Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,267

Akizungumza jana eneo la tukio, Mama mzazi wa mtoto huyo, Stella Hamis alisema juzi saa 2. 00 asubuhi, alimfokea mtoto huyo baada ya kumuona nyumbani badala ya kwenda shule
Stella alisema alimtaka mwanawe aende shule mara moja naye akaelekea Shambani. Hata hivyo alisema, baada ya muda mfupi, mtoto wake huyo alijifungia ndani na kunywa dawa za Hospitalini aina saba tofauti zilizokuwapo na kuandaa kamba kwa ajili ya kujinyonga
"Lakini kwa bahati mmoja wa wana familia, aliingia ndani ya nyumba hiyo na kumkuta mtoto huyo hajiwezi kutokana na dawa alizokunywa", alisema
Stella alisema taarifa zilisambaa kwa jirani ambao walifika eneo la tukio na kumchukua mtoto huyo na kumpeleka Zahanati ya Kijiji kwa matibabu
Ofisa Mtendaji wa Kijiji hicho, Solana Kazikodi, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema Ofisi yake ilipata taarifa mapema juu ya tukio hilo na ndiyo waliofanya kazi ya ziada kuhakikisha mtoto huyo anakimbizwa haraka katika Zahanati yao ya Kijiji
Alisema mtoto huyo alifaulu kuendelea na masomo ya Sekondari baada ya kufanya vizuri kwenye mtihani wa darasa la saba katika shule ya msingi Katani
Hata hivyo, alisema tangu aripoti katika shule hiyo, mahudhurio yake yamekuwa hafifu kutokana na kutopenda kusoma
Mganga wa Zahanati hiyo, Godfrey Manga alithibitisha kumpokea Mwanafunzi huyo na kwamba alipatiwa matibabu na hakuathiriwa kwa kiwango kikubwa na dawa hizo kwa kuwa walimuwahisha Zahanati kupata huduma.
Chanzo: Nipashe