RUFAA YA KAFULILA: MPAMBANO UNAENDELEA TABORA
Mahakama ya rufaa imekubaliana na pingamizi la mawakili wa serikali kwenye kesi ya Kafulila kuwa Notice yake ilikuwa na kasoro hata hivyo haiondoi haki yake ya rufaa na hivyo ili rufaa iendelee anapaswa kuingiza notice upya.
Nikama wakati ule mahakama kuu ilivotakiwa kuandika upya hati za viapo na kesi kuendelea. Hivyo kesho Mhe. Kafulila ataingiza maombi ya kuingiza upya Notice hiyo kwa maelekezo hayo ili kesi iendelee katika ratiba ya mwezi ujao.
Rufaa hii ni ya kupinga Hukumu ya Mahakama Kuu iliyotolewa May17, 2016 na Jaji F. Wambali ambaye wiki chache baada ya hukukumu hiyo aliteuliwa kuwa Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu Tanzania
Msingi wa rufaa hiyo ni kwamba Mahakama Kuu ilikataa kuweka wazi fomu za tume za matokeo zilizokuwepo mahakamani ili kubaini mshindi.
Kwa mujibu wa madai ya Kafulila fomu hizo za tume zilizokuwa mahakamani yeye ndiye anaeongoza kwa kura 34000 dhidi ya mgombea wa CCM 32000. Hata hivyo Jaji alikataa fomu hizo kuwekwa wazi
Katika hatua ya rufaa, Jaji aliyehukumu kesi hiyo aliendelea kuelekeza fomu hizo zisitolewe kwa mujibu wa barua ya Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Tabora
Hata hivyo, Jaji Mkuu Othuman Chande hatimaye alielekeza fomu hizo 21B ziwe wazi na Kafulila apewe nakala husika ili afanikishe rufaa yake.
Hivyo mpaka sasa Kafulila alikabidhiwa fomu hizo na Msajili wa Mahakama ya rufaa kwa maelekezo ya Jaji Mkuu na msingi wa rufaa yake ni Mahakama ya rufaa izitumie fomu hizo za tume za kila kituo zilizopo mahakamani kuamua mshindi.
Aumuzi wa leo sio mwisho wa kesi na sio hukumu ya mwisho kwani Mawakili wa Mhe Kafulila wanaweza kurekebisha kasoro hiyo ili Mahakama ya rufaa ifikie maamuzi kwa msingi wa kujua ukweli kuhusu nani aliyeshinda kwa mujibu wa fomu hizo za matokeo zilizopo mahakamani na Kafulila kuwa na nakala.