training was done in a forest camp in Rwanda.

“They told the group that they had been recruited in the Mahama Refugee Camp in eastern Rwanda in May and June 2015 and were given two months of military training by instructors, who included Rwanda military personnel,” according to Reuters.

18 Burundian combatants including six children in South Kivu province, in eastern Congo told the experts they were trained in military tactics, use of assault rifles, rocket propelled grenades among others.

Rwanda Ambassador to the UN Eugene Gasana dismissed the claims.

“This further undermines the credibility of the Group of Experts, which seems to have extended its own mandate, but apparently investigating Burundi,” Ambassador Gasana told Reuters.

In December, Burundi had accused Rwanda of supporting a rebel group that was recruiting Burundi refugees in Rwanda but President Paul Kagame dismissed the claims describing it as “childish”.


Source:
Reuters
 
Pamoja na yoote Kagame ni kitu chaajabu sana!kwetu kama nikitoto tunakiita kigego yani kilichoanza kuota meno ya juu,mda mwingi anachonganisha wenzie,nasikitika Rwanda hamna mwenye ufahamu mkubwa kumzidi.
 
kinacho waponza wahutu ni Woga na kutokuwa na mikakati ya kueleweka, inashangaza sana watu mko asilimia 90% mnakubali kutaliwa na watu asilimia 9%, then huyu Kagame naye napaswa kuwa makini maana ipo siku kitawaka kwake pia.
 
Kagame alishateka saiklojia ya wanyaru. Kawaminisha kuwa yeye ndiye hakuna wenye uwezo wakuitala Rwanda zaidi yake. Vitisho vingi mno kaweka kwenye mioyo ya Wanyaru balaa
 
Ripoti ya siri ya UN imeeleza kuwa Rwanda ilitoa mafunzo kwa wakimbizi wa burundi ii kumng'oa Nkurunzinza!
Mkuu unawezakutupa chanzo au kuweka hiyo document au ni habari za virabu vya wanzuki?maana unachokiongea ni kitu kizito kuongea bila hata ushahidi ni kuropoka au umbea!Usijidanganye nyuma ya keyboard!
 
kinacho waponza wahutu ni Woga na kutokuwa na mikakati ya kueleweka, inashangaza sana watu mko asilimia 90% mnakubali kutaliwa na watu asilimia 9%, then huyu Kagame naye napaswa kuwa makini maana ipo siku kitawaka kwake pia.
unahamasisha ukabila na vita ya wenyewe kwa wenyewe
 
Kagame aneaendelea ututsi, kitu ambacho ni sio kizuri kwa sababu itaendeleza ubaguzi. Hao wahutu hawatokubali itafika kipindi nao wakianza jitihada za kupiana uhutu wao na yatajirudia ya 94. Watutsi wanaweza kuona fahari sasa hivi anayoyafanya Kagame lakini anatengenez tatizo kubwa huko baadae.
 
Ukiulizwa chanzo ni link au URL
Weka link kama ushahidi wa habari yako, vinginevyo utaonekana una chuki binafsi na rwanda.
Wadau, mlijaribu ku-copy angalau sentence moja na ku-Google kama namna ya kupata source of information? Anyway, tuyaache hayo manake only first sentence imenipatia links zifuatazo:

SOURCE FROM REUTERS
A confidential report to the United Nations Security Council accuses Rwanda of recruiting and training Burundian refugees with the goal of ousting Burundian President Pierre Nkurunziza.

INTERNATIONAL BUSINESS TIMES
A leaked memo to the United Nations Security Council has become the most compelling testimony yet that Rwanda is meddling in Burundi's affairs, accusing Rwanda of recruiting and training Burundian refugees with the goal of ousting Burundian President Pierre Nkurunziza.

AFRICA NEWS
A United Nations report has accused Rwanda of recruiting and training refugees from Burundi to oust President Pierre Nkurunziza, according to a Reuters news agency report.

Rebel fighters told the UN panel of experts who monitored sanctions on the Democratic Republic of Congo, that the training was done in a forest camp in Rwanda.

BBC
A confidential report to the UN Security Council accuses Rwanda of recruiting and training Burundian refugees with the aim of overthrowing Burundi's President Pierre Nkurunziza, Reuters news agency is reporting.
 
Mkuu unawezakutupa chanzo au kuweka hiyo document au ni habari za virabu vya wanzuki?maana unachokiongea ni kitu kizito kuongea bila hata ushahidi ni kuropoka au umbea!Usijidanganye nyuma ya keyboard!
Lini umeanza ku-behave kama hawa wanaoitwa NYUMBU?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom