Rpc Shana na mauaji

Rpc Shana na mauaji

Bado sana, maybe hiyo nchi kama tunaiota tuu,
 
We wasema hivyo...ungekuepo eneo la tukio ndio ungejua nini kilikuwa kinaendelea.

Polisi wamewaua hao majambazi wawili wakiwa katika harakati za kujihami kwa njia ya kujibizana risasi na hao majambazi.

Polisi wangeuwawa sijui hapo ungesemaje. Ungepongeza majambazi au ungesema polisi wanaume wa dar?

Kama umewahi kuvamiwa na kuibiwa na kuuliwa ndugu zako au familia yako sidhani kama ungethubuti kusema unayo yasema.

Acha polisi wafanye kazi yao we tulia kula ugali na pambana na hali yako.

ASANTE
Anaropoka tu, utadhani alikuwepo eneo la tukio, mbona hawajaenda kumuua yeye?
 
jamani mnapotoa mada muwe mnafikiria kwanza halafu mtoa mada inaonekana anataka kuangalia watu wata comment vipi,hivi kweli unapambana na jambazi lina silaha utalibembeleza eti jamabazi njoo nikukamate?/si una taka kufa wewe?? ngoja siku yakutembelee hata panya road tu uone shughuri yake
 
Unakuwa judgemental as if hao waliouawa wamethibitika kufanya huo ujambazi unaodaiwa!
Siku na wewe ukigombania hawara na polisi kisha akakufumania guest house uko naye akakutwanga risasi na kukubatiza ujambazi, ndipo utatia akili kama utanusurika kifo!
unanipa mashaka kwa unachokitetea hapa, inawezekana na wewe ni mmoja wa hao watu au upo kwenye network ya hizo shughuli, hivyo unatafuta sympathy hapa.., achana na hizo mambo nakushauri mkuu, Police wanajua wanachokifanya ikifika sehemu na wao wanaona maisha yao yapo hatarini na mhalifu ana siraha kama yake unadhani anamkamataje? au tukupe wewe kazi ya kumkamata jambazi mwenye siraha ya moto!
 
Haya mambo ya kiusalama yaache kama yalivo mkuu. Kama hujui undani wake unaweza kudhani wameonewa .
Nashauri waachie wenye mamlaka.
 
Haya mambo yana mengi nyuma ya pazia,usiombe yakukute,OVA
 
Huwa anakamata wahalifu hasa hasa matapeli na vibaka ambao hawatumii silaha za moto.

In short jambazi sio mtu wa kumkamata..ukimwona kavamia anatumia silaha hamna mjadala mpige risasi maana ukizubaa anakuua...

Rejea mauaji ya kibiti ndgu vile askari walivyokufa na raia wasio na hatia.

Majambazi sio watu wazuri.

ASANTE
Kabisa nawachukia mpaka basi,, walishawahi kuvamia Dukani kwangu chanika mchana kweupe na bunduki wakakomba Simu zote mauzo yote
 
Hakuna haki ya Jambazi hapa,tutawalaza chini na kuwanyang'anya silaha.Hatuna muda wa kupoteza mahakamani na kesi za majambazi ,hata mahabusu zetu zimejaa.Kama una ndugu jambazi mwambie aache hiyo kazi ,,,,,,,,,
 
Nina anakumbuka anakumbuka inshu ya zombe.watanzania kujifanya mnajua kusahau
 
Hivi huyu Shana nani kampa kibali cha kuua? Maana kaua walioiba gari Costa kahama leo tena itv wanataarifu kuuawa waliokuwa guest house wamepumzika eti wanadhaniwa kuwa majambazi.

Tena anajigamba kumpiga risasi zisizo idadi anayesemekana kukimbilia juu ya dari hajatuambia kama naye alikuwa ana "chaji" kama anayedaiwa yule aliyeuawa akiwa nje.

Serikali ya umwagaji damu hainaga baraka,tujifunze kutoka nchi zinazotuzunguka ambapo umwagaji damu ni kwa viongozi na na wakuu wa polisi pia.

Wewe kama sio jambazi basi maisha yako yana ukaribu wa hali ya kuu na majambazi
 
Huyu Mzee hua mwacheni afanye kazi na anaifahau vizuri kazi yake. Alipambana kule kibiti mwishowe akawa mshindi sasa hivi kibiti ni salama. Hongera zako RPC Mshana
 
Hivi huyu Shana nani kampa kibali cha kuua? Maana kaua walioiba gari Costa kahama leo tena itv wanataarifu kuuawa waliokuwa guest house wamepumzika eti wanadhaniwa kuwa majambazi.

Tena anajigamba kumpiga risasi zisizo idadi anayesemekana kukimbilia juu ya dari hajatuambia kama naye alikuwa ana "chaji" kama anayedaiwa yule aliyeuawa akiwa nje.

Serikali ya umwagaji damu hainaga baraka,tujifunze kutoka nchi zinazotuzunguka ambapo umwagaji damu ni kwa viongozi na na wakuu wa polisi pia.
kaibe na wewe akukamate
 
Back
Top Bottom