Hapana. Kwa maoni yangu amani haiwezi kupatikana Rwanda kwa kuzungumza na FDLR. Ni kama vile umwambie Myahudi enzi za holocaust azungumze na Wanazi. Kikwete is still wrong on this.
Convince me with a better argument. Mimi napinga hoja yako kwa sababu zifuatazo. Baada ya vita kuu ya Pili ya Dunia, mambo makuu kadhaa yalitokea, lakini kubwa ninalo liona mimi lilikuwa lile ya mwenye nguvu kutafuta maridhiano ya wale walio shindwa. Vita ya Rwanda Wahutu walishindwa SI kwa sababu Watusi peke yao waliwazidi Wahutu nguvu , bali kwa sababu walijitokeza watu kuwasaidia Watusi kwa huruma ya mauaji ya Kimbari.
Wale waliokuwa wamewasaidia Watusi kuingia maradarakani walikuwa watu wa nje. Hawa watu walitaka wafukuze Wahutu ile nchi ibakie kuwa ya Watusi Peke yao? Najua utakubaliana na mimi kuwa lengo si hilo. Walio wasaidia Watusi walikuwa wanatufuta kupunguza nguvu ya Wahutu ili kuleta amani pale Rwanda watu (Watusi na Wahutu) wakae pamoja kwa amani.
Tatizo ni kwamba kilichotokea pale Watusi wanataka wakae peke yao. Ili kujua namna ya kukaa pamoja mazungumzo ni kitu cha Msingi kabisa. Hakuna njia mbadala.
Baada ya Vita Kuu ya Pili ya dunia Marekani aliibuka Mtawala wa dunia. Kitu cha kwanza alichofanya baada ya kuibuka mshindi ilikuwa kutafuta amani na wale aliowashinda nguvu. Na haya yalifanyika kwa njia za mazungumzo; mazungumzo ambayo yalisababisha Ulaya Magharibi na Japani --sehemu ambako Marekani walikuwa wameweka mchango mkubwa sana wa kuchakaza watu na miundombinu--kupewa misaada mingi na hatimaye kujenga mahusimano makubwa sana na maridhiano. Marekani ilichukua jukumu la Kuilinda Japani na kuiwezesha kiuchumi. Walipewa pesa nyingi za kufufulia uchumi. Pale Ulaya Magharibi vivyo hivyo ulipelekwa msaada wa kufufulia uchumi na huduma muhimu za Kijamii. Mahitaji haya yalijulikana kwa kuzungumza kati ya mwenye nguvu na yule asiye na nguvu.
Huwezi kujua huyu unayepigana naye anataka nini hasa ili kumaliza vita bila kufanya mazungumzo naye. Kwa hiyo Mazunguzo ni jambo la msingi sana katika kutafuta amani.
Hizi pande mbili zinatakiwa kuweka madai yao mezani ili madai haya yaanze kujadiliwa kutafuta mwafaka. Wahutu ni Wengi kuliko Watusi. Bila mazungumzo kuona ni kwa njia gani hawa wengi na hawa wachache wanaosaidiwa kuwa madarakani kwa nguvu kutoka nje wanaweza kumaliza tofauti zao, vita hii haitaisha bila kuzungumza.
Wewe sasa nipe maelezo yanayojitosheleza kwanini amani itapatikana Rwanda kwa kabila dogo kukandamiza kabila kubwa. Yaani sikuelewi kabisa Mkuu!