Rufaa ya Zombe Kusikilizwa Kesho

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
MAHAKAMA ya Rufani kesho inatarajia kusikiliza rufaa dhidi ya Mkuu wa Upelelezi wa mkoa wa Dar es Salaam (RCO) wa zamani Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Abdallah Zombe na askari wenzake wanane, anaandika Faki Sosi.

Mkurugenzi wa mashtaka (DPP) alikata rufaa hiyo namba 358 ya mwaka 2013, akipinga Zombe na wenzake kuachiwa huru na Mahakama Kuu katika kesi ya mauaji ya watu wanne iliyokuwa ikiwakabili.

Rufaa hiyo imepangwa kusikilizwa leo Mahakama ya Rufani na jopo la Mmjaji watatu ambano ni Bernard Luanda, kiongozi wa jopo, na wengine ni Jaji Sauda Mjasiri na Jaji Semistocles Kaijage.

Mbali na Zombe, wajibu rufaa wengine ni ASP Christopher Bageni, ASP Ahmed Makelle, Konstebo Jane Andrew, Konstebo Emanuel Mabula, Konstebo Michael Shonza, Koplo Abeneth Salo, Koplo Rajabu Bakari na Koplo FestusGwabisabi.

Katika rufaa yake, DPP anapinga hukumu ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, iliyowaachia huru wajibu rufaa hao katika kesi ya msingi ya mauaji, kwa madai kuwa Jaji alikosea kuwaachia huru kwani kulikuwa na ushahidi wa kutosha kuwatia hatiani wote.

Awali Zombe na wenzake walikuwa wakidaiwa kuwaua kwa makusudi wafanyabiashara watatu wa madini kutoka Mahenge Morogoro na dereva mmoja wa teksi.

Wafanyabiashara hao Sabinus Chigumbi, (Jongo) na ndugu yake Ephrahim Chigumbi. Mwingine ni Mathias Lunkombe na Juma Ndugu, ambaye alikuwa dereva teksi mkazi wa Manzese Dar es Salaam.

Watu hao waliauawa Januari 14, 2006, katika msitu wa Pande uliopo Mbezi Luis, Dar es Salaam, na ilidaiwa kuwa walikamatwa na washtakiwa hao wakiwa ha, eneo la Sinza.

Mahakama Kuu katika hukumu yake iliyoteolewa na Jaji Salum Massati Agosti 17, 2009iliwaachia huru washtakiwa wote baada ya kuwaona kuw ahawana hatia kwa makosa yaliyokuwa yakiwakabili na kwamba upande wa mashta ulishindwa kuthibitisha makosa hayo kwa washtakiwa bila kuacha mashaka.

DPP hakuridhika na hukumu hiyo na mwaka huohuo (Oktoba 6, 2009), alikata rufaa Mahakama ya Rufani, akipinga hukumu hiyo ya Mahakama Kuu.

Alikuwa akidai kuwa Jaji Massati alikosea kuwaachia huru washtakiwa hao, na kwamba kulikuwa na ushahidi wa dhahiri na wa kimazingira wa kutosha kuwatia hatiani washtakiwa wote.

Rufaa hiyo hata hivyo ilitupiliwa ambali na Mahakama Mei 8, 2013 kutokana na dosari za kisheria zilizobainika kwenye rufaa hiyo, lakini baadaye DPP alipeleka maombi Mahakama Kuu aruhusiwe kukata tena rufaa hiyo nje ya muda, ambapo Mahamaka Kuu ilikubalia maombi yake.
 
inauma sana watu waliitwa majambaka wakabakwa roho zao, wakipatikana na hatia wafungwe tu kwani damu bado inawalilia na watoto wao wamekosa faraja ya wazazi wao
 
Kwanza Zombe bado yupo nchini? Maana muda mfupi tu baada ya hukumu yake tuliambiwa kuwa amepita Hivi!!! Ila Ok! Kama majaji nao wanaenda na kasi ya magufuli ndiyo tutaona wakati huu! Japo majaji wote wa upande wetu ni wale wa Form 1! Yaani majaji wa viwango vya chini,
 
Kwanza Zombe bado yupo nchini? Maana muda mfupi tu baada ya hukumu yake tuliambiwa kuwa amepita Hivi!!! Ila Ok! Kama majaji nao wanaenda na kasi ya magufuli ndiyo tutaona wakati huu! Japo majaji wote wa upande wetu ni wale wa Form 1! Yaani majaji wa viwango vya chini,

Zombe yupo,but now kafulia mbaya
 
Mungu isaidie serikali ishinde kesi hiyo kwani Zombe Na wenzake wamewauwa hao watu bila hatia
 
Madawa waliokuwa wanatumia ili aepuke huo msalaba yameshaaisha sasa lazima wakanyee ndo pumbavu
 
Kwanza Zombe bado yupo nchini? Maana muda mfupi tu baada ya hukumu yake tuliambiwa kuwa amepita Hivi!!! Ila Ok! Kama majaji nao wanaenda na kasi ya magufuli ndiyo tutaona wakati huu! Japo majaji wote wa upande wetu ni wale wa Form 1! Yaani majaji wa viwango vya chini,
Kama magu anabyotumbua wakati yeye Ni jipu, ndivyo majaji wala rushwa wanvyoenda kusinamia mahakama ya mafisadi
 
Zombe na genge lake wanyongwe tu ni hasira polisi basi tu huwa nashindwa kujizuia kabisa hawa watu hawa siku nikifa nikakuta polisi yuko mbinguni nitakata rufaa kwa muumba anitenganishe na hawa wanyama kasoro mikia
 
Back
Top Bottom