Rostam alikurupuka au alishinikizwa? Watuhumiwa wa ufisadi hawana mtandao rasmi.....

Crucifix

JF-Expert Member
Feb 20, 2011
1,651
588
Baada ya kushuhudia ugumu wa magamba ya EL na AC, nimefikia kujiuliza endapo RA alikurupuka kwa hasira kujiuzulu au alishinikizwa? Endapo RA naye angegoma kujiuzulu, sidhani kungekuwa na tofauti yoyote kama ilivyo sasa. Au labda alijazwa woga kuhusu uhai wa biashara zake. Inaonekana pia hakuna umoja fulani miongoni mwa watuhumiwa wa ufisadi CCM bali kila mmoja anapigana kivyake ili kujiokoa. Wakati Chenge akishindwa kupata uspika, Lowassa aliukwaa uenyekiti wa kamati ya mambo ya nje na kumpa fursa za kujijenga. Rostam alisemwa kufadhili ili Sitta asirejee uspika na cheo kikaangukia kwa Makinda ambaye hasemekani kuwa katika mtandao wa Lowassa mwenye malengo ya urais '15. Hivyo naona japo hawa wanatuhumiwa kwa pamoja lakini wao hawana huo umoja wala msimamo wa pamoja.
 
Rostam alisema ukweli kwamba sababu ya kuacha ni biashara. Ilifikia wakati kila mtu akitafuta habari za biashara za Rostam anapata mambo ya ufisadi. Wafanya biashara wengi hasa wa kitaifa hawapendi kufanya biashara na watu wenye matatizo na wananchi kama tuhuma za umma kama ufisadi. Haya mambo yalishaanza kufanya biashara zake za kifaifa ziyumbe!!. Hii ni sababu muhimu sana kama unataka kufanya biashara zaidi ya siasa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom