Sinoni
JF-Expert Member
- May 16, 2011
- 6,174
- 10,650
Rais wa Russia Vladimir Putin amesema nchi yake itasaidia juhudi za Palestina za kuupatia ufumbuzi mgogoro kati yake na utawala wa kizayuni wa Israel kwa njia ya mazungumzo.
Putin aliyasema hayo jana Jumatatu mjini Moscow katika mkutano wake na Mahmoud Abbas, Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina na kuongeza kuwa, Russia ingependa kufanya mazungumzo ya kuimarisha uhusiano wa pande mbili na Palestina na haswa katika uga wa kiuchumi.
Kadhalika Rais Putin amesisitizia juu ya umuhimu wa kuundwa Kamisheni ya Pamoja ya Serikali za Russia na Palestina.
Kwa upande wake, Mahmoud Abbas, Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina amesema kwa sasa kadhia kuu na yenye umuhimu kwa Wapalestina ni kuandaa kongamano la kimataifa la amani katika ardhi zao zinazokaliwa kwa mabavu na utawala ghasibu wa Israel.
Ni vyema kuashiria hapa kuwa, duru ya mwisho ya eti mazungumzo ya amani kati ya Israel na Palestina iligonga mwamba mwaka 2014. Tel Aviv ilifutilia mbali mazungumzo na Palestina mnamo Aprili 24 mwaka 2014, baada ya Mahmoud Abbas kusaini makubaliano ya amani na harakati ya Kiislamu ya Palestina Hamas.