Rufaa ya Ole Sabaya kutajwa Desemba 13

Rufaa ya Ole Sabaya kutajwa Desemba 13

Kinuju

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2021
Posts
2,384
Reaction score
5,330
Jaji wa mahakama kuu amesema rufaa ya aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai kisha kusingiziwa ameiba simu aina ya Tecno na pesa laki tatu na sitini na kufungwa miaka 30 jela Lengai Sabaya itaanza kusikilizwa 13/12/2021 mfululizo mpaka haki itakapopatikana.
===

Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Butamo Philip anatarajiwa kuanza kusikiliza rufaa ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili.

Arusha. Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Butamo Philip anatarajiwa kuanza kusikiliza rufaa ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 16, 2021, Wakili Edmund Ngemela anayemwakilisha mleta rufaa wa pili, Sylvester Nyegu amesema rufaa hiyo imepangwa kutajwa Desemba 13 mwaka huu mbele ya Jaji Philip.

Amesema rufaa hiyo namba 129, 2021 imetokana na shauri la jinai namba 105 la mwaka huu, ambapo mshitakiwa mwingine katika shauri hilo alikuwa ni Daniel Mbura.

Sabaya na wenzake wawili walihukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kila mmoja, Oktoba 15 mwaka huu baada ya kukutwa na hatia katika makosa matatu likiwamo unyang'anyi wa kutumia silaha.

"Tunashukuru tumeshapata nyaraka zote na imeshasajiliwa na kupangiwa Jaji wa kusikiliza.Tuna sababu zaidi ya 10 za kukata rufaa hii," amesema.

Oktoba 18, 2021 Wakili Mosses Mahuna anayemwakilisha Sabaya aliwaeleza waandishi wa habari nje ya mahakama kuwa, wamewasilisha notisi ya nia ya kukata rufaa.

Wakati rufaa hiyo ikisubiriwa kuanza kusikilizwa, Sabaya na wenzake sita wanakabiliwa na kesi nyingine ya uhujumu uchumi inayoendelea kusikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.

Leo Jumanne Novemba 16, 2021 katika kesi ya uhujumu uchumi namba 27 ya mwaka huu shahidi wa tisa wa Jamhuri, Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Kwa Mromboo, Mary Kimasa ametoa ushahidi wake wa msingi.

Akiongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Tarsila Gervas shahidi huyo ameieleza mahakama namna namna alivyofika benki Januari 22, 2021 na kukuta mteja wao ambaye ni mfanyabiashara Francis Mrosso akitaka kutoa Sh90 milioni.

Ameieleza mahakama kuwa kutokana na mteja huyo kutokuwa na desturi ya kutoa kiasi kikubwa kama hicho cha fedha alilazimika kumhoji kwanini anatoa fedha hizo ambapo Mrosso alimweleza ana mtu anatakiwa kumlipa kiasi hicho cha fedha.

Wakati shauri hilo likiendelea upande wa utetezi wakiongozwa na Wakili Mosses Mahuna, waliwasilisha pingamizi kupinga kupokelewa kwa nyaraka tatu ikiwemo benki statement ya Mrosso na nakala halisi ya bank slip iliyotumika kutoa kiasi hicho cha fedha.

Hakimu Mkazi Patricia Kisinda aliahirisha kesi hiyo hadi kesho Jumatano atakapotoa uamuzi mdogo juu ya pingamizi hilo.

Katika kesi hiyo watuhumiwa wengine ni Enock Mnkeni, Watson Mwahomange, John Aweyo, Sylvester Nyegu, Jackson Macha na Nathan Msuya.

Mwananchi
 
Atachomoka.Uhuru wake unakuja muda si mrefu.
 
Hivi mataga mna akili sawa? Laana ya Magufuli inaweza kumpata nani, kivipi!

Halafu, Kikristo laana ni kitu hakiruhusiwi

Acheni huo upumbafu wa kusema laana ya Magufuli itampata Rais Samia...

Mataga mnataka Nini? Semeni shida yenu msaidiwe
 
Jaji wa mahakama kuu amesema rufaa ya aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai kisha kusingiziwa ameiba simu aina ya Tecno na pesa laki tatu na sitini na kufungwa miaka 30 jela Lengai Sabaya itaanza kusikilizwa 13/12/2021 mfululizo mpaka haki itakapopatikana...
Bado hujaelewa kuwa uchawa wa aina hiyo hautakiwi, au wewe ndiye uliye kuwa shahidi na mtumishi wake wa ndani?
 
Sawa atatoka lakini anatakiwa kwenda kushonwa kuziba pengo la kutolea kinyesi
 
Back
Top Bottom