Rusumo: Kijana mbadilisha fedha auawa na majambazi karibu na alipokuwa IGP

Tinde nsalala

JF-Expert Member
Feb 12, 2017
248
253
Mapema leo asubuhi IGP Mangu alikuwa mpakani mwa Tz na Rwanda (Rusumo).Lkn kuna tukio la kusikitisha sana na ni la kutia AIBU mno jeshi la polisi!

Akikagua jengo la kilipokuwa kituo cha polisi zamani km hatua 100 tu kijana mmoja mbadilisha fedha alivamiwa na kukatwa katwa mapanga huku askari wakiwepo jirani kabisa na vibaka hao kutokomea kusikojulikana!AIBU!

Mm pamoja na wenzangu tuliokuwa ktk msafara huo tumehudhunishwa sana na jambo hilo!Najiuliza,km mbele ya IGP,mkuu wa wilaya,mshauli wa mgambo wa wilaya,ocd wa wa eneo husika na ocid wake,mashushu walio kuwa eneo hilo na bado tukio la AIBU km hilo limeweza kutukia?!AIBU!

Sasa km vibaka wameweza kufanikiwa kufanya uhalifu tena bila kipangamizi chochote na mbele ya mkuu wa hawa wadhibiti uhalifu (IGP) .....

AJABU lingine hadi IGP anaondoka eneo husika hakufahamishwa kuhusu tukio hilo.Kuna wakati alishtuka na kuhoji idadi ya watu waliokuwa wanakimbia kuelekea eneo la tukio lkn alipotoshwa!

Hii ni hatari sana!Si kwa RAIA na mali zao pekee bali na kwa usalama wa IGP mwenyewe.Km wahalifu wanaweza kufanya jambo la AIBU hivyo na karibu kabisa na eneo alilopo ni hatari hata kwa usalama wake.

Nimehudhunishwa na kusikitishwa sana na AIBU hii!
 
Inamaana polisi walishuhudia tukio lakini hawakuchukua hatua yoyote? Au walikuwa hawana habari wapo busy kumlinda IGP?

Hatua 100 ni umbali mfupi sana. Hao polisi waliompotosha IGP walimuambia nini kuhusu kelele za watu waliokuwa wanaenda kushuhudia huo uhalifu?

Je huyo kijana aliyevamiwa amepona?
 
Sina uhakika na hiyo taarifa. Hatua mia ni ndogo sanaa huyo dogo hata angeweza kupiga kelele akasikika
 
Inamaana polisi walishuhudia tukio lakini hawakuchukua hatua yoyote? Au walikuwa hawana habari wapo busy kumlinda IGP?

Hatua 100 ni umbali mfupi sana. Hao polisi waliompotosha IGP walimuambia nini kuhusu kelele za watu waliokuwa wanaenda kushuhudia huo uhalifu?

Je huyo kijana aliyevamiwa amepona?
Km unavyoelewa,askari wetu huwa km wamechanganyikiwa mara viongozi wao wawapo na ziara ktk maeneo yao ya kazi.Binafsi,hadi tunaondoka (Msafara) kuelekea upande wa Rwanda walipokuwa wanakutana IGP wetu na RWANDA sikuona hatua zozote za haraka zilizochukuliwa na askari wetu.Kuhusu afya ya majeruhi pia sina hakika juu maendeleo yake.Kwa mjibu wa afisa wa TRA sitaki kumtaja jina kijana yule kaumizwa sana!
 
Mapema leo asubuhi IGP Mangu alikuwa mpakani mwa Tz na Rwanda (Rusumo).Lkn kuna tukio la kusikitisha sana na ni la kutia AIBU mno jeshi la polisi!

Akikagua jengo la kilipokuwa kituo cha polisi zamani km hatua 100 tu kijana mmoja mbadilisha fedha alivamiwa na kukatwa katwa mapanga huku askari wakiwepo jirani kabisa na vibaka hao kutokomea kusikojulikana!AIBU!

Mm pamoja na wenzangu tuliokuwa ktk msafara huo tumehudhunishwa sana na jambo hilo!Najiuliza,km mbele ya IGP,mkuu wa wilaya,mshauli wa mgambo wa wilaya,ocd wa wa eneo husika na ocid wake,mashushu walio kuwa eneo hilo na bado tukio la AIBU km hilo limeweza kutukia?!AIBU!

Sasa km vibaka wameweza kufanikiwa kufanya uhalifu tena bila kipangamizi chochote na mbele ya mkuu wa hawa wadhibiti uhalifu (IGP) .....

AJABU lingine hadi IGP anaondoka eneo husika hakufahamishwa kuhusu tukio hilo.Kuna wakati alishtuka na kuhoji idadi ya watu waliokuwa wanakimbia kuelekea eneo la tukio lkn alipotoshwa!

Hii ni hatari sana!Si kwa RAIA na mali zao pekee bali na kwa usalama wa IGP mwenyewe.Km wahalifu wanaweza kufanya jambo la AIBU hivyo na karibu kabisa na eneo alilopo ni hatari hata kwa usalama wake.

Nimehudhunishwa na kusikitishwa sana na AIBU hii!

Wewe ni muongo mita 100 nikidogo sana tena eneo lililo na watu unless uniambie ni porini!!!
 
Kama ni hivyo basi polisi sio chombo cha kulinda raia tena bali ni chombo cha kushughulikia watu na kusahau kazi yao
 
Huko.hata wale waliouawa wakivua Serikali badala ya kutatua tatizo wakawanyima Watanzania haki ya kwenda kuvua kwenye MTO wao.Hivyo si ajabu hilo kutokea.
 
Tunajilinda kwa kila namna, ukitegemea ulindwe na police hawa basi imekula kwako...tuwe tunafanya mazoezi ya kila namna ili kupambana na waharifu ktk maisha yetu, na tujilinde pia na police uchwara
 
Wewe ni muongo mita 100 nikidogo sana tena eneo lililo na watu unless uniambie ni porini!!!

Mtu yeyote mwenye nia mbaya /alie dhamiria kwa sababu ya kupata kitu flani anapo panga mipango yake kabla ya kutekeleza nae pia hutumia akili naamna ya kufanikiwa..Usishangae kuhusu umbali ,jiulize baadhi ya Maraisi waliowahi kushambuliwa pamoja na ulinzi mkubwa walifanikiwaje ...

Kinacho tushangaza hapa ni kwanini Polisi hawakuchukua hatua wakati silaha walikuwa nazo..
 
Back
Top Bottom