Rukwa: Ahukumiwa miaka 50 jela kwa kumbaka na kumpa mimba Mwanafunzi wa darasa la tano

Matukio ya ubakaji yamekuwa mengi mno....Mabaharia tunafeli wapi..?tunashindwa hata kununua ...na kama hela huna si bora upande mnazi kwa mkono...
 
Mahakama ya Wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa imemuhukumu kwenda jela miaka 50 Ally Kibwe mwenye umri wa miaka 20, Mkazi wa Kijiji cha Ninde kwa kosa la kumbaka na kumpa mimba Mwanafunzi wa darasa la tano katika shule ya Mkilingila.

-----
MAHAKAMA ya wilaya Nkasi mkoani Rukwa imemhukumu kwenda jela miaka 50 Ally kibwe (20) mkazi wa kijji cha Ninde kata ya Ninde wilayani Nkasi kwa kosa la kumbaka na kumpa mimba Mwanafunzi wa shule ya msingi Mkilinga wa darasa tano.

Akitoa hukumu hiyo hakimu mkazi wa mahakama ya wilaya Ramadhani Rugemalila alidai kuwa mahakama yake imejiridhisha na maelezo ya upande wa mashitaka na kumkuta na hatia mtuhumiwa na kwenda kutumikia kifungo jela miaka 50 chini ya kifungu cha 130 (1)(2) (e) ya kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Awali mwendesha mashitaka wa jeshi la Polisi Jemsi Mlawa aliiambia mahakama hiyo kuwa mtuhumiwa huyo alimbaka mwanafunzi huyo wa darasa la Tano kwa nyakati tofauti tofauti na kupelekea kumpa ujauzito mwanafunzi huyo wa miaka 12.

Aliieleza mahakama hiyo kuwa kitendo cha mtuhumiwa kufanya kitendo hicho ni kosa kisheria kifungu cha 60 A (3) cha sheria ya elimu sura ya 353 kama ilivyorekebishwa kwa kifungu cha 22 cha sheria No,4/2016.

Upande wa mashitaka uliiomba Mahakama itoe adhabu kali kwa mtuhumiwa ili liwe ni fundisho kwa wengine na ndipo hakimu wa mahakama hiyo alipotoa adhabu hiyo licha ya utetezi wa upande wa mashitaka kutaka Mahakama imuhurumie kutokana na kwamba hilo ni kosa lake la kwanza kulitenda
[/QUOT kama namuona kijana avumilie ndo ukubwa huo😬lla nyege hizi vijana tuwe makini
 
cutelove kuna uzi wako uliongelea hili suala la wanaume kupenda watoto wadogo, watu waliku kirashi lakini ulikuwa sahihi hebu ona huyu yaliyompata
Mimi ni mmoja ya watu ambao siafiki adhabu kubwa namna hiyo kwa watu wanaotenda makosa kama hayo. Kijana ana miaka 20 tu. Huyu bado ni mdogo sana. Angefungwa miaka saba ingetosha. Napinga adhabu kubwa namna hiyo siyo kwa sababu naunga mkono kitendo alichofanya ila ni kwa sababu ni wananchi wanyonge tu ambao huangukiwa na adhabu kama hizi. Kuna wanasiasa, matajiri na watu maarufu wengi huwa wanatembea na watoto wadogo ila tu wanajua kukwepa mitego ya kukamatika au wakikamatwa wanamaliza mambo bila kujulikana.
 
Back
Top Bottom