Rufaa ya Sioi yatinga NEC


Mkuu FJM, shukrani kwa maelezo ya kina ambayo yametuelimisha wengi juu ya mambo ya uraia na sheria zake.

Hii ndo raha na faida ya JF, ni kisima cha elimu.
 
Kama hujui sheria kuhusiana na uraia wa Tanzania inasemaje si unakaa kimya ndugu ya nini kujiaibisha na maneno mengiutafikiri unaelewa kumbe hamna kitu.kama kitu hujui unauliza si lazima uchangie hapa au unaongeza idadi ya post zako JF?

Sasa wewe "UNAYEJUA" mbona huelezi hicho unachokijua insteady unatoa SWEEPING & INCOHERENT statement like a intoxicated madman!
 

watampaisha bila wao kujijua. tusubiri tuone. wengi tunakumbuka jinsi WENJE wa Mwanza alivyowekea pingamizi la namna hiyo na MASHA matokeo yake ndo walivyosaidia kumtangaza kwa wananchi na mwisho akashinda
 
Ngongo naomba nikujibu pamoja na Politiki.

... Ndiyo Uraia wa Sioyi utaamuliwa kwa kufuata SHERIA za Tanzania. Lakini pia utaangalia sheria za URAIA wa Kenya alikozaliwa HASA Kabla ya Katiba mpya.
Mkuu acha kupotosha, uraia wa Tanzania unaamuliwa kwa sheria za Tanzania, si za Kenya wala nchi nyingine yoyote. Vinginevyo tungekuwa na raia wa Tanzania ambao katiba ya Tanzania haiwatambui lakini katiba za nchi ya nje inawatambua, jambo ambalo lingekuwa ni vurugu. Ukitaka kuamini kwamba uraia wa Tanzania unaamuliwa kwa sheria za Tanzania wala si za nchi nyingine, ujiulize kwa nini Uhamiaji wakifukuza mtu nchini huwa hawamwambii nchi ya kwenda, ila wanachojali aondoke Tanzania!!
 

kuongezea hapo timu zinanapocheza mpira wanategemea defender wa timu pinzani atakosea na wao kufunga kirahisi,kwenye siasa kuna kamati ya ufundi kazi yake ni kutafuta makosa na chance kama hizo
 

Mkuu FJM,

Naheshimu mchango wako maana umeenda shule. Umesoma vifungu mbalimbali na kuviandika kwa lugha nyepesi. Hiyo ndiyo JF ya zamani ambayo wengi tulikuwa tunajivunia kuwa sehemu yake. Ambapo watu walikuwa wanaingia chini kusoma na kuelewa na kisha kutufundisha sisi sote hapa.

Ninapingana na wewe kwenye tafsiri hiyo ya kwamba mtoto akizaliwa nje ya nchi na wazazi wote wawili au mmoja Mtanzania basi serikali ya TZ kwa miaka 18 ya mwanzo inamtambua kama ana uraia wa nchi mbili. Kwa mawazo yangu naona hilo sio sahihi. Ukitaka kuona sio sahihi angalia form ya kiapo ambayo iko kwenye act hiyo hiyo ya uraia ya 1995. Unapoapa lazima utaje nchi nyingine ambayo una uraia wake. Sasa kama huna na hujawahi kuwa na uraia wa nchi nyingine, utataja nini?

Sheria yoyote hapa duniani ni ngumu ku cover scenarios zote na ndio maana kunakuwa na mahakama za kutafsiri sheria. Hapa muhimu ni kurudi nyuma na kuangalia je waliotunga hii sheria walikuwa wanataka ku achieve nini? Ukisoma documents zote unagundua lengo lao lilikuwa kuzuia Mtanzania kuwa na uraia wa nchi nyingine kwa kujua au kutokujua. Na njia kubwa ya kupata uraia wa nchi nyingine waliainisha kama kupitia mzazi mmoja kuwa wa hiyo nchi nyingine au kuzaliwa kwenye hiyo nchi nyingine. Hapo ndipo suala lote hili linapotakiwa kukaa.

Ninaamini kabisa hawakuwa na lengo la kuwalenga watu kama akina Siyoi. In fact tafsiri ya sasa ya kifungu hiki ni faraja kwa Watanzania wengi sana hasa wale wanaoishi sehemu za mipakani. Mkuu, mimi nataoka wilaya ya mpakani na ninaelewa hili jambo likiangaliwa kisiasa litaleta usumbufu kwa watu wengi sana. Kule mipakani ni kawaida watu wa upande mmoja kwenda kutibiwa upande mwingine kutegemeana na ubora wa huduma za sehemu hiyo nyingine. kwa mfano kati ya Tanzania na Malawi, kuna kipindi huduma za Malawi zilikuwa bora zaidi, Watanzania wengi wa Kyela walikuwa wanaenda kutibiwa huko ikiwa na pamoja na hata kujifungua. Hivyo hivyo kuna kipindi watu wa Malawi walikuwa wanakuja TZ kutibiwa.

Ukiachia hiyo, angalia wafanyakazi wote waliokuwa wanafanyakazi kwenye jumuia ya Afrika Mashariki. Kulikuwa na maelfu ya watanzania waliopelekwa kenya au Uganda kikazi. Kuna wengine walizaa watoto wao huko na kurudi TZ watoto wao wakiwa wachanga. Kuna wengi wao wamekufa na si ajabu hata watoto hawajui walizaliwa Kenya au Uganda. wanachojua Wazazi wao wote wawili walikuwa Watanzania.

Ndio maana tokea mwanzoni na mpaka sasa binafsi naamini tafsiri iliyotolewa na mkuu wa uhamiaji ndio sahii na ndiyo ilikuwa lengo la kutungwa kwa sheria hii. Kama umezaliwa nje na wazazi wote wawili ambao ni Watanzania basi sharti pekee liwe kuangalia kama wakati unazaliwa je hiyo nchi ulikozaliwa ilikuwa inatoa uraia automatically?

haya majadiliano yatakuwa na maana kama kuna watanzania wenzetu watajifunza na kuzuia mikanganyiko kama hii.
 

yote lazima yaende sambamba ili kuwadhoofisha kotekote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…