Ruzuku itatuathiri kichama - CHADEMA

Ruzuku inasagwa na viongozi wachache ndani ya chama halafu na wewe unataka kuendeleza kuchangia wanaume wenzako waweze kulea wake zao na vimada wao? Hii ni aibu.

zile mlizoficha uswisi mmeshazirudisha?
 
Wangeifuta kabisa ili hawa wachumia tumbo, CHADEMA wajifunze adabu!

View attachment 117425 View attachment 117428

Ikifutwa unafikiri hawa misukule mnayoitumikisha mtaiona tena, maana yote haya wanayafanya kwa sababu ya Ruzuku mnayopewa


Na Ruzuku ikifutwa hii kitu hapo juu hamtaweza tena kununua na itakuwa nafuu kwa CHADEMA mikutano itakuwa salama.
 
EPA,DEEP GREEN na MEREMETA

RADA, NDEGE YA RAIS, RICHMOND, DOWANS, IPTL, NBC, KIWIRA, KUSAFITISHA WANYAMA HAI KIA, PESA ZA USWISI, BUZWAGI N.K.
 
Mkuu mamseri binafsi napendekeza viongozi wa Chadema waitishe harambee ya dharura kwa wanachama kote nchini ili operesheni za chama zisisimame.

hata mimi nasapoti cdm waitishe harambee haraka iwezekanavyo tukichangie chama chetu cha ukombozi wa kweli.ila tu naskitika ile timu y lb7 itakufa kifo cha panya.
 
Last edited by a moderator:
Kama kweli kuna ufujaji basi anayetoa hizo fedha bila udhibiti wa matumizi yake yu -------- zaidi
 
Kamati ya PAC inatekeleza majukumu yake kisheria. Hii ni taarifa njema kwa wapenda nchi yao.
 
Hivi kwani kufuata utaratibu kuna shida gani? Nilivyosikia vyama vinatakiwa kwanza kupitisha report zao kwa mkaguzi mkuu wa serikali ambae atapitia akiridhika ata sign na kuweka muhuri wake,kabla ya kupeleka kwa msajiri. Vyama havikupitosha kwa CAG kwa kuogopa kubanwa kimahesabu wenyewe wakakimbilia kupeleka kwa msajiri.VYAMA VYOTE VYA SIASA Acheni ubabaishaji fuateni utaratibu kwani hizo ni KODI ZETU
 
Chama chetu cha CDM hakina deni. Sakata la kuwang'oa hawa wababe linaendelea kama kawaida nchini kote.
 
Nahisi zile safari za USA na Uk zitapungua hata uratibu wa maandamano utadhoofika, kelele nyingi kumbe unategemea nyumba ya kupanga kama ni kweli ruzuku imezuiwa tusubiri ofisi za CDM zikifungwa kwa kushindwa kulipa kodi.
 

kama ni kweli basi huu ukali wote utakuwa umeratibiwa na ccm kwa ajili ya kuvihujumu vyama vya upinzani vinavyotegemea ruzuku katika kutekeleza shughuli zao za kichama na kimaendeleo ila kwa ccm wao wako imara kwa kuwa na vyanzo vingi vya upatikanaji wa hela..mfano leo karibia viwanja vyote vitaingizia ccm hela kibao
 
Kama ni kweli ruzuku ingesitishwa, na kama ni kweli Chadema ingeathirika, basi CCM ndio ingekufa kabisa!.
Ndio maana ruzuku haitasimamamishwa. CCM nao wamo katika mkumbo huo!
 
Nimekwama ada ya shule jamani, kwa yule mwenye mapenzi naomba msaada wake ili niweze kutimiza ndoto yangu! na amini watanzania mara zote si watu wa kutupana bali ushikamana pale kunapokuwa na uhitaji. natanguliza shukurani zangu za dhati kabisa kwa yoyote atakaeguswa, kwa maelezo zaidi tafadhari ni PM
 

Mungu akubariki kwa mawazo mazuri sana ya kujenga.

Naamini viongozi wamekupata sawasawa.

Tumaini Makene Ben Saanane
 
Last edited by a moderator:

You are a star! Great Idea.
 

Hongera kwa ujasiri na kuwatia moyo viongozi.
 
Ccm kudhoofika ni ndoto ndugu zangu nyie jipangeni vizuri na zile harambee zenu za mia mia la sivyo mjichimbie kaburi mapema.

bora kidogo kuliko kikubwa cha masimango!sisi maskin wa mia mia tutakichangia inshallah
 
Nahisi zile safari za USA na Uk zitapungua hata uratibu wa maandamano utadhoofika, kelele nyingi kumbe unategemea nyumba ya kupanga kama ni kweli ruzuku imezuiwa tusubiri ofisi za CDM zikifungwa kwa kushindwa kulipa kodi.

pole kwa mawazo mgando.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…