Ruwasa katika ushindi unaomtua ndoo mwanamke wa Shinyanga

Apr 4, 2020
16
7
1586433563134.png


Waliofuata maji km. 3, imewajia mlangoni DC akoshwa, aja na ziara ya ushuhuda SERA ya Maji ya Mwaka 2002, inasema asilimia 85 ya wananchi vijijini wapatiwe maji safi na salama ifikapo mwaka 2020, huku mijini kukilengwa asilimia 100.

Serikali hivi sasa imeshaanzisha Wakala wa Maji Vijijini (Ruwasa), lengo ni kuongeza kasi ya utekelezaji miradi ya maji vijijini ili katika mwaka uliopo 2020, wananchi wake wafikiwe na maji safi na salama kwa asilimia 85 kama sera inavyoainisha.

Ruwasa wilayani Shinyanga, imekuwa na kasi kubwa ya utekelezaji miradi mingi kuondoa changamoto ya uhaba wa maji, pamoja na ‘kumtua ndoo kichwani’ mwanamke wa kijijini, hali inayomuokolea muda na safari ndefu ya kufuata maji.

Emmanuel Nkopi ni Kaimu Meneja wa Ruwasa, wilaya ya Shinyanga, anayesema miradi mingi ya maji wanayoitekeleza kwa wananchi, ni ya maji kutoka Ziwa Victoria. Nkopi anasema, kuna baadhi ya miradi imeshaanza kutoa huduma ya maji kwa wananchi, ikiwamo katika vijiji cha Mwiseme na Lyabusalu, huku miradi inayotarajiwa kukamilika mwezi huu, ni iliyoanza ujenzi Februari mwaka huu.


“Tunashirikiana na Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Shinyanga (Shuwasa), ambao wao wametoa Sh. milioni 100 na sisi Ruwasa milioni 50. “Mradi wa Maji kijiji cha Mwang’osha tunautekeleza sisi wenyewe ambao una gharama ya Sh. milioni 40; Lyabusalu Sh. milioni 39; Mwiseme Sh. milioni 41 na mradi mkubwa wa Masengwa, wenyewe una gharama ya Sh. bilioni 4.19 na miradi yote hii mwezi huu itakuwa imekamilika.” Nkopi anasema, kuna mikakati mikubwa ya utekelezaji miradi ya maji vijijini katika wilaya ya Shinyanga, ili kuhakikisha Sera ya Maji ya Mwaka 2002 inatekelezwa ipasavyo na kuondoa changamoto ya uhaba wa maji vijijini.

Taarifa ya Jimbo la Solwa wilayani Shinyanga, iliyosomwa na mbunge wake, Ahmed Salum, mbele ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, ni kwamba kuna vijiji 126 na kati yake, 93 ndio vina maji safi na salama. Salum anasema, mradi mkubwa wa maji kutoka Ziwa Victoria unatekelezwa katika Kata ya Masengwa, ambao utakapokamilika mwaka huu, kuna matarajio ya kunufaisha vijiji 14 vitakavyopitiwa na bomba kuu la maji, ikiwa ni hatua ya upatikanaji maji safi na salama.

DC MBONEKO
Jasinta Mboneko, ni Mkuu wa Wilaya Shinyanga, katika ziara ya kukagua utekelezaji miradi ya maji wilayani kwake, anasisitiza itekelezwe kwa wakati, ili kuondoa adha ya kupoteza muda wa shughuli za kiuchumi, kwa sababu ya kutafuta maji safi na salama.

Mkuu wa Wilaya, anaipongeza Ruwasa kutekeleza miradi mingi ya maji kwa muda mfupi walioanza kufanya kazi, akiwataka waendeleze kasi hiyo, huku akisisitiza vituo watakavyovitenga kwa wananchi kuchota maji, viwe karibu na makazi ya watu, ili kumtua ndoo mwanamke. “Nimefanya ziara hii, ili kukagua kasi ya utekelezaji wa miradi ya maji katika wilaya ya Shinyanga.

Nimeona inaridhisha na Ruwasa wanafanya kazi vizuri. “Baadhi ya miradi nimeona imeshaanza kutoa huduma ya maji kwa wananchi, licha ya kutokamilika kwa asilimia 100 jambo ambalo ni hatua nzuri. “Lengo la utekelezaji wa miradi hii ya maji, ni kukakikisha wananchi hawapotezi tena muda wa kufanya shughuli za kiuchumi, kwa sababu ya kutafuta maji safi na salama kutoka umbali mrefu, bali maji yawe karibu na wachape kazi,” anaeleza. Pia, rai yake kwa wananchi wanaotekelezewa miradi hiyo ya maji safi na salama, watunze miundombinu iliyopo wasiiharibu, iweze kudumu kwa muda mrefu kutoa huduma ya maji safi na salama.

MWENYEKITI KIJIJI
Mwenyekiti wa kijiji cha Mwiseme katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Deus Nyema, anaipongeza serikali kupitia wakala huyo wa maji vijijini Ruwasa, akilalamika kijiji hicho kilikuwa na tatizo kubwa la ukosefu wa maji safi na salama.

Anasema, wakati wanaletewa mradi huo wa maji kijijini hapo, ilibidi wahamasishe wananchi kujitolea kuchimba mitaro ya maji umbali wa kiliomita tano, kuonyesha uzalendo wao wa hamu ya kupata maji yao safi na salama kijijini humo. “Tulikuwa tunapata shida sana ya kutafuta maji ya kunywa umbali mrefu na wake zetu ndio walikuwa wakihangaika kufuata maji hayo, wakiamua mida ya usiku, lakini sasa hivi shida hiyo imekwisha kabisa,” anasema Nyema.

Diwani wa Kata ya Solwa, Awadhi Abood, anasema miradi ya maji vijijini inawakomboa wananchi katika kuinua uchumi, kwa sababu hawatapoteza muda, mbadala wake watajikita katika shughuli za maendeleo.

Anasema suala la ukuaji uchumi katika jamii, lina uhusiano mkubwa sana na upatikanaji wa maji, hivyo kuwapo vijiji au jamii inayokosa huduma ya maji, wanarudi nyuma kimaendeleo. “Nampongeza sana Kaimu Meneja wa Ruwasa,” anasema Abood na kuendelea: “Yaani ndani ya kipindi hiki kifupi ametekeleza miradi mingi ya maji safi na salama katika maeneo ya vijijini.” Huku akitoa kauli ya ‘kujipigia debe’ kwamba katika kipindi kilichopo cha lala salama ya awamu yake ya uongozi, anaahidi kuendeleza ushirikiano wa wananchi kujitolea katika kufanikisha miradi hiyo
 
Back
Top Bottom