DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,129
Rais wa Kenya, William Ruto, ameendelea kusisitiza nia yake ya kujenga kanisa la kisasa ndani ya Ikulu (State House), akipinga vikali kauli za baadhi ya watu wanaodai kuwa mradi huo utagharimu mabilioni ya fedha. Akizungumza katika ibada ya Jumapili ya leo, Ruto alisema haoni sababu ya watu kuhoji gharama ya ujenzi wa nyumba ya Mungu katika eneo la heshima kama Ikulu.
Ruto alieleza kuwa hatua ya kujenga kanisa hilo inalenga kubadilisha taswira ya kanisa la sasa lililopo ndani ya Ikulu ambalo limejengwa kwa mabati, jambo alilosema halilingani na hadhi ya taasisi hiyo ya juu ya nchi.
Soma Pia: Rais Ruto: Sitoomba msamaha Kwa kujenga Kanisa Ikulu
"Wengine wanasema eti kujenga kanisa Ikulu ni kutumia mabilioni. Lakini je, nikikutana na Mungu na aniulize kwa nini nilikaa kwenye jumba lenye vigae lakini kanisa likawa la mabati, nitamjibu nini?" — Rais William Ruto, Jumapili 6 Julai 2025.