Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 20,341
- 38,493
Mapambano dhidi ya Rushwa ni suala la Kisera linalohitaji utashi mkubwa sana wa kisiasa kwenye kuyafanikisha. Tangu enzi za "Tume ya Rushwa" iliyoongozwa na Jaji Joseph Warioba, mahakama ilitajwa na wananchi kama moja ya sehemu zenye ubobezi wa kupokea rushwa kama walivyo pia ni wabobezi wa sheria.
Binafsi nimeshuhudia mara kadhaa rushwa ndani ya mhimili huu muhimu wa kutoa haki. Kuna mtu alipelekwa mahabusu kwa kesi ya jinai ambayo ilianzia hapo hapo mahakamani bila ya Polisi kuhusika nayo kwenye ngazi ya uchunguzi. RCO hakuifahamu wala jalada lake halikuwahi funguliwa polisi. Baadaye iligundulika hakimu alipewa rushwa.
Nimewahi kuwasikia Mawakili wawili tofauti ten kwa nyakati tofauti wakiwashawishi wateja wao kutoa hela ili "wakamweleweshe" hakimu aliyekuwa anasimamia kesi husika. Nikajiuliza sasa wanapofanya mjadala mahakamani huwa wanatumia sheria kushinda kesi au ile rushwa waliyotoa ndiyo huwasaidia kushinda? Mifano ya aina hiyo ipo mingi sana.
Mahakama ambayo ndiyo chombo cha kutoa haki kama inagubikwa na rushwa haki itapatikana wapi. Tutakuwa na hakika kiasi gani kwamba maamuzi ya mahakama hayatokani na ushawishi wa rushwa kama hata mawikili wanaamini mahakimu wanatakiwa kupewa rushwa ili "waelewe" hoja zao wakati wa undeshaji wa kesi?
Nini kifanyike ili kukomesha rushwa ndani ya mhimili wa mahakama?