RUSHWA bungeni na Nchini: Tumeyataka wenyewe. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

RUSHWA bungeni na Nchini: Tumeyataka wenyewe.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by masopakyindi, Aug 1, 2012.

 1. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #1
  Aug 1, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,909
  Likes Received: 2,336
  Trophy Points: 280
  Kwa kweli mimi sishangai sana na habari za rushwa kupiga hodi Bungeni kwa kishindo.
  Kwa miaka kadhaa tena ni Bunge hilihili liliibua rushwa kubwa kubwa kama ya RICHMOND,EPA, KAGODA, RADAR,MEREMETA na hata scandals za pesa nyingi kupitia Import Support progammes za wafadhili.

  Iliyochunguzwa na kuchukuliwa hatua nusu nusu ni ile ya Richmond tu, na mpaka leo watuhumiwa wakuu wanaendelea kupeta katika siasa badala ya kuwa jela.

  Rushwa siku hizi ni rafiki ya mfuko, iwe Polisi, mahakamani na sehemu nyingi tu za kutolea haki.Usipokuwa na fedha za kujinasua katika matatizo ole wako!

  Hii rushwa kubwa kubwa ya fedha za kiwango cha mabilioni na matrilioni imeendelea kuvumiliwa kwa vile "hakuna ushahidi".

  Kwa hali hii Mbunge mwenye damu nyekudu, anayeishi tTanzania tutegemee nini?

  IF YOU CANT BEAT THEM,JOIN THEM!!!!

  Tumecheka na nyani sasa tunakula mabua, na tumefunika kombe, wanaharamu wa rushwa hawataki kuondoka.

  Wala rushwa tumewalea wenyewe na mimi sioni ni kwa vipi leo ushahidi wa rushwa ya wabunge wetu wapenzi utapatikana.

  Wasalaam!
   
 2. m

  mob JF-Expert Member

  #2
  Aug 1, 2012
  Joined: Dec 4, 2009
  Messages: 2,027
  Likes Received: 509
  Trophy Points: 280
  MKuu tatizo letu watanzania ni kuwa tumekuwa tukiyasikia na kuyaacha yapite.ila tunatakiwa kufanya maamuzi magumu kwa kuandamana hadi tuondoe huu mfumo kandamizi
   
 3. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #3
  Aug 1, 2012
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Rushwa siku hizi is the name of the game,
  Ni poa tu.
   
Loading...