RUVUMA : Mtoto adaiwa kumuua baba yake mzazi kisha kuchimba shimo kutaka kumzika

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
20,413
2,000
Jeshi la polisi mkoani Ruvuma linamshikilia Patrick Malindisa (29) mkazi wa mtaa wa Namanyigu kata ya Mshangao Manispaa ya Songea mkoani humo kwa tuhuma za kumuua baba yake mzazi Atanas Malindisa (70) kwa kumpiga na kitu chenye ncha butu kichwani na kidevuni upande wa kushoto kisha kufanya jaribio la kuchimba shimo kwenye nyumba hiyo kwa malengo ya kumzika baba huyo

Akizungumza na Ruvuma TV katika eneo la tukio mmoja wa wanafamilia ambaye ni mdogo wa marehemu Pius Malindisa, alisema kuwa wao walipata taarifa ya kifo cha ndugu yao Januari Mosi mwaka huu majira ya 1.30 kutoka kwa mtoto wa marehemu Patrick Malindisa

Pius alisema kuwa mtoto huyo ambaye alikuwa akiishi kwenye nyumba hiyo na marehemu huyo alitoa taarifa kwa wanandugu kuwa baba yake amefariki kwa homa ya tumbo na ndugu walipofika kabla ya kuingia chumbani alikokuwa akilala marehemu waliamua kuuita uongozi wa mtaa ambao uliingia na kubaini kuwa Atanas Malindisa ameuawa kwa kupigwa na kitu kichwani na kidevuni

Alisema kuwa baada ya kubaini hilo walitoa taarifa polisi kisha mwili huo ulichukuliwa na kwenda kuhifadhiwa Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma (HOMSO) kwa uchaguzi huku jeshi la polisi likimshikilia mtoto wa marehemu kwa mahojiano zaidi

Akifafanua kuwa polisi wakiwa bado kwenye nyumba hiyo walibaini kuwa kwenye moja ya chumba ambacho hakijaezekwa kulichimbwa shimo linaloendana na vipimo vya marehemu ambalo lilihisiwa kuwa alitaka amfukie humo ili watu wasijue kwa kuwa kwenye nyumba hiyo walikuwa wakiishi wawili

"Uchunguzi wa shimo hilo lenye mithiri ya kaburi lilimshinda kisha akaamua kulifukia na kuchukua hatua ya kuja kutoa taarifa kwetu wanandugu kuwa baba yake amefariki kwa homa ya tumbo ambalo inadaiwa alikuwa akilia nalo kumbe sivyo bali kapigwa na kitu kichwani"alisema ndugu wa marehemu
Picha ya kwanza mwenye Tishert ya damu ya mzee ni Pius Malindisa ambaye ni mdogo wake marehemu.
Na picha nyingine ni Ndugu jamaa na marafiki wakiwa wamejitokeza nyumbani kwa Bwana Atanas kwa ajili ya kwenda kumsitiri.

Chanzo : Michuzi Blog
 

64gb

JF-Expert Member
Sep 24, 2013
1,233
2,000
kweli binadamu asipo kuwa na dini, na sheria ni myama hatari sana
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom