Mzalendo Mkuu
JF-Expert Member
- Nov 2, 2010
- 735
- 191
Huyo ndio mkwere tatizo la gari ni engine yeye anaenda kununua tairi mpyaHivi jamani kweli Kikwete hafahamiani na Rostam Aziz?Maana juzi kauongopea uma wa watanzania kuwa hawajui dowans na wala wao dowans hawamjui yeye.NI AJABU NA KWELI LAKINI IMETOKEA HAPA TANZANIA, RAIS WA NCHI KUWAONGOPEA RAIA WAKE WAPATAO MILION 40 MCHANA KWEUPE
Au hajawahi kumjua mama salmaJinsi Kikwete alivyosema hawajui Dowans, iko siku mtasikia anasema hajui kama kuna mgao wa umeme
Ni kweli JK hawajui Dowans,ila anawajua Ricmonds,hao ndiyo walioingia mkataba na siyo Dowans hii ndiyo habari ya kubadili majia ya kampuni leo Mobitel,kesho Buzz keshokutwa TIGO au CELTEL - ZAIN - AIRTEL kumbe kampuni ni ileile,watueleze ukweli hawa wasituchanganye kwani kuna mkataba wa DOWANS au ni wa RICMONDS au kubadili majina kuficha madhambi kwa kutumia majina tofauti.Hivi TANESCO na BUNGE nani zaidi ROSTAM yuko bungeni kuchunguza udhaifu wa Bunge na serikali yake na kutafuta pa kupatia fedha huyu yupo kimaslahi zaidi.Hivi hizo Almasi anazochota huko mwadui hazimtoshi? umewahi kusikia kiwanda cha kukata almasi kilichokuwa Iringa? naamini hakipo je hizo almasi hazipo?huyu jamaa hana chembe ya uzalendo wala siamini kama ni mtazania tamaa ya namna hii kutaka wewe ndiyo uwe na fedha kuliko serikali inatisha.dawa yake ipo jikoni siku wa TZtutakapoamka lazima aziteme zote
Mwizi siku zake ni Arobaini. Siku zote imekuwa siri lakini hatimaye amekuja kujulikana mmiliku wa Dowans. Jambo moja la kushangaza ni kuwa kwenye gazeti la Mtanzania Rostam anasema Dowans ndiyo kampuni iliyoleta mitambo kwa haraka na kuzalisha umeme wa bei nafuu zaidi! Hapa ninashanga kwa kuwa Mitambo ililetwa na Richmond naye Rostam anasema mitambo ililetwa na Dowans. Kwake Rostam Richnomond na Dowans ni kitu kimoja? Nchi inakwenda wapi hii?
Inawezekana alichanganywa akili mpaka akajisahau. safi sana