kindikwili
JF-Expert Member
- Oct 5, 2016
- 1,862
- 2,876
Umofia kwenu wakuu,
Wakuu habari za muda huu?
Kuna video iko YOU TUBE ikionesha mahojiano ya watangazaji wa XXL ya clouds fm na mwimbaji wa kike RUBY. Katika video hiyo Rubi anaomba radhi wapenzi wa clouds, management na wafanyakazi kwa yote yaliyotokea.
Katika mahojiano hayo kuna mengi unaweza kujifunza ukiwa na jicho la ziada na akili pevu, watangazaji hasa B DOZEN anaonekana kumuuliza Ruby maswali mengi ya kikuda yasiyo ya msingi maana mtu akiamua kuomba radhi si lazima uanze tena kumuuliza maswali yenye lengo la kutaka ku-justify makosa yake. Hata hivyo si kweli kwamba ni Ruby tu ndiye aliyekosa, kwahiyo hakukuwa na haja ya kutaka kuleta mambo kama yale.
Lakini katika mahojiano hayo B DOZEN anasikika akisema waliambiwa wasipige tena nyimba za ruby cjui october mwaka jana (kama sijasahau). Mimi sijui chanzo cha ugomvi wao ila inaonekana Ruby alikosana na management ya THT na na kisha baadaye aliongelea kamati ya FIESTA kwamba inatoa hela kidogo kwa wasanii (kulingana na trend ya mahojiano hayo).
Sasa kama ni hivyo hii amri ya nyimbo za Ruby kusitishwa kupigwa Clouds ulikuwa na mashiko gani?. Yaani clouds ukikosana na Ruge na THT yake ina maana umekosana na kampuni nzima? Ukikosana na kamati ya fiesta tayari umkosana na clouds kama kampuni? Mfano kama zamaradi alikuwa mpenzi wa Ruge kisha wakamwagana ndiyo kusema hapo Zamaradi hatakiwi clouds kabisa na hata kile kipindi chake kinafutwa kisa kakosana na Ruge?. Hivi lady Jaydee yeye alikosana na nani?
Katika business law company is a separate legal entity, ni vizuri Ruge na wenzake wakajua hili. Kwamba clouds media group ni kampuni na ina utofauti na Ruge na Kusaga. Yaani si kwamba ukikosana na kusaga au ruge basi ndiyo uwe umekosana na clouds. Ingekuwa ni hivyo kwenye kila jambo mbona dunia isingekuwa sehemu salama kwa kuishi jamani. Hawa watu waache utoto, mtu akikosana hata kama na bsoi wao waache kuingiza kampuni nzima.
Kuna wakati jirani yetu moja alimuweka mzee wangu ndani (korokoroni) wiki 2, mzee wangu akiwa bado yuko ndani mke wa yule jamaa akawa ameumwa usiku akatakiwa kupelekwa hospitalini, mama yetu alitoa gari na mafuta nikaweka bila kujali kwamba mzee wangu yuko ndani kwasababu ya mumewe.
Ugomvi wa mtu na mtu hauwezi kufanywa ugomvi wa familia kwa watu wastaarabu. Kwa kumalizia naomba nimshauri Ruge aachane na kuingiza mambo yake binafsi, kama mapenzi, ugomvi wake na watu mitaani, au na wasanii wake wa THT, au watangazaji wa clouds na clouds kama kampuni. Hata wengine wenye tabia kama hizi waachane nazo sidhani kama ni ustaarabu.
Kindikwili