DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,129
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro SACP Simon Maigwa amewasihi Wananchi kutunza amani kwa maslahi ya nchi na vizazi vijavyo ili kuleta maendeleo katika Taifa.
Kamanda Maigwa ameyasema hayo alipokuwa akitoa elimu ya umuhimu wa amani kwa Watumishi wa Serikali na Wananchi katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Same leo Oktoba 13,2025.
SACP Maigwa amesisitiza kwa kusema "Amani ya nchi yetu ni Tunu ya kujivunia kwani zipo nchi nyingi zinatamani kuwa na amani kama sisi lakini wameshindwa kuipata baada ya kutoweka kwa vita, baadhi ya watu wasio na nia njema na nchi yetu wanatumia nguvu kubwa kuhakikisha amani hii inatoweka na kuleta machafuko katika Taifa"
Kamanda Maigwa ameongeza kuwa Jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro lipo imara na litahakikisha tunailinda amani kwa nguvu zote na Wananchi wasikubali kurubuniwa kuingia katika mtego wa watu wachache wenye malengo mabaya na nchi hasa kipindi hiki cha uchaguzi mkuu 2025.
Kwa upande Mwingine elimu hiyo imeendelea kutolewa kwa Wananchi katika Wilaya ya Hai ambapo Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Richard Mollel ametoa elimu hiyo kwa Makundi ya Wananchi wakiwemo Bodaboda, Madereva Bajaji, Askari Mgambo na Watumishi wa Serikali.