Mwanantogakulya
Senior Member
- Mar 18, 2025
- 130
- 118
Kamanda wa polisi mkoa wa Simiyu,Edith Swebe(ACP)amewaonya walinzi shirikishi Sungusungu mkoani humo kuacha mara moja tabia ya kujichukulia sheria mkononi.
Onyo hilo amelitoa wilayani Itilima na kamanda wa polisi mkoa wa Simiyu, alipokuwa akizungumza na vikundi vya ulinzi shirikishi katika wilaya hiyo,”
Amesema kuwa ingawa jeshi hilo ni sehemu ya mifumo ya jadi ya ulinzi inayotambuliwa na jamii, hawaruhusiwi kuwachukulia hatua watu bila kufuata taratibu za kisheria.
“Tunakiri mchango wa Sungusungu katika kudumisha amani vijijini, lakini tunawakumbusha kuwa hakuna mtu aliye juu ya sheria,”
“Mtu akituhumiwa kwa kosa lolote, ni wajibu wenu kumfikisha kwenye vyombo vya dola, si kumpiga au kumwadhibu mtaani,” amesema.
Amesema vikundi hivyo vya ulinzi shirikishi likiwemo jeshi hilo la jadi vinatambulika kisheria hivyo viongozi wa vikundi hivyo wanatakiwa kusimamia kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu pamoja na miongozo ya nchi.
Baadhi ya wananchi wakitoa maoni yao amesema ni vizuri kwa serikali kutoa mafunzo rasmi kwa wanajeshi wa jeshi hilo la jadi ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria na bila kuvunja haki za binadamu.
Jeshi la jadi la Sungusungu limekuwa likitekeleza jukumu la kulinda usalama katika maeneo mbalimbali ya vijijini, hasa maeneo yenye uhaba wa askari wa polisi, lakini limekuwa likikumbwa na malalamiko ya matumizi ya nguvu kupita kiasi.