RPC amsweka rumande OCD kwa rushwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

RPC amsweka rumande OCD kwa rushwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by OSOKONI, Aug 30, 2012.

 1. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #1
  Aug 30, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,797
  Likes Received: 3,883
  Trophy Points: 280
  KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Salum Msangi amemsweka rumande Mkuu wa Polisi Wilaya ya Bariadi (OCD) na Mkuu wa Kituo cha Polisi Bariadi (OCS), kwa tuhuma za rushwa.Wakati hayo yakitokea, jeshi hilo limezidi kuandamwa na kashfa baada ya baadhi ya askari wake kudaiwa kumpiga Kadogoo Kalanga (16), hadi kulazwa chumba cha wagonjwa mahututi (ICU).

  Katika tukio la Simiyu, Kamanda Msangi anawashikilia maofisa hao kutokana na madai ya kuomba rushwa ya Sh3.5 milioni kutoka kwa mtuhumiwa kwa kisingizio RPC huyo ndiye aliyewatuma.
  Taarifa zilizopatikana jana na kuthibitishwa na Kamanda Msangi, zimeeleza kuwa tukio hilo lilitokea Jumapili iliyopita saa 6:00 mchana, ambapo maofisa hao walimkamata mtu anayetuhumiwa kufanya ujambazi kwa kutumia silaha na kumtaka awape fedha hiyo ili wamwachie.

  Alisema maofisa hao wamechukuliwa hatua ili iwe fundisho kwa wengine ambao wanafanya kazi kwa mazoea na kulipaka matope jeshi hilo.

  Akisimulia tukio hilo, Kamanda Msangi alisema: "Maofisa hao wakiwa kazini waliarifiwa kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo… (jina tunalo) ambaye ni mfanyakazi wa Mgodi wa Barrick North Mara, akihusishwa na jambazi sugu aliyekuwa akitafutwa kwa kuhusika na tukio la uporaji dhahabu katika Mgodi wa Geita.

  "Mtu huyo alipokamatwa, ofisi yangu iliarifiwa na kuanza kufanya taratibu za kuwasiliana na watu wa Geita na maeneo mengine ili kubaini kama mhusika ndiye mtuhumiwa sahihi, ila kabla ya kukamilika kwa uchunguzi aliachiwa."

  Alisema kitendo hicho kilimkera na kuamuru mtuhumiwa huyo atafutwe tena.
  Alisema baada ya kuwaagiza maofisa hao wamtafute mtuhumiwa, walipompata walimtaka awape kiasi hicho cha fedha na kumweleza kuwa wametumwa na RPC.

  Alisema ndugu wa mtuhumiwa huyo baada ya kuona wameombwa kiasi kikubwa cha fedha, walikwenda katika ofisi za RPC na kumweleza nia ya maofisa hao hali iliyomfanya aanze kuweka mitego ya kuwanasa.

  Alisema atahakikisha anasafisha idara zote za polisi mkoani humo hususan wenye tabia ya kuwabambikizia watu kesi.
  "Huo ndiyo msimamo wangu. Haiwezekani watu wafanye wanavyojisikia halafu tukae kimya wakati wanalipaka matope jeshi la polisi. Kabla ya kuwa mkoa, wilaya hii ilikuwa mbali na makao makuu ya Mkoa wa Shinyanga, hivyo watu walikuwa wakiishi kama kuku wa kienyeji," alisema Msangi.
  Alisema yapo malalamiko mengi ya wananchi dhidi ya askari wa mkoa huo na kuahidi kuyashughulikia.

  Unyama Manyara

  Polisi mkoani Manyara, wanadaiwa kumpiga hadi kupoteza fahamu Kadogoo Kalanga, mkazi wa Orkesmet, wilayani Simanjiro juzi saa 5:30 asubuhi kwa madai kuwa ameiba mbuzi wa jirani yake. Kutokana na kipigo hicho, kijana huyo amelazwa katika wodi ya wagonjwa mahututi (ICU), katika Hospitali ya Selian, Arusha.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Akili Mpwapwa alikiri kupata taarifa ya tukio hilo na kueleza kuwa tayari ameshatoa maelekezo kwa Mkuu wa Polisi Wilaya (OCD), Simanjiro kufanya uchunguzi wa kina na kuwasilisha kwa ripoti.

  "Nimeshatoa maelekezo kwa OCD kwamba uchunguzi wa kina ufanyike na nipewe ripoti kamili kwa kuwa jana ndiyo nilipigiwa simu na kuelezwa juu ya tukio hilo," alisema na kuongeza kuwa endapo kuna askari atakayebainika kuhusika na tukio hilo, hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

  Akizungumza na waandishi wa habari hospitalini hapo, mama wa kijana huyo, Paulina Kalanga alisema askari watatu walimfuata mtoto wake katika eneo la Mnadani na kumtuhumu kuiba mbuzi kisha kuanza kumpiga.
  Alisema walianza kumpiga sehemu mbalimbali za mwili wake na kusababisha kijana huyo kuanza kutokwa mkojo mfululizo kabla ya kupoteza fahamu.

  Huku akitokwa na machozi, mama huyo alisema askari hao wakati wakiendelea kumpiga, walimshika katika sehemu zake za siri na kuzivuta huku wakizigongagonga kwa kitako cha bunduki."Walimkamata na kumpiga kwa marungu na mateke, hawakuridhika wakazishika sehemu zake za siri na kuanza kuzigongagonga na kitako cha bunduki. Nilimwona mwanangu akitokwa na mkojo na akapoteza fahamu."

  Daktari: Hali mbaya

  Mkuu wa Kituo cha Afya cha Orkesmet, Dk Loishorwa Ole Yamak alikiri kumpokea kijana huyo kituoni hapo juzi na kueleza kuwa alifikishwa akiwa katika hali mbaya huku akitokwa na damu puani."Ni kweli huyo kijana aliletwa hapa akiwa anatokwa damu puani kuna askari mmoja ndiye alimleta hapa na kutoa maelezo kwamba alianguka na pikipiki," alieleza daktari huyo.Alisema baada ya kuona hali yake hairidhishi, aliwashauri ndugu wa kijana huyo wampeleke Arusha ili akapatiwe huduma ya CT-Scan na X-ray.

  Uchunguzi Morogoro

  Katika hatua nyingine, matokeo ya uchunguzi uliofanywa na madaktari mkoani Morogoro kubaini jeraha lililosababisha kifo cha mfuasi wa Chadema, Ally Zona wakati polisi wakitawanya maandamano ya chama hicho yametolewa na mwili huo umezikwa jana.

  Akieleza matokeo hayo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shillogile alidai kuwa jeraha lililosababisha kifo cha marehemu lililokuwa kichwani, lilitokana na kugongwa na kitu kizito kilichorushwa na siyo risasi kama ambavyo watu walikuwa wakidhani.

  Alisema uchunguzi huo ulifanywa na madaktari wawili wa mkoani hapa pamoja na Dk Ahmed Makata kutoka Dar es Salaam na kushuhudiwa na mwanasheria wa Chadema, Aman Mwaipaya pamoja na baadhi ya askari polisi.

  Alisema kuwa baada ya matokeo hayo ya daktari, polisi sasa wanaendelea na uchunguzi wa kubaini kitu hicho kilichorushwa na kusababisha kifo cha mfuasi huyo kabla ya kuchukua hatua za kisheria kwa askari au mtu mwingine atakayebainika kurusha kitu hicho ikiwa ni pamoja na kumkamata mtu au kiongozi wa chama hicho aliyechochea au kuandaa maandamano hayo yaliyozua vurugu.

  Serikali imeunda tume ya kuchunguza ikiwashirikisha polisi na watu wengine.
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Aug 30, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,339
  Likes Received: 19,519
  Trophy Points: 280
  wamefoji vyeti hawa
   
 3. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #3
  Aug 30, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,641
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Tanzania inaudhi sana, na tumekuwa mabingwa wa kulalamika sana kwenye mitandao as if Mungu hakutupa na sisi utashi! Hivi hicho kitu kizito kilirushwa na nini hasa mpaka kitoboe fuvu? Hawa mapolisi wana majibu mengine zaidi ya haya, na kuna haja ya kuwa na jeshi lingine la polisi kwa ajili ya wananchi badala ya hili kwa ajili ya CCM.
   
 4. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #4
  Aug 30, 2012
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,698
  Likes Received: 8,238
  Trophy Points: 280
  Kumbe na mwanasheria wa chadema alikuwepo...basi aseme yeye. Kwa ufahamu wangu mdogo risasi halisi ikikupiga kwa nyuma ya kichwa basi reception haitambuliki...sidhani kama ndivyo ilivyokuwa kwa bw. Ally
   
 5. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #5
  Aug 30, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,225
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  bora wewe umeliona hilo, siyo watu wengine hata kwenye technical info wanapinga. Chadema wabebe hizi lawama.
   
 6. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #6
  Aug 30, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,332
  Likes Received: 2,636
  Trophy Points: 280
  naona wameanza kukamatana eenh!
   
 7. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #7
  Aug 30, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  ila wako kazini....ha ha ha ha
   
 8. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #8
  Aug 30, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,800
  Trophy Points: 280
  kulikuwa na ulazima gani wa kumtoa dr. Dar kwenda kufanya posmortem morogoro? Ina maana moro hakuna qulified Dr.

  Huyo ni dr. IGHONDU phisical adress - mabwepande.
   
 9. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #9
  Aug 30, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Tunakoelekea kazi itakuwa ngumu zaidi ya tuiyonayo!

  MUNGU tutangulie!
  Askari waliokabidhiwa dhamana ya Mtanzania leo amegeuka kuwa mwuaji???

  Ama kweli kazi ipo!
  Ila hakika tutafika tu!

  WAO WANA PESA SISI TUNA MUNGU:
   
 10. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #10
  Aug 30, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,800
  Trophy Points: 280
  Ni bora tuzipige na wamalawi, ili wakaone silaha hutumika wapi, kwa sasa hawajui.
  Tuwapeleke wakilegeza makalio yanarudi majina na nyimbo.
   
 11. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #11
  Aug 30, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,323
  Likes Received: 22,137
  Trophy Points: 280
  Polisi wetu ndio wanaowafundisha majambazi mbinu za kipolisi.
   
 12. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #12
  Aug 30, 2012
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,698
  Likes Received: 8,238
  Trophy Points: 280
  jogi, JAMBO USILOLIJUA NI SAWA NA USIKU WA GIZA.
  Dr. Makata ni daktari wa jeshi wa masuala ya postmortem..ongea lingine!

  NB: I am not supporting any violent acts or excessive use of force against citizens byt our police force...ila tusiseme mambo kiushabiki! tuongee ukweli nao utatuuweka huru!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. M

  Malipo kwamungu JF-Expert Member

  #13
  Aug 30, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 574
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Naomba mtoe ufafanuzi aliye uwawa na POLISI alikuwa muuza magazeti au mwanachama muandamanaji? taarifa ya polisi inasema "Mwanachama wa CDM aliyefariki wakati polisi wanazuia maandamano.....??" Tafadhali usahihi ni upi
   
 14. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #14
  Aug 30, 2012
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  alafu wachunguzwe na elimu zao kama waligushi basi wawajibishwe
   
 15. NusuMutu

  NusuMutu JF-Expert Member

  #15
  Aug 30, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 423
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  RPC anasema atasafisha uozo(rushwa) idara zote?¿? KWEEENDA ZAKE! Rushwa imewashinda PCCB sembuse polis ambao hadi watoto wadogo wanajua trafik dau lake ni ngapi,tigo dau lake,wale wa mizani kibaha(hawa naskia ni buku tu magari makubwa),nk
   
 16. fangfangjt

  fangfangjt JF-Expert Member

  #16
  Aug 30, 2012
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 571
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 33
  http://www.mwananchi.co.tz/news/4-habari-za-kitaifa/25851-rpc-amsweka-rumande-ocd-kwa-rushwa.html

  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Wednesday, 29 August 2012 20:55[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]

  Waandishi Wetu
  KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Salum Msangi amemsweka rumande Mkuu wa Polisi Wilaya ya Bariadi (OCD) na Mkuu wa Kituo cha Polisi Bariadi (OCS), kwa tuhuma za rushwa.Wakati hayo yakitokea, jeshi hilo limezidi kuandamwa na kashfa baada ya baadhi ya askari wake kudaiwa kumpiga Kadogoo Kalanga (16), hadi kulazwa chumba cha wagonjwa mahututi (ICU).

  Katika tukio la Simiyu, Kamanda Msangi anawashikilia maofisa hao kutokana na madai ya kuomba rushwa ya Sh3.5 milioni kutoka kwa mtuhumiwa kwa kisingizio RPC huyo ndiye aliyewatuma.

  Taarifa zilizopatikana jana na kuthibitishwa na Kamanda Msangi, zimeeleza kuwa tukio hilo lilitokea Jumapili iliyopita saa 6:00 mchana, ambapo maofisa hao walimkamata mtu anayetuhumiwa kufanya ujambazi kwa kutumia silaha na kumtaka awape fedha hiyo ili wamwachie.

  Alisema maofisa hao wamechukuliwa hatua ili iwe fundisho kwa wengine ambao wanafanya kazi kwa mazoea na kulipaka matope jeshi hilo.

  Akisimulia tukio hilo, Kamanda Msangi alisema: “Maofisa hao wakiwa kazini waliarifiwa kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo… (jina tunalo) ambaye ni mfanyakazi wa Mgodi wa Barrick North Mara, akihusishwa na jambazi sugu aliyekuwa akitafutwa kwa kuhusika na tukio la uporaji dhahabu katika Mgodi wa Geita.

  “Mtu huyo alipokamatwa, ofisi yangu iliarifiwa na kuanza kufanya taratibu za kuwasiliana na watu wa Geita na maeneo mengine ili kubaini kama mhusika ndiye mtuhumiwa sahihi, ila kabla ya kukamilika kwa uchunguzi aliachiwa.”
  Alisema kitendo hicho kilimkera na kuamuru mtuhumiwa huyo atafutwe tena.
  Alisema baada ya kuwaagiza maofisa hao wamtafute mtuhumiwa, walipompata walimtaka awape kiasi hicho cha fedha na kumweleza kuwa wametumwa na RPC.

  Alisema ndugu wa mtuhumiwa huyo baada ya kuona wameombwa kiasi kikubwa cha fedha, walikwenda katika ofisi za RPC na kumweleza nia ya maofisa hao hali iliyomfanya aanze kuweka mitego ya kuwanasa.

  Alisema atahakikisha anasafisha idara zote za polisi mkoani humo hususan wenye tabia ya kuwabambikizia watu kesi.
  “Huo ndiyo msimamo wangu. Haiwezekani watu wafanye wanavyojisikia halafu tukae kimya wakati wanalipaka matope jeshi la polisi. Kabla ya kuwa mkoa, wilaya hii ilikuwa mbali na makao makuu ya Mkoa wa Shinyanga, hivyo watu walikuwa wakiishi kama kuku wa kienyeji,” alisema Msangi.
  Alisema yapo malalamiko mengi ya wananchi dhidi ya askari wa mkoa huo na kuahidi kuyashughulikia.

  Unyama Manyara
  Polisi mkoani Manyara, wanadaiwa kumpiga hadi kupoteza fahamu Kadogoo Kalanga, mkazi wa Orkesmet, wilayani Simanjiro juzi saa 5:30 asubuhi kwa madai kuwa ameiba mbuzi wa jirani yake. Kutokana na kipigo hicho, kijana huyo amelazwa katika wodi ya wagonjwa mahututi (ICU), katika Hospitali ya Selian, Arusha.
  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Akili Mpwapwa alikiri kupata taarifa ya tukio hilo na kueleza kuwa tayari ameshatoa maelekezo kwa Mkuu wa Polisi Wilaya (OCD), Simanjiro kufanya uchunguzi wa kina na kuwasilisha kwa ripoti.

  “Nimeshatoa maelekezo kwa OCD kwamba uchunguzi wa kina ufanyike na nipewe ripoti kamili kwa kuwa jana ndiyo nilipigiwa simu na kuelezwa juu ya tukio hilo,” alisema na kuongeza kuwa endapo kuna askari atakayebainika kuhusika na tukio hilo, hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

  Akizungumza na waandishi wa habari hospitalini hapo, mama wa kijana huyo, Paulina Kalanga alisema askari watatu walimfuata mtoto wake katika eneo la Mnadani na kumtuhumu kuiba mbuzi kisha kuanza kumpiga.
  Alisema walianza kumpiga sehemu mbalimbali za mwili wake na kusababisha kijana huyo kuanza kutokwa mkojo mfululizo kabla ya kupoteza fahamu.

  Huku akitokwa na machozi, mama huyo alisema askari hao wakati wakiendelea kumpiga, walimshika katika sehemu zake za siri na kuzivuta huku wakizigongagonga kwa kitako cha bunduki.“Walimkamata na kumpiga kwa marungu na mateke, hawakuridhika wakazishika sehemu zake za siri na kuanza kuzigongagonga na kitako cha bunduki. Nilimwona mwanangu akitokwa na mkojo na akapoteza fahamu.”

  Daktari: Hali mbaya

  Mkuu wa Kituo cha Afya cha Orkesmet, Dk Loishorwa Ole Yamak alikiri kumpokea kijana huyo kituoni hapo juzi na kueleza kuwa alifikishwa akiwa katika hali mbaya huku akitokwa na damu puani.“Ni kweli huyo kijana aliletwa hapa akiwa anatokwa damu puani kuna askari mmoja ndiye alimleta hapa na kutoa maelezo kwamba alianguka na pikipiki,” alieleza daktari huyo.Alisema baada ya kuona hali yake hairidhishi, aliwashauri ndugu wa kijana huyo wampeleke Arusha ili akapatiwe huduma ya CT-Scan na X-ray.

  Uchunguzi Morogoro
  Katika hatua nyingine, matokeo ya uchunguzi uliofanywa na madaktari mkoani Morogoro kubaini jeraha lililosababisha kifo cha mfuasi wa Chadema, Ally Zona wakati polisi wakitawanya maandamano ya chama hicho yametolewa na mwili huo umezikwa jana.

  Akieleza matokeo hayo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shillogile alidai kuwa jeraha lililosababisha kifo cha marehemu lililokuwa kichwani, lilitokana na kugongwa na kitu kizito kilichorushwa na siyo risasi kama ambavyo watu walikuwa wakidhani.

  Alisema uchunguzi huo ulifanywa na madaktari wawili wa mkoani hapa pamoja na Dk Ahmed Makata kutoka Dar es Salaam na kushuhudiwa na mwanasheria wa Chadema, Aman Mwaipaya pamoja na baadhi ya askari polisi.
  Alisema kuwa baada ya matokeo hayo ya daktari, polisi sasa wanaendelea na uchunguzi wa kubaini kitu hicho kilichorushwa na kusababisha kifo cha mfuasi huyo kabla ya kuchukua hatua za kisheria kwa askari au mtu mwingine atakayebainika kurusha kitu hicho ikiwa ni pamoja na kumkamata mtu au kiongozi wa chama hicho aliyechochea au kuandaa maandamano hayo yaliyozua vurugu.

  Serikali imeunda tume ya kuchunguza ikiwashirikisha polisi na watu wengine.
  Imeandikwa na Hamida Shariff, Morogoro; Moses Mashalla, Arusha na Frederick Katulanda, Bariadi.[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 17. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #17
  Aug 30, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 737
  Trophy Points: 280
  Danganya toto hiyo......
   
 18. u

  usungilo JF-Expert Member

  #18
  Aug 30, 2012
  Joined: Aug 9, 2012
  Messages: 501
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 60
  Huyu anataka kufukuzwa kazi, ameenda kinyume kabisa na maadili ya ccm. Alitakiwa aseme ameunda tume ya kufanya uchunguzi na upembuzi yakinifu.
   
 19. TOWNSEND

  TOWNSEND JF-Expert Member

  #19
  Aug 30, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,597
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Sitaona ajabu huyo rpc msangi akirudishwa makao makuu dar akawekwa benchi
   
 20. m

  mwinukai JF-Expert Member

  #20
  Aug 30, 2012
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 1,448
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Waende kwa Gwajima huenda wakampata maana katika mauaji kama haya watu huwa wanaenda kwa Gwajima kuungama
   
Loading...