Rule no9; Acha malalamiko"Be Grateful"

Rule no9; Acha malalamiko"Be Grateful"

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
34,114
Reaction score
79,522
RULE NO 9, ACHA MALALAMIKO" BE GRATEFUL"

Anaandika, Robert Heriel
Shahidi.

Moja ya vitu ambavyo ni nadra Sana kuvisikia kutoka katika mdomo ya watu waliofanikiwa katika Jambo lolote ni malalamiko.
Kanuni inasema; usijilaumu wala usilaumu wengine Kwa Yale yanayokutokea katika maisha yako, isipokuwa shukuru Kwa kila Jambo.
Neno kushukuru haimaanishi KURIDHIKA isipokuwa inamaanisha kukubali Hali halisi na kulitafutia ufumbuzi/suluhisho.

Uzoefu na uchunguzi wangu nilioufanya ulibaini kuwa 90% ya watu walioshindwa katika mambo fulanifulani katika maisha ni watu wa malalamiko. Aidha kujilaumu wao wenyewe au kulaumu wengine.

Malalamiko yamaanisha;
i. Kukata tamaa
ii. Kisingizio cha kushindwa au kuonewa
iii. Kutokuwa na Shukrani na kutokubaliana na Hali.
iv. Kuishiwa mbinu na akili ya kutatua tatizo.
V. Kubebesha wengine lawama/zigo la misumari.

Aina za Malalamiko
1. Malalamiko ya kimaumbile
2. Malalamiko ya kimazingira
3. Malalamiko ya Malezi na Makuzi
4. Malalamiko ya Kisiasa na kiuchumi.

1. Malalamiko ya kimaumbile.
Wapo watu ambao hulalamika kutokana na maumbile Yao. Mathalani watu wafupi, wanene kupitiliza, wembamba kupitiliza, walemavu, na wakati mwingine wapo watu hulalamika Kwa sababu ya jinsia zao hasa wanawake.
Mfano wa watu waliokuwa wanatumia udhaifu wa maumbile Yao kulalamika ni Nabii Musa ambaye alitaka kukataa misheni aliyopewa na Mungu kisa anaulimi mzito.

Maumbile hayakuzuii wewe kupata mafanikio, ninauhakika na ninachokisema,

Jinsi ya kufanya ikiwa unajiona unaupungufu wa maumbile ili ufanikiwe katika Jambo lolote utakalo;

i. Jikubali vile ulivyo kisha shukuru.
ii. Tumia wale wenye maumbile yaliyokamili kutimiza malengo yako. Hii itakupasa utumie akili kuwatumia watu hao.
Nitakupa mifano kadhaa ya watu waliotumia kanuni hii;
Mfano wa 1. Nabii Musa alimtumia Kuhani Haruni kuwa kama msemaji wake. Hivyo udhaifu wa Musa wa ulimi mzito, haruni aliu-cover.

Mfano wa 2. Bin Khadija na Muhammad S.W.A .
Wapo wanawake wenye ndoto ya kufanya biashara au kuwa matajiri na wanamitaji lakini kila wakifanya biashara zinawashindwa Kwa sababu ya jinsia zao.
Bi. Khadija Kwa kujua Jambo hilo alimuomba Mtume Muhammad amuoe, ili mbali na kuwa mume wake lakini awe msimamizi wa Biashara na Mali zake(Mali na biashara za Bi. Khadija) kumbuka tayari Muhammad alikuwa na uzoefu wa Biashara za Mjomba wake na alikuwa mtunza pesa za Makureshi.
Hivyo jinsia haiwezi kumfanya mtoto wakike asifanikiwe, Kama ataona jinsia yake ni kikwazo basi anaweza kutafuta mwanaume wa ku-cover pengo Hilo.

2. Malalamiko ya kimazingira.
Dunia iliumbwa ku-fit kila kiumbe na tabia zake.
Hakuna tabia mpya ambayo kiumbe ataianzisha ambayo dunia haijaandaliwa kukabiliana nayo.
Wapo watu hulalamika kuwa mazingira ndio sababu ya wao kushindwa, labda ukosefu wa mvua, Ardhi mbaya isiyo na rutuba, tabia ya nchi mbovu miongoni mwa sababu zingine.
Siku zote nasemaga mtu anayelalamika ni kwamba ameamua Kwa makusudi kushindwa na kutafuta sababu ya kushindwa kwake, wakati mtu ambaye anashukuru ni mtu anayetafuta sababu za kushinda kwake. Yaani afanye nini ashinde

Kuna namna mbili za kukabiliana na mazingira;
i. Kutumia Akili na Teknolojia kuyabadilisha vile utakavyo.
ii. Kuhama na kuondoka kwenda sehemu nyingine
Kama eneo ulilopo halikusapoti Kwa nini usihame? Au Kwa nini usitumie akili na Teknolojia kulibadilisha Liwe vile utakavyo.
Huwezi ng'ang'ania sehemu ambayo inakufanya ushindwe.
Kama wanyama tuu wenyewe wanahama sembuse wewe binadamu!

Mifano ya watu waliohama;
i. Ibrahimu na mkewe kutoka Uhuru wa ukaldayo kuelekea Canaan.
ii. Gadafi kutoka Sirte kuelekea Tripoli, Libya.
iii. Daudi kutoka Rama kwenda Yerusalemu,
iv. Muhammad kutoka Madina kwenda Makka.
v. Israel kutoka Misri Kurudi Canaan
vi. Ngoni Tribe kutoka Afrika Kusini mpaka Bongo Tanzania.
VIi. Boer kutoka Ujerumani na ufaransa mpaka south Afrika n.k.

Kuhama sio kosa, kuhama ni namna ya kutafuta maisha mazuri. Ni moja ya mbinu muhimu ya Msingi katika maisha.
Aina za kuhama.
1. Kuhama Kwa muda mfupi
2. Kuhama moja Kwa moja.
Kuhama Kwa muda mfupi hii ni kile kitendo cha mtu kuondoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine Kwa muda Fulani labda kutafuta maisha, au kukimbia njaa, kisha baadaye kurejea nyumbani(sehemu ya Asili)

Kuhama moja Kwa moja ni kitendo cha kuondoka moja Kwa moja Kwa kuhamisha eneo na Asili ya mtu kwenda sehemu nyingine. Ni Kama kuhamisha uraia/asili.
Mfano, Taikon nitoke Makanya kwenye kule Same nihamie Morogoro Kwa Waluguru au wakaguru moja Kwa moja.
Au vile Ibrahimu alivyoondoka Uhuru wa ukaldayo na kuvamia nchi ya Kanaani.
Au Wadachi(wajerumani) walivyohama Ujerumani wakafika Afrika Kusini wakaitwa Boer(lugha ya wenyeji huko Afrika Kusini).

Mazingira yasikufanye ulalamike. Kuwa na Shukrani.

3. Malalamiko ya Malezi au Makuzi.
Kuna watu wanatabia ya kulaumu wazazi wao au walezi wao Kwa vijitabia walivyokuwa na to.
Huna sababu ya kulaumu wazazi au walezi Kwa tabia ulizozikuta kwao.
Binadamu ni kiumbe ambaye anaweza kubadilisha tabia yake ingawaje ni Jambo gumu kubadili mazoea.
Kama unaona tabia Fulani ni mbaya na uliipata Kwa walezi au wazazi wako ibadili.

Sio ulaumu wazazi wako, hiyo haikufanyi uonekane hauna hatia.

4. Malalamiko ya Kisiasa na kiuchumi.
Baadhi ya watu hupenda kulalamika kutokana na Hali zao za kiuchumi.
Kuanzia ngazi ya familia mpaka taifa.

Kikawaida watu Kama Taikon hatuwavumilii watu wanaopenda kulalamika, kunung'unika,
Unakuta Mke kutwa kucha kukulalamikia labda chakula unachomlisha ni kibaya.
"Kila siku Dagaa, kila siku maharage yaani wewe mwanaume umenichosha"
Mimi kama Taikon mke wangu kamwe hatoweza kuthubutu kuongea huo upumbavu nikamvumilia. Nitamfukuza mchana kweupe.
Mama/Baba mlalamishi hawezi kuwa baraka katika maisha yako kubali au kataa.
Mama au Baba mlalamishi huzaa vitoto vilalamishi Visio na Shukrani.
Mkeo hashukuru Kwa kidogo ulichonacho kamwe hawezi kushukuru Kwa kikubwa utakachompa.
Mke anataka nyama wakati Hana mawazo ya maana ya kukufanya upate nyama, Hana ushauri wowote zaidi ya lawama. Sisi kina Taikon tunafukuza mchana kweupe akale nyama Kwa Baba yake huko.

Mungu mwenyewe hawezi mvumilia mtu mlalamishi hata siku moja, embu tuone Mungu anawachukuliaje watu walalamishi na anawafanyaje;
Hesabu 11:1
Kisha hao watu walikuwa kama wanung’unikao, wakinena maovu masikioni mwa BWANA; BWANA aliposikia hayo, hasira zake zikawaka; na moto wa BWANA ukawaka kati yao, ukateketeza katika mipaka ya mwisho wa marago.

Hesabu 11:2
Ndipo watu wakamlilia Musa; naye Musa akamwomba BWANA, na ule moto ukakoma.

Hesabu 11:4
Kisha mkutano wa wafuasi waliokuwa kati yao, wakashikwa na tamaa; wana wa Israeli nao wakalia tena, wakasema, N’nani atakayetupa nyama tule?

Hesabu 11:5
Twakumbuka samaki tuliokula huko Misri bure; na yale matango, na matikiti, na mboga, na vitunguu, na vitunguu saumu;

Hesabu 11:6
lakini sasa roho zetu zimekauka; hapana kitu cho chote; hatuna kitu cha kutumaini isipokuwa hii mana tu.

Ukioa mke mlalamishi asiye na Shukrani sio ajabu akakumbuka nyama choma alizokuwa anakula na Ex wake hata kama ni siku moja alikula lakini akatamka waziwazi.
Ndicho wanachofanya hao waisrael.
Watu wamekombolewa kutoka utumwani lakini Kwa kukosa kwao Shukrani wanaingiwa tamaa Kwa vitu vidogovidogo na kuanza kulalamika.

Dawa Yao ni kuwafutilia Mbali. Nasisitiza mtu asiye na Shukrani, mlalamishi huyo sio WA kuishi naye. Fukuza.
Au kama ni mke unaishi na Mwanaume asiye na Shukrani yeye kila kitu anakulalamikia achana naye huyo Mbuzi.
Yaani kwako hauna kitu chema, yeye kila kitu unachomfanyia ni malalamiko. Huyo muache/achana naye. Hamtafika popote.

Sifa za mtu mlalamishi.
1. Hana Shukrani
2. Mbinafsi
3. Ni rahisi kukusaliti
4. Mhesabu makosa tuu
5. Hana ufumbuzi/suluhisho n.k.

Wito: tuwafundishe watoto wetu tabia ya kuwa na Shukrani ili kujenga kizazi Bora chenye kuleta maendeleo.
Sio kizazi cha kulaumu wengine.
Usioe au kuolewa na mtu Mlalamishi hata kama unampenda vipi. Mlalamishi ni Kama nyoka kamwe hafugiki.

Vitabu vilivyotayari;
1. Wakala wa Siri Tsh 15,000/=
2. MLIO WA RISASI HARUSINI 15,000/=. Softcopy 8,000/=
3. Funguo 7 milango 12 Tsh 20,000/=
4. Kaburi la mwanamuziki. Tsh 15,000/=
0693322300

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Asante kwa ujumbe hii nchi kila mtu analalamika hadi akina Mwingulu na Makamba walalamika wamechoka kulamba asali.
 
"Mke anataka nyama wakati Hana mawazo ya maana ya kukufanya upate nyama, Hana ushauri wowote zaidi ya lawama. Sisi kina Taikon tunafukuza mchana kweupe akale nyama Kwa Baba yake huko."
 
Nimekuelewa sana mkuuu
 
Back
Top Bottom