Rushwa imeingia katika Mafunzo ya Udereva

nndondo

JF-Expert Member
Feb 1, 2010
1,251
895
Nimeamua kutuma hii post huku pia kutokana na umuhimu wake. Naomba sana Afanda Mpinga, Takukukuru na uongozi wa chuo cha usafirishaji pale ubungo muingilie kati mara moja tabia iliyozoeleka ya walimu wa mafunzo ya udereva kuchukua rushwa ili kupasisha wanafunzo wasio na uwezo. Ni wiki moja tu mafunzo ya udereva ya wiki mbili yalizinduliwa toka July 1 na yataisha julai 8. Tuko wanafunzo zaidi ya 167 ambao tumelipa ada ya walau shs 200,000/-. Ndio kwanza jana tumemaliza wiki moja ya mafunzo ya darasani tukitegemea kuanza mafunzo kwa vitendo kesho.

Cha kushangaza ni pale jana ambapo mwenyekiti wa darasa alipelekezwa kukusanya majina ya watu wanaotaka kupata cheti kati ya wanafunzi. Mwenyekiti alituita mmoja mmoja kisiri na kutueleza mpango huo ambapo mtu ulitakiwa kutoa shs 35,000/- ili jina lako lipelekwe kwa walimu, na kwamba wiki ijayo utakapopata namba ya mtihani uiwakilishe kwa mwenyekiti ili ampe huyo mwalimu na kuhakikisha kuwa unapasi na kupata cheti. Tayari wakati napata habari hizi majin yalishakuwa yamekusanywa na watu wametoa hela. Sasa cha kushangaza utachukuaje hela kwa watu hata kabla hatujaenda kwenye mafunzo ya vitendo na kufanya mtihani? hili jambo ni la hatari sana kwa kuwa walimu hawa kwa tamaa ya pesa na rushwa wanawapasisha madereva wasio na uwezo wakiwemo wale waliosababisha ajali ya mabasi ya city boys.

Sasa kwa kuwa nchi yetu imegubikwa na ajali nyingi zisizo za lazima na kuua mamia ya watu wasio na hatia wakiwemo vijana wadogo waliokufa juzi, naomba sana uongozi wa chuo, uongozi wa trafi na afanda mpinga, na takukukuru watumia wiki hii tuliyobakiza kufanya uchunguzi wa kina na kuwatia mbaroni wahusika. Hili liko wazi mfuateni mwenyekiti awape list ya majina aliyokua anaandika jana pale darasani. Mwalimu husika ni yule wa kipindi cha mwisho jana pale kilichoisha saa 10. Chanzo cha ajali kumbe si lolote ni Rushwa ya walimu wa chuo kilichoamini na serikali kuwafundisha na kuwatathmini madereva
 
Aisee huu wakati mgumu pesa hakuna kila sehemu kumebana ww nawee unataka kupoteza riziki za wenzako any way vizuri sana kijana ila mm naamini udereva ni issue nyepesi haswa ukizingatia masomo na practise haswa haswa hapo NIT watu wanafata cheti na usikute wengine tayari ni madereva hapo wanapita njia kinachokuja mbeleni madereva kusababisha ajali sio hilo mkuu maana hakuna Tajiri atakae mpa gari mtu lenye dhaman kubwa bila kumfanyie interview ya vitendo kuona km kweli yuko makini na anajua.

Ila tatizo la madereva ni Bangi, viroba, Mbwembwe, haraka za kupata abiria vituo vya mbele, Matunzo ya gari kwa matajiri na ujinga wa madereva walio nao ndo vinasobabisha ajali na ndomana kuna raia akasema bora kwenye basi kuwe na askari. Au ww hujaona viongozi wenye kila sifa za elimu ndo wanaongozwa kwa kula rushwa na kula mali za umma
 
Back
Top Bottom