Royal Madrid

Royal Madrid

mollel_afrika

Member
Joined
Sep 5, 2026
Posts
8
Reaction score
12
Leo nataka nitikise meza ya vinywaji vya gharama kubwa maana watoto wanazungumza kuwa whiskey ndio kinywaji cha gharama kubwa zaidi, sipo mbali nao ila acha niwaambie football ndio kilevi hatari na Cha gharama kubwa sana kwani kinahitaji moyo na muda kama malipo ya kile unacho taka kukishuhudia katu hatuta zungumza kuhusu fedha ambazo kule hazitumiki bali zinamwagwa ili kutimiza ladha ya kilevi,
kuna viwanda vingi sana ambavyo vinatengeneza kilevi hiki lakini royal real Madrid, ni miongoni mwa wale wanao utakatisha mpira wa miguu kwani kama nikiwaita mafia hasa wale wa Cosa Nostra sidhani kama nitakuwa nimekosea,

Ninapo sema mafia simaanishi kisiwa cha mafia kilichopo chini ya mamlaka ya jamhuri ya Tanzania bali ni wale wazee wa 'Lost generation' lakini vijana na watoto katika generation X,Y& Z ndio ni wale Gen Z wa Karne ya 19, ambao walifanya maafa makubwa na kugawana madaraka ya lile taifa la Mazzini na hata Benedict Mussolini kwa maana ya waitaliono, walijitengenezea ufalme katika masuala ya kiuhalifu haswa katika miji ya Naples, Palermo na hata Regio Calabria,

Mwaka 1947 ndani ya LA CAPITAL wanachama wakafikia azimio la kufikisha tamati ya miaka 46 bila ya machinjio kwa maana ya uwanja ulio bora na hadhi ya kufalme kwani toka mwaka 1901 walipo zaliwa kutoka kwenye vichwa vya wenye nia hawakuwahi kupata zawadi kubwa kama hiyo,

Nuevo Chamartín ukawa ubatizo wa machinjio hayo na ukaanza kukusanya kodi kutoka geti ambapo Kila mwenye chapa ya royal Madrid kwenye moyo wake basi angeweza kuishuhudia miguu ya vijana hawa wa mfalme,

Ulikuwa umejengwa chini ya uongozi wa Santiago Bernabéu, ambaye alikuwa rais wa Real Madrid kuanzia 1943 hadi 1978. Uwanja huo mpya ulifunguliwa tarehe 14 Desemba 1947 ukiitwa Nuevo Chamartín.

KATU heshima haito acha kwenda kwa 'El Presidente Eterno Don Santiago Bernabau' kwa maana ya raisi wa heshima na wa milele Santiago Bernabau,

Huyu alikuwa nahodha, kocha,na baadaye rais kwanzia mwaka 1943 mpaka mwaka 1978,
Don Santiago alimleta mafia aliyeleta utata mkubwa ndani ya Hispania kwa maana ya Di Stéfano alifika Madrid mwaka 1953 baada ya moja ya sakata tata zaidi katika historia ya usajili wa wachezaji. Barcelona ilikuwa tayari imefanya makubaliano na River Plate, wakati Real Madrid ikafikia makubaliano na Millonarios, klabu ambayo Di Stéfano alikuwa akiichezea wakati huo. FIFA na mamlaka za soka la Hispania ziliingilia kati, na hatimaye Barcelona ikaondoka kwenye mpango huo, huku Di Stéfano akiishia Madrid.
Na hapo ndipo “kazi” ya mafia ilipoanza kuonekana.

Itaendelea...............,

#football #madrid #madridistas #Galacticos #tanzania #MichezoTODAY
 

Attachments

  • 60243.jpeg
    60243.jpeg
    71.5 KB · Views: 2
  • 60245.jpeg
    60245.jpeg
    40.2 KB · Views: 1
  • 60244.jpeg
    60244.jpeg
    70.7 KB · Views: 1
Unaambiwa kila baada ya mechi morhno anaingia kwenye gari anaicheka halaa madrid
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom