Rushwa katika mitihani ya leseni ya wafamasia

Cashman

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2018
Posts
3,289
Reaction score
5,741
Mwishoni mwa Disemba tuliona matokeo mabaya sana ya leseni kwa kada ya ufamasia.

Licha ya matokeo kuwa mabaya hivyo,kuna ushahidi wa baadhi ya watu wa kada ya kati walioombwa rushwa ili wafaulu mitihani hiyo.Waliotoa walifaulu pasipo kufanya mtihani wowote.

Kumekuwa na baadhi ya watu wanaoitumia mithihani hii kujinufaisha kifedha na kingono.

Napendekeza yafuatayo ili kupunguza au kuzuia uwezekano wa mianya ya baadhi ya watu kupata leseni bila kufanya mitihani.

1. Kuwe na mitihani ya vitendo,isimamiwe na wafamasia walioko hospitalini.

2. Orodha ya watahiniwa watarajali zipelekwe baraza la wafamasia na vyuo husika vikiambatana na matokeo yao,nakala zipelekwe kwa wafamasia wa mikoa.Orodha ya majina haya ichapishwe wazi kwenye tovuti ya baraza la wafamasia.

3. Wote wasajiliwe kufanya mitihani bila kujali wamelipia ama hawajalipia.Kama mtahiniwa akifanya bila kulipia,gharama hizo azilipe wakati wa kwenda kuchukua leseni yake.

4. Mitihani ya leseni ifanyike mara tu baada ya matokeo ya mwisho vyuoni na kwa wote wenye sifa ya kufanya mitihani hiyo.

5. Baraza lisomeshe wataalamu wa IT ili kuongeza uwajibikaji kwani waliopo inaonekana sio wanataaluma wa famasia na wanahusika sana na matukio ya kughushi na kuvujisha mitihani

6. Mchakato wa mitihani uwe na uwazi na kuondoa maamuzi ya watu wachache wanaogeuka miungu watu na wakipewa chochote wanakiuka maadili.
 
Una hoja usikilizwe
 
Pharmacy council wapo kimaslahi. Wanafanya kufaulu iwe bahati badala ya contents
 
Back
Top Bottom