RPC wa Mwanza awashauri Viongozi wa Chadema wafike Ofisini kwake ili aweze kuwasaidia warejeshewe Simu zao zaidi ya 15

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,915
141,875
Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza amewataka viongozi na wafuasi wa Chadema wanaodai simu zao zinashikiliwa na polisi kwa zaidi ya miezi 5 sasa wafike ofisini kwake aweze kuwasaidia.

Akiongea na mwandishi wa Eatv kamanda Hamis alisema hana taarifa za kushikiliwa kwa simu hizo zaidi ya 15 zote Smartphones na kwamba kama ni kweli basi waende ofisini.

Viongozi na wafuasi hao wa Chadema walikamatwa na polisi baada ya kufanya mkusanyiko usio halali ndani ya Kanisa Katoliki na kesi yao bado haijaanza kusikilizwa mahakamani tangia October, 2021.

Watuhumiwa wote wako nje kwa dhamana.

Source: Eatv habari

Maendeleo hayana vyama.
 
Sasa itakuwaje kama GPO haizingatiwi,wakati wa ukamataji Mali,SI zitakuwa zingine hatakufa zilisha kufa kwani wengine watakuwa wamesha zigawa Kwa hawara.🤸
 
Akili zimeanza kuwarudia polisi baada ya kuathirika kwa muda mrefu na Umagufuli. Kesi ya akina Mboye imewafundisha kwa kina kuhusu "custody of chain" na pia umuhimu wa PGO.
 
Bila shaka elimu inaendelea kuwakaa mabadiriko yanafanyakazi umungu mtu unaondoka polepole. Rais wetu asifiwe, aombewe na Mungu atamlinda daima.
 
Akiongea na mwandishi wa Eatv kamanda Hamis alisema hana taarifa za kushikiliwa kwa simu hizo zaidi ya 15 zote Smartphones na kwamba kama ni kweli basi waende ofisini.

Tuna viongozi bure kabisa...

Sasa hata taarifa hana, halafu anatoa wito wa wahanga kufuata simu zao...
 
Back
Top Bottom