(ROONEY na CHACHARITO) ( ZITTO na DAVID SILINDE) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

(ROONEY na CHACHARITO) ( ZITTO na DAVID SILINDE)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Taifa_Kwanza, Mar 23, 2011.

 1. T

  Taifa_Kwanza JF-Expert Member

  #1
  Mar 23, 2011
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 443
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  kwa wale wapenzi wasoka kama waliangalia mechi ya Manchester United na ---- last week watakubaliana na mimi kwamba Rooney alionyesha kiwango cha juu sana cha uchezaji wa kiteam. Japo hii ni kawaida kwa rooney lakini mechi hiyo specifically aliifurahisha zaidi.

  Katika mechi hiyo, zaidi ya mara tatu, Rooney alimpasia mpira Chacharito katika mazingira ambayo yeye mwenyewe alikiwa na nafasi nzuri zaidi ya kufunga goal.

  Katika maisha ya kawaida ni nadra sana kukuta vijana wakishirikiana kwa dhati kabisa (sio mdomoni) katika kuhakikisha kwamba ama kila mmoja anafanikiwa ama mwenzie anafanikiwa zaidi, Katika siasa za Tanzania naomba kuchukua nafasi huu kumshauri ZITTO KABWE kwamba asiogope kufunikwa na wanasiasa wadogo ndani ya chama chake, anatakiwa kushirikiana nao na hasa kuwasaidia ili wafanye vizuri zaidi katika utendaji kazi ukizingatia kwamba yeye atakuwa na experience nzuri ya kufanya siasa advanced akiwa na umri mdogo.

  Kinachonifanya nitoe ombi hili kwa ZITTO ni kwamba kwa mtazamo wangu kwa matendo yake ya hivi karibuni ni kwamba amekuwa muoga kwa kufikiri kwamba vijana hawa wanaweza kupata umaarufu zaidi yake hivyo katika khakikisha hawamfikii ameanza kufanya siasa ambazo sio za kipinzani lakini zinazomfaidisha yeye binafsi ambazo kwa kweli kabisa zitamfanya kuwa mkwasi kuliko wao, anajitengenea connection serikalini ambazo ni nadra sana kupatikana ukiwa mwanasiasa mwenye mlengo wa kichadema especially sasa.

  Namshauri ZITTO ajaribu kumuiga ROONEY, ambaye kama angekuwa na mawazo kama ya ZITTO basi angetaka yeye ndio awe the top scorer, the most terrifying manutd striker nk. inawezekana anafahamu kwambA hiyo sio displine ya game, au anafahamu umuhimu wa team playing au ndo kwamba amejaariwa hekina na busara, anatambua kwamba atoaye riziki ni Mwenyezi Mungu.

  Hivyo napenda kutoa dukuduku langu kwamba ningependa kumuona ZITTO anashirikiana na Divid Silinde Mbunge wa Mbozi kama sikosei kama ambavyo ROONEY anacheza na Chacharito. Napenda kuwaona wakiwa jukwaa moja wakifanya first class politics (kama hizi za sasa), Napenda sana kumuona ZITTO akisimama na kutetea hoja za mnyika na Rema bungeni kwa style ile ile aliyomshukia mwenyekiti wa kikao cha Bunge baada ya DR SLAA kupewa majibu ya hovyo hovyo. Natamani kumuona ZITTO anazunguka kuhamasisha UMA na silinde wakisimama na kuzipangua hoja za Ridhiwan na Beno.

  Kwa nini haiwi hivi?
   
Loading...