STRUGGLE MAN
JF-Expert Member
- May 31, 2018
- 8,633
- 16,601
Russia yajibu mapigo baada ya wanadiplomasia wake kutimuliwa nchini Ujerumani
Serikali ya Russia imejibu mapigo ya kutumuliwa nchini Ujerumani wanadiplomasia wake wawili ambapo nayo imetangaza kuwatimua wanadiplomasia wawili wa Ujerumani walioko mjini Moscow, hatua ambayo inaashiria kuibuka mgogoro wa kidiplomasia baina ya nchi mbili hizo.
Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Russia imetangaza kuwa, imechukua uamuzi wa kuwatimua nchini humo wanadiplomasia wawili wa Ujerumani kama kujibu mapigo hatua kama hiyo iliyochukuliwa na Ujerumani.
Taarifa zaidi zinasema kuwa, Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Ruussia mapema leo ilimwita katika wizara hiyo Geza Andreas von Geyr, balozi wa Ujerumani mjini Moscow ambapo sambamba na kumkabidhi malalamiko ya nchi hiyo dhidi ya hatua ya Ujerumani ya kuwatimua wanadiplomasia wa Russia ilitaka maelezo kuhusiana na hatua hiyo.
Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Russia imetangaza kuwa, imewatimua wanadiplomasia hao kwani ni watu wasiofaa kubakia nchini humo na imewataka kuondoka nchini humo mara moja.
Siku chache zilizopita, Ujerumani ilichukua hatua kama hiyo baada ya kuwatimua wanadiplomasia wawili katika ubalozi wa Russia ikiwatuhumu kwamba, walihusika katika mauaji dhidi ya raia mmoja wa Georgia mjini Berlin na kueleza kwamba, ni watu wasiofaa kubakia nchini humo.
Wachambuzi wa mambo wanasema kuwa, huenda huu ukawa mwanzo wa mgogoro wa kidiplomasia baina ya Russia na Ujerumani endapo hakutachukuliwa hatua za haraka za kuondoa suutafahamu hii iliyojitokeza.
Sent using Jamii Forums mobile app