RUFIJI, PWANI: Kada wa CCM auawa kwa kupigwa risasi akiwa nyumbani kwake

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
6,042
10,787
Mtu mmoja Aitwae Amri Chanjale (55), mkazi wa kitongji cha Makaravati katika Kijiji cha Umwe Kusini wilayani Rufiji ameuawa kwa kupigwa risasi akiwa nyumbani kwake.

Tukio hilo limetokea jana saa 1.30 usiku baada ya watu wasiojulikana kufika kwake na kutekeleza shambulio hilo.

Marehemu huyo ambaye pia ni mwanachama wa CCM ameuawa ikiwa ni baada ya siku tano kuuawa kwa Mohammed Malinda ambaye nae alikuwa ni mwanachama wa chama hicho.

Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM wilayani Rufiji, Musa Nyeresa amethibitisha kuuawa kwa mwanachama huyo kwa kupigwa risasi.
 
Vyombo vya habari, leo vimeripoti mwananchi mmoja kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), mwenyeji wa kitongoji cha Makaravati, kijiji cha Umwe Kusini, wilaya Rufiji, Amri Chanjale (55), kuuawa kwa kupigwa risasa na watu wasiojulikana jana saa moja na nusu usiku akiwa nyumbani kwake. Aidha habari hizo zimekariri kuwa tukio hili limetokea ikiwa imepita siku tano tu baada ya kuuawa kwa mwananchi mwingine, Mohamed Malinda, naye akiwa kada wa CCM.

Kwa wataalamu wa ulinzi na usalama (Amani) wataona kuwa mauaji haya yanafanyika kwa mpangilio fulani, si kwa kushitukiza wa shaghala baghala. Wanaofanya mauaji haya wanaonekana kuwa si majambazi wa kawaida kama Serikali inavyotaka kuaminisha taifa. Wanaotekeleza mauaji haya wanajaribu kutumia political bearing kutimiza malengo yao. Tunaweza kusema kuwa mauaji haya ni syndicated killings committed by trained snipers. Wauaji watakuwa wanalipwa pesa nyingi na wanaowatuma. Binafsi ninaweza kusema serikali inafanya makosa kuamini kuwa wauji ni majambazi wa kawaida. Hapana. Wauaji hawa wanaonekana kuwa ni kundi kubwa lenye malengo mahsusi yasiyokuwa wazi.

Linaweza kuwa ni kundi ya wafanyabiashara wa mihadarati, wafanyabiashara [sukari?]walioathiriwa na sera za uongozi wa JPM.

Linaweza kuwa kundi la majangili waliokuwa wakifanya biashara ya meno ya tembo, pembe za faru na nyara nyingine za serikali.

Linaweza kuwa kundi la watakatishaji pesa na biashara nyingine haramu waliokuwa wakitumia biashara ya magogo kutoka ukanda huo kutakasa pesa haramu.

Au linaweza kuwa ni kundi la wapiganaji wa Kisomali linafanya majaribio baada ya ku-train asikari wake waliowa-recruit kutoka katika ukanda huo. Tunajua kuwa makundi hayo ya kisomali kwa sasa yanapata shida kutumia ukanda wa pwani ya Kenya kwa uhuru kwa sababu ukanda huo sasa umedhibitiwa.

Iwe ni mojawapo ya makundi na/au sababu zilizoainishwa hapo juu kuwa ndio chimbuko la mauaji yanayofanyika ukanda wa Pwani ya Tanzania, Serikali na hususan vyombo vya ulinzi na usalama vinapaswa kutathmini mbinu wanazotumia iwapo badi ni appropriate kuendelea kutumika kudhibiti uhalifu huu. Serikali inatakiwa kwa sasa kutumia njia za kijasusi za hali ya juu kuwagundua na kisha kuwa-uproot wahalifu hawa. Njia za polisi kwenda na magari kupitia vituo vya polisi au kuongeza idadi ya polisi katika vituo vya maeneo kunakofanyika vitendo vya mauaji wa raia wasiokuwa na hatia, ninafikiri, kwa uwelewa wangu, kuwa havitafua dafu.

Hawa wauaji hawa wamejiandaa na inaelekea wanashauriwa na political intellectual guru. Wanajaribu kutumia political grudges za vyama vya upinzani ili kuyapa mauaji political leverage. Tunakumbuka mwezi Marchi yaipoua askari polisi kule Kibiti yalifikia hata hatua ya kushangiliwa na wananchi kwa kuwaruhusu wachukue mkaa na mbao bure kutoka kituo cha udhibiti wa mazao ya misitu na mali asili.

Wazee wa kwetu husema: 'Bagambila balinsi......'
 
Serikali kupitia jeshi la Polisi na Tiss watumie intelligency technics kama kutuma askari wapelelezi kupata information. Ikiwa kuanzisha makazi kwa wapelelezi katk kulishughulikia suala hili.
 
Duh

R.I.P

Naona jeshi la polisi badooo kabisa katika kutatua kinachoendela huko.
Sijui wanafanya nino huko.... na Waziri nae kimya kama vile haya uisha mara moja. Ina maana hawajatatua kitu...Kuna uwezekano mkubwa ni njia ya watu kuisumbua serikali ya JPM kwa matukio haya ambayo yanatendeka karibu na Dar.
 
Tatizo serikali haishauriki.wameambiwa wakae na wananchi.wajadiliane.hawataki.
 
Back
Top Bottom