Rostam azidi kuthibitisha alivyoweka nchi mfukoni mwake

mpayukaji

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
940
349
[h=3]Bongo nchi ya wauza bwimbwi[/h]

thumbnail.aspx

Taarifa kuwa mtuhumiwa wa kusafirisha madawa ya kulevya ambaye ni mdogo wa mbunge wa zamani wa Igunga Rostam Aziz aitwaye Abdulrasul kutokutwa na hatia ni pigo kwa taifa. Ukisoma jinsi kesi ilivyoendeshwa haraka na kinamna unashangaa hawa majaji wetu au tuseme waendesha mashtaka huvuta bangi gani. Uzoefu unaonyesha kuwa kesi za madawa ya kulevya au ufisadi zinazohusisha vigogo au makuwadi wao, huisha kinamna huku wateule wakiachiliwa huru na wanyonge kubeba mzigo wao.Abdulrasul alikuwa akikabiliwa shitaka la kutaka kusafirisha madawa ya kulevya kupitia bandari ya Tanga. Kama ilivyokuwa kwa Kagoda, Rostam amezeidi kupeta huku waswahili vidagaa waliosaidiana naye wakiendendelea kukabiliwa na kesi yake! Kwa habari zaidi Bonyeza hapa.

Si ndie mnamwita king-maker! Tanzania mwenye hatia hufutiwa na asie kuwa nayo hubambikwa! Namkumnbuka mtoto wa Mengi
 
Hii ni hatari kuliko hatari yenyewe! Duu! Kazi qeli qeli qani tutafika ila tukiwa katika hali mbaya sana yaani tukitambaa kama sio ku"crow"
 
[h=3]Bongo nchi ya wauza bwimbwi[/h]

thumbnail.aspx

Taarifa kuwa mtuhumiwa wa kusafirisha madawa ya kulevya ambaye ni mdogo wa mbunge wa zamani wa Igunga Rostam Aziz aitwaye Abdulrasul kutokutwa na hatia ni pigo kwa taifa. Ukisoma jinsi kesi ilivyoendeshwa haraka na kinamna unashangaa hawa majaji wetu au tuseme waendesha mashtaka huvuta bangi gani. Uzoefu unaonyesha kuwa kesi za madawa ya kulevya au ufisadi zinazohusisha vigogo au makuwadi wao, huisha kinamna huku wateule wakiachiliwa huru na wanyonge kubeba mzigo wao.Abdulrasul alikuwa akikabiliwa shitaka la kutaka kusafirisha madawa ya kulevya kupitia bandari ya Tanga. Kama ilivyokuwa kwa Kagoda, Rostam amezeidi kupeta huku waswahili vidagaa waliosaidiana naye wakiendendelea kukabiliwa na kesi yake! Kwa habari zaidi Bonyeza hapa.

Hiii ndo Tanzania!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Pinda alionya "....mafisadi wakishughulikiwa nchi itayumba.....". Jaribu kupitisha hiyo sentensi ktk ubongo utaona mambo

Pinda hajakosea kabisa..hivi mnajua Rostam anaidai hii serikali kiasi gani??? Huyu ndio mfalme wa hii nchi siku akisema watanzania wote nataka leo mtembee na chupi tu barabarani ujue wewe mimi ndugu zetu wote tunachojoa nguo tunatembea na vyupi mpaka akisema inatosha ndio tunaacha...Halafu tunasema hii nchi ina uhuru wakati tunatawaliwa hivi hivi tunajiona!!
 
Mi nilifikiri kapewa ile tuzo ya richmond? Nilitaka kujua mgawo wa richmond kati ya kikwete rostam na lowasa utafanyika lini na wapi.
Nna hasira sn na kikwete lowasa na rostam
 
Mzigo/shehena hiyo ndio kubwa kuwahi kukamatwa Tanzania na Afrika kwa wakati mmoja kwa Takwimu za sasa ni Kilo 179 zenye dhamani ya bilioni 3.

Mtaji wake ni wa mtu mzito hiyo ni shehena ya biashara moja tu mbali na kukamatwa hakuna kuyumba ni sawa na kuiba pipi moja dukani
 
Pinda hajakosea kabisa..hivi mnajua Rostam anaidai hii serikali kiasi gani??? Huyu ndio mfalme wa hii nchi siku akisema watanzania wote nataka leo mtembee na chupi tu barabarani ujue wewe mimi ndugu zetu wote tunachojoa nguo tunatembea na vyupi mpaka akisema inatosha ndio tunaacha...Halafu tunasema hii nchi ina uhuru wakati tunatawaliwa hivi hivi tunajiona!!

acha wendawazimu wewe, kama kutmembea na chupi utatembea wewe na familia yako....
 
Rostam amehangaika sana kumtoa mdogo wake hadi kafanikiwa alikamatwa na ushahidi akiwa na shehena lakini ati hana kesi ya kujibu lakini kwa vile ametoka atapambana kuwatoa vibarua wake walioko mahabusu.
 
Back
Top Bottom