Sauti Ndogo
Member
- Mar 8, 2015
- 14
- 12
Nawe usipokee rushwa. Kwani hiyo rushwa hupofusha macho yao waonao na kuyapotoa maneno ya mwenye haki (Kutoka 23:8).
Wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu tumeendelea kushuhudia mambo yenye kuleta mashaka. Kubwa ni kubadilika kwa Dr. Slaa kuegemea upande wa CCM na kwanza kubomoa yale aliokuwa anayajenga kwa miaka mingi. Yeyote mwenye kufiri atahitimisha kuwa mtu huyu amenunuliwa.
Jambo la kwanza ni kuwa amepoteza 'objectivity' na kwake yeye ufisadi pekee Tanzania ni Richmond. Anataka kuwaaminsha watanzania kuwa tatizo kubwa la Tanzania ni Lowasa. Kwamba Tanzania ni maskini kwa sababu ya Lowasa. Kwa sasa haoni kashifa kama EPA, Radar, Uuzwaji wa nyumba za serikali, Tokomeza, Tegeta ESCROW nk. kwasababu kala Rushwa na hivyo macho yamepofuka.
Aidha ni ajabu sana kupigia kampeni chama kilichotawala kwa zaidi ya miaka hamsini lakini umasikini mkubwa bado umeshamili pamoja na rasilimali tulizonazo. Chama ambacho kimekataa katiba ya wananchi na kwa kiburi kabisa kupuuza yale yenye maslahi kwa nchi na kushikilia yale yanayolinda chama kwa kuwa wao ni wengi bungeni. Kwa kufanya hivi ni dhahili amesaliti matarajio ya wananchi malofa waliokuwa wamemwamini.
Kwa sasa Dr Slaa anajiona ni mwenye hekima machoni pake mwenyewe na kudhani yeye ndiye mwerevu pekee na kupuuzi ushauri wa watu wengi. Anapaswa kukumbuka kuwa kiburi hutangulia maangamivu na roho yenye kutakabari utangulia maanguko (mithali 16:18).