RPC Mtwara: Wananchi kaeni mkijua ya kwamba hizo vurugu mnazozipanga kesho sisi tumejipanga vilivyo

Nchi hii kwa mipango!......Wananchi wanajipanga na Polisi nao wanajipanga.....Watawala nao "wanajipangia"
Na ndio mpango mzima kama kwenye Usafiri. Barabara mbovu, Abilia wengi na Kigari kidogo.

Dawa ni kuwajaza, mashimo yatawapanga tu!.

Na sisi wametujazwa shida zinatupanga ukibahatika kuifikia siti unakaa ikishindikana unaning,inia tu!.
 
Nakaa najiuliza na kujishangaa, labda mimi ni mshamba sana au? maana hao wana Mtwara ni akina nani ambao wao kukuza uchumi ni kufanya vurugu? Pili najiuliza hao wana Mtwara ambao akina mama na watoto wao wako tayari kufa kwa lisilojulikana ni akina nani?

Wana Harakati na Wanasiasa, chonde chonde msiwagonganishe wananchi na utawala wao maana hiyo siyo utawala bora. Jamaani eeh kwani Mtwara ndio mkoa pekee wenye madini hapa nchini mbona mnatukerehesha niyie mnaowachochea wananchi?
Naona nashindwa kuwaelewa tu maana hiyo gesi huko Mtwara imekuwa gesi kweli? Au wanachukua advantage ya wengine kutokuelewa mambo? wanaowachochea wanafaidi nini?

Najiuliza tena iwapo ikitokea cha kutokea, mtoto mpendwa wa mtu akafa kwenye varu la gesi, mwenyewe mtamweleza nini? kuwa tulipigania vizazi vijavyo kwa kuuwa wa kwako? hii inanikumbusha wakati wa mgomo wa madaktari, daktari mmoja kijana (shujaa) alitamka wazi, mimi nimeacha kumtibia mtoto wa kaka yangu nikamuacha afe, kwa kuwa niko kwenye mgomo na nataka haki. Hayo ndiyo mambo

ALAMSIKI
usishangae ndo mambo ya kizazi cha zama hizi,maendeleo ya upashanaji habari ndo umepelekea hali hii.leo generation ya leo wanapoona arabspring au occupy wallstreet wao pia wanacopy na kupaste.saa hizi watu wanadai haki zao tena kwa kuforce wakijiorganise kwa kutumia intanet sites.

Zama hizi ukiwa na account mia kadhaa za social media kama tweeter,facebuk,jf,etc .kamera phones mia kadhaa kwa ajili ya kuchukua matukio ya polisi wakiwashughulikia waandamanaji,pesa kiasi za kuwalipa wanaharakati wanao organise protest,demonstration,unaweza anzisha revolution na ukaweza kufanikiawa.
 
kila kheri hakuna ukombozi ambao unakuja kirahisi kwa watu maskini na tabaka lililosaauliwa.

"IF POOR PEOPLE DO NOT INVEST IN TO POWER WHY SHOULD POWER INVEST IN TO POOR PEOPLE". MALCOM X.
 
Kutulia majumbani kuangalia BUNGE ni fujo????

Wanasema kwa kuwa serikali ya CCM imeamua kutumia ubabe basi na wao wataonesha ya upande wao kwa MASLAHI YA VIZAZI VYAO VIJAVYO...[/QUOTE said:
NATUMAINI KUTUMIA UBABE ndiyo kuangalia bunge kwa maana uliyonanyo. Mie nilijaribu kuona context siyo kisingizio cha kuangalia bunge, context ya message nzima jinsi ilivyo. Najua unaweza kusema unaangalia bunge au wote mnunue mahitaji kwa kuwa tutakuwa tunaangalia bunge, bunge lina mida, hoja za Serikali huanza saa nne na kuisha saa 7, huanza tena saa 11, ya nini usiache wawakilishi unaowapenda wafanye kazi yao, ninaloleta kwako ndugu yangu ni busara ya kutambua mambo, usiwapumbaze wananchi kwa kuwambia unaangalia bunge na kuwatahadharisha wanunue vitu leo. Bunge hukaa na kuisha na maisha ni zaidi ya hapo. Basi huduma zitakuwepo kuanzia saa za asubuhi hadi saa nne, then saa 7 hadi 11, taabu yake nini? waenda kazini (watumishi wa Serikali) maana najua ukiumwa kidogo homa ukaenda Hospitali ukakuta Daktari kaenda kuangalia bunge au muuguzi yuko kwenye luninga, kwa taswira ninayoipata utakuwa wa kwanza kumnungunikia kwenye JF, unajua wanatazama luninga. Hivyo madhara yatakuwa si makubwa. KAANGALIE BUNGE, na weka bodaboda yako chini (japo nina shaka mwendesha bodaboda kuwa yuko JF hongera), hesabu jioni. Kibaya ndugu yangu ni kuchochea ???? hidden agenda - VURUGU
 
usishangae ndo mambo ya kizazi cha zama hizi,maendeleo ya upashanaji habari ndo umepelekea hali hii.leo generation ya leo wanapoona arabspring au occupy wallstreet wao pia wanacopy na kupaste.saa hizi watu wanadai haki zao tena kwa kuforce wakijiorganise kwa kutumia intanet sites.

Zama hizi ukiwa na account mia kadhaa za social media kama tweeter,facebuk,jf,etc .kamera phones mia kadhaa kwa ajili ya kuchukua matukio ya polisi wakiwashughulikia waandamanaji,pesa kiasi za kuwalipa wanaharakati wanao organise protest,demonstration,unaweza anzisha revolution na ukaweza kufanikiawa.

Hapo ndugu yangu umenena, na hasa ile sehemu ya mwisho ya "ukiwa na pesa ya kuwalipa wana-harakati, ...."
 
Nakaa najiuliza na kujishangaa, labda mimi ni mshamba sana au? maana hao wana Mtwara ni akina nani ambao wao kukuza uchumi ni kufanya vurugu? Pili najiuliza hao wana Mtwara ambao akina mama na watoto wao wako tayari kufa kwa lisilojulikana ni akina nani?

Wanamtwara ni wananchi wa tz!!
Wacha wafanye yao kwani serikali imewasahau kwa miaka mingi sana!
watu wamechoka!

Nadhani ni vema kusema umechoka, maana ni wewe, na wasiwasi wangu kama wewe mwana Mtwara, ila well si kila mtu ana mawazo yake na misimamo yake? tuwemo
 
Wanamtwara komaeni,BAGAMOYO inawapiku muda si mrefu,si mnajua mwamba ngozi........BAGAMOYO
 
mimi natokea kaskazini, lakini nawaunga mkono kusini kwa asilimia mia, huu mgawanyo mmbovu wa rasilimali ndiyo umesababisha mikoa kama lindi, mtwara, ruvuma, na hata tabora, singida, shinyanga, kigoma ikiwa chakari vibaya. Wacha gesi ibaki mtwara, viwanda viende kule, umeme uzalishwe kule....kwani kuna tatizo gani katika hilo? Hiyo ni nafasi ya pekee kwa mkoa huo kuendelea, na litakuwa jambo la kujivunia mno kwa rais atakayefanikisha hilo!

nakuunga mkono..mia mia
 
Hapo ndugu yangu umenena, na hasa ile sehemu ya mwisho ya "ukiwa na pesa ya kuwalipa wana-harakati, ...."
pesa ni great motivator...ndo inawamotivet hao figurehead wanaorganise hiyo.kitu.hao wanao operate hizo social media account kwa lengo la kusambaza habari na kuincite watu wajoin movement,watu wanaokuwa on the spot the cameraphone kurecord matukio na kuupload kwenye social media.

Lazima uwape pesa,mtu anashindaje nyuma ya keyboard bila kupata kipato,he is got to eat,that is why money come in .
 
Nasikia wabunge wote wa huko wamehamia dsm ukimtoa baruani wa cuf wengine wote wanaogopa kufanya collabo na wananchi wakiogopa kushughulikiwa na chama chao ccm.

kaka tanzania karibu yote itakuwa haitawalika mda si mrefu.uu ubabe hautasaidia chochote
 
Kila la kheri wanamtwara katika kupigania ukombozi wa uchumi wa kusini! Usitegemee serikali ya Dar es salaam itakufikirieni kama nyie mtakuwa mmelala!
 
RPC wangu, wanaosema dawa ya moto ni moto hao ni waongo sana, usiwazikilize, hao ni wauaji wanataka damu iwe mikononi mwako. Nasema dawa ya moto ni maji. Usikubali kumwaga damu. Waache hao 'Wamakonde' waandamane kwa amani hata wakifika Dar au Chalinze shauri lao. Wewe utakuwa umeshinda hapa duniani na peponi. Vitisho na mbwembwe si za mwenye hekima. Maneno laini Tembo huondoka shambani.
 
mangatara
Re: RPC Mtwara: Wananchi kaeni mkijua ya kwamba hizo vurugu mnazozipanga kesho sisi tumejipanga vili
RPC wangu, wanaosema dawa ya moto ni moto hao ni waongo sana, usiwazikilize, hao ni wauaji wanataka damu iwe mikononi mwako. Nasema dawa ya moto ni maji. Usikubali kumwaga damu. Waache hao 'Wamakonde' waandamane kwa amani hata wakifika Dar au Chalinze shauri lao. Wewe utakuwa umeshinda hapa duniani na peponi. Vitisho na mbwembwe si za mwenye hekima. Maneno laini Tembo huondoka shambani.

Kama vurugu zitatokea basi kuna hatari ya watu wengi kupoteza maisha ata askari maana RPC MTWARA hayuko tiari kuona maandamano najua atatumia nguvu nyingi kuyatuliza mahandamano bila kujali nguvu gan.JARIBU KUJIEPUSHA NAYO KAMA ITAWEZEKANA.
 
kama nimemuelewa sawasawa THE BIG SHOW ni kuwa kesho ni Passive resistance ( kwa tafsiri yangu ni "mgomo") hakuna huduma za kijamii usafiri na kadhalika. Wewe hayo maandamano yanatoka wapi ?
 
Last edited by a moderator:
Asanteni wana mtwara kwa kuto kata tamaa. wananchi wa nchi nzima wangekuwa na moyo kama ya wana mtwara hakika nchii hii inge badilika kabisa.
 
kama nimemuelewa sawasawa THE BIG SHOW ni kuwa kesho ni Passive resistance ( kwa tafsiri yangu ni "mgomo") hakuna huduma za kijamii usafiri na kadhalika. Wewe hayo maandamano yanatoka wapi ?

Siyo kosa lake kaka, ENWYO hajaelewa somo. Hakuna anayeandamana, lakini watu wako kwenye mgomo, mji wote ziiii!
 
Last edited by a moderator:
Hii passive resistance kumbe ishaanza kuwasumbua na itawasumbua sana mafisadi wa CCM,watu wameamua kukaa zao nyumbani na kuacha kufanya shughuli zao kwa khiyari yao,nashangaa serikali inasema kwa tambo kuwa imejipanga,imejipanga nini sasa??
imejipanga kuwalazimisha watu kufungua maduka yao??
 
Back
Top Bottom