s
sijasoma mkuu nisaidie wanasemaje
Nashindwa kuliweka hapa, lakini kwa kifupi.
RUFAA VYETI NDIO BASI
Na Nasra Abdallah
Unaweza kusema watumishi wa umma waliokutwa na vyeti feki kisha kukata rufaa, hatma yao kurudi kazini ipo shakani.
Utata huo unatokana na serikali kushindwa kutangaza matokeo ya rufaa zao huku ikitangaza ajira lukuki kuziba nafasi zilizoachwa wazi na watumishi waliong'olewa kwa kukutwa na vyeti feki, bila bila kujali kwamba baadhi yao waliondolewa kimakosa.
Hadi jana serikali imeshindwa kutangaza matokeo ya rufaa zao kama ilivyoahidi kufanya hivyo juni 30, mwaka huu.
Majibu yaliyotolewa jana na waziri mwenye dhamana na utumishi wa umma, Angela Kairuki, yaliongeza giza na utata juu ya hatma ya watumishi hao waliokata rufaa huku wengi wao wakiwa na imani ya kurudishwa kazini.
Waziri Kairuki alipoulizwa na gazeti hili ili kujua nini kimesababisha ukimya wa hatma ya rufaa za watumishi hao, alijibu kwa kifupi kuwa mchakato wa kupitia rufaa zao haujakamilika na utakapokuwa tayari umma utajulishwa.
Alipoulizwa kama mchakato haujakamilika kwa nini wametangaza ajira mpya:"Ndugu mwandishi nimekuambia kuwa tukishakuwa na taarifa zote kuhusu suala hilo tutawaiteni, kwa sasa sina majibu yoyote kwa hayo unayoniuliza naomba unielewe.
KWA KIFUPI NI HAYO, ZAIDI TAFUTA GAZETI USOME.
Lakini kama habari yako ni ya uhakika ni vyema sana