Brother James
JF-Expert Member
- Feb 21, 2012
- 234
- 173
Barriadi, Simiyu.
Ni wiki ya tatu sasa tangu niingie Bariadi, kitu kimojawapo nilichogundua (katika shughuli zangu za utafiti) ni uwepo wa uvunjifu mkubwa wa sheria za barabarani hapa Bariadi ambapo ni makao makuu ya mkoa wa Simiyu tena unaofanywa na Traffic Officers.
Mji wa Bariadi una vyombo vya usafiri vichache sana, magari yanahesabika barabani. Usafiri kuzunguka mji wa Bariadi ni pamoja na Baiskeli, Pikipiki na Bajaj. Usafiri wa tax, kwa bariadi nzima kuna tax 3 tu na vijidaladala vichache vinavyobeba abiria kutoka vijijini kuja Bariadi mjini.
Pamoja na mambo mengi sana ninayoendelea kuyafanyia utafiti kwa upande wa shughuli za usafirishaji, leo naomba nijikite zaidi katika usafiri (Bajaj) kuzunguka mji wa Bariadi mjini.
Bajaj ndio usafiri maarufu hapa Bariadi mjini kwa mizunguko ya hapa na pale lakini Waendesha Bajaji wamekuwawakipata adha za hapa na pale katika shughuli zao hususani usumbufu mkubwa kutoka kwa Traffic officers wa Bariadi ambao wao pia wanakiri kwamba kinachofanyika ni maagizo kutoka ofisi ya RTO.Bariadi. Wengi wa waendesha Bajaj hawana elimu ya darasani, elimu ya udereva, hawajui sheria na haki zao ndio maana wamekuwa watoaji rushwa wazuri sana kwa Traffic officers kwa sababu nimeambiwa kuwa mara nyingi wakikamatwa na kosa lolote Bajaj ikifika Kituo cha Polisi basi Makosa huongezeka maradufu na ndio maana Madereva hawa hulazimika kuhonga matrafiki ili wasifikishwe kituo cha polisi na jambo hili hata mmoja wa matrafiki (jina limehifadhiwa) kakiri kwa uwazi kabisa anasema ni kwa sababu madereva wengi hawajitambui ndio maana wakifika kituo cha polisi wanabambikiziwa makosa, "hawa madereva hawana elimu ya kutosha juu ya haki zao na sheria hawazijui kwa sababu kuendesha Bajaj wamejifunzi mtaani na wengi wao hata leseni hawana hivyo akipelekwa kituoni na kosa moja lazima atakutwa na makosa mengineyo hata matatu na kila kosa atalipia 30,000'' mwisho wa kumnukuu. Kwa kauli hiyo ya afande ndio maanamadereva wengi hulazimika kuhonga kila wasimamishwapo na trafiki kuogopa kupelekwa kituoni;kifupi wamejengewa uwoga ambao umepanua ongezeko la rushwa. Bajaj zimekuwa zikiwaingizia pesa (rushwa) nyingi sana za matumizi Matrafiki hawa kwa sababu makosa kama kukosa fire extinguisher, side mirror, kupakia abiria wanne, kupaki pembezoni mwa barabara, kukosa leseni, plate number za zamani, etc. na hawana msamaha aidha mpaka ukalipie kituo cha polisi au utoe rushwa.
Kitu kingine kipya kwangu nilichokiona ni pale Dereva wa Bajaj anapokamatwa kwa kukosa mikanda ya abiria katika bajaj zao. Nimezunguka sana nchi hii kwa kweli sijawahi kukutana na utaratibu wa mikanda ya dereva na abiria katika Bajaj; na kwa sababu karibia Bajaj zote hapa Bariadi hazina hiyo mikanda basi Trafiki wamekuwa wakijiingizia kipato (rushwa) kupitia kosa la mikanda. Wenzetu (wenye ufahamu wa sheria za usafirishaji) mtatusaidia kufafafanua juu ya mikanda katika Bajaj. Suala la mikanda kuwa geni na gumu basi mara nyingi madereva wamekuwa wakifanya kazi zao kwa kujificha ficha na kwa taarifa nilizopewa na katibu wa waendesha Bajaj Bariadi ni kwamba haya makosa yanapelekea madereva wengi sana kushindwa kurejesha mauzo kwa wamiliki wa Bajaj na mwisho wake wananyang'anywa bajaj na kupewa mtu mwingine.
MY TAKE:
Haya yote yanafanywa na trafiki ambao wapo chini ya RTO wa Simiyu na kwa taarifa nilizopata ni kwamba RTO yeye ndio kichocheo cha haya mambo kwa sababu mara nyingi viongozi wa waaendesha bajaj wamekuwa wakipeleka malalamiko yaokatika ofisi ya RTO lakini wamekuwa wakiambulia Patupu. Nilipotembelea ofisi zaRTO ili kupata maelezo yao juu ya haya yafanywao na matrafiki, kila trafiki alijibu kuwa yeye si msemaji wa hayo mambo mpaka RTO mwenyewe, bahati mbaya sana mpaka naandika ujumbe huu nimeshindwa kumfikia RTO ili ajibu hizi tuhuma.
Pia kwa sababu imebainika kwamba hawa Madereva wa Bajaj wanaonewa hivyo kwa sababu wao ndio chanzo pekee kikubwa cha vipato vya trafiki (baada ya kukosekana vyombo vingine vya usafiri) basi niishauri ofisi ya RTO Simiyu kupunguza idadi ya matrafiki mkoani Simiyu na kupelekwa kwenye uhitaji vinginevyo uwingi wao pasipo na kazi huchocheo rushwa za hovyo kama hizo nilizozitaja.
Niiombe POLICE TANZANIA (IGP) kuliona hili jambo na kulijibia mara moja kama sio kubadilika moja kwa moja kwani wananchi wamekuwa wakipokonywa ajira zao na Maboss wao na kupelekea ugumu wa maisha kwa sababu yao; na hii hupelekea watu wengi kuwachukia trafiki na kuwaona kama sio watu wema.
Imeandikwa na;
CHACHA JAMES
jameschacha@gmail.com