Rufaa ya Sabaya na wenzake yaanza kusikilizwa

peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
12,829
21,460
Arusha. Mahakama Kuu Kanda ya Arusha leo imeanza kusikiliza rufaa ya kupinga kuachiwa huru aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya na wenzake watano.

Rufaa hiyo imekatwa na upande wa Jamhuri dhidi ya Hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, iliyowaachia huru.

Juni 10, 2022 Sabaya na wenzake sita walishinda kesi ya uhujumu uchumi na kuachiwa huru baada ya mahakama hiyo kubaini ushahidi uliotolewa na Jamhuri ulighubikwa na utata hivyo kushindwa kuthibitisha mashtaka yaliyokuwa yanawakabili na kuwatia hatiani.

Leo Jumanne Desemba 13 Mahakama Kuu Kanda ya Arusha ilipanga kuanza kusikiliza rufaa hiyo baada ya jana kushindwa kusikilizwa kutokana na Sabaya kuieleza mahakama kuwa hana wakili na alikuwa alipata wito wa mahakama jana asubuhi na hakujua anakuja kufanya nini mahakamani hapo.

Mbali na Sabaya wajibu rufaa wengine ni Enock Mnkeni, John Aweyo, Sylvester Nyegu, Jackson Macha na Nathan Msuya.

Leo waomba rufaa wanawakilishwa na mawakili wa serikali waandamizi Patrick Mwita, Abdallah Chavula, Hebel Kihaka, Felix Kwetukia na Timotheo Mmari.

Wajibu rufaa wanawakilishwa na mawakili Mosses Mahuna, Sylvester Kahunduka, Fridolin Bwemelo na Fauzia Mustapha.

Mbali na Sabaya leo mjibu rufaa mwingine ambaye amekuja mahakamani ni Nyegu ambaye anawakilishwa na wakili Kahunduka huku Sabaya akiwakilishwa na mawakili wengine watatu.

Mbele ya Jaji Salma Maghimbi anayesikiliza rufaa hiyo namba 155/2022 wakili Mwita ameileza mahakama kuwa jana walipokea notisi ya pingamizi la awali kwa wakili Mahuna anayemwakilisha Sabaya.

Hoja za pingamizi hilo la awali zinaanza kuwasilishwa na wakili Mahuna.

Aidha katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 27/2021 iliyotolewa hukumu na mahakama hiyo ya chini, aliyekuwa mshitakiwa wa tatu katika kesi hiyo (Watson Mwahomange) hajajumuishwa katika rufaa hiyo.

Mwananchi
 
Utawala wa shetani,Jezebel..wachawi hawafi mapema ila watu wema huondoka mapema,hata Yesu kristo ameondoka akiwa na miaka 33,nabii Musa akiwa na miaka 40,wachawi na wenye roho nyeusi hawaitajiki kwa Mungu..
Watu wabaya Mungu anawasusa na shetani anawasusa ndio maana wanaishi muda mrefu.
Siku hizi 120 ndo 40 mpya?
 
Una uhakika Nabii Mussa aliishi miaka 40. Yesu alikuja kwa jukumu la muda mfupi ndio maana aliishi miaka michache, ingawa alalifufuka.
 
Huyo ni takataka tu kwa ushenzi aliofanya enzi ya utawala wa dhalim huyu jambazi hastahili kuwa uraiani afungwe kifungo cha maisha jela na kazi ngumu.
 
Moja ya mambo yanayoitia aibu awamu hii ni suala la kuendelea na hii kesi mpaka leo. Wanashindwaje kumhukumu kumnyonga kama hawamtaki. Mnaonekana hamkujipanga mlipofungua mashtaka mwisho wa siku mtakuja mlkumfanya awe maarufu sana
 
Back
Top Bottom