Ronaldo de Lima

Huyu Jamaa alikukuwa Tishio kwa mabeki na makipa maana alikuwa anawanyanyasa sana,Sijapata kuona Mshambuliaji wa aina yake kwa miaka ya hivi karibuni,hata wa kufananishwa nae kwa uchezaji wake!
 
Nakumbuka ile 2002 world cup kuna big G flani hivi ukinunua ndani zina picha ila ukikuta picha ya de Lima unashinda zawadi

Baada ya mda mrefu siku iyo nikaja kupata kapicha ka de Lima yule mwenye duka kachukua ile picha akanidanganya kesho ntaenda kukuletea zawadi yako ukichanganya na utoto basi nikapigwa kesho kesho kesho mpk ule mchezo ukaishaga na duka likafirisika likafungwa

Kwa sasa yule jamaa yupo nyumba flani ivi anauza maji ya bomba na uzee unamnyemelea nikija kitaa lazma anigongee buku buku coz ananikumbuka sana

Hilo ni moja ya jambo linalonikumbusha kuhusu de Lima mbali na ustadi wake wa soka
 
Mbona mpira wa sasa hauvutii???au ndio nazeeka wadau!!!!!

Dem boy, uliishawahi kuwa na kidaftari umebandika picha za wachezaji kutoka katika babrish???
 
Mbona mpira wa sasa hauvutii???au ndio nazeeka wadau!!!!!

Dem boy, uliishawahi kuwa na kidaftari umebandika picha za wachezaji kutoka katika babrish???
Hiyo ya Kubandika Picha za wachezaji kwenye daftari nimepitia miaka ya mwisho ya Themanini,hasa timu za nyumbani....wakina Selestine Sikinde Mbunga,Faustine kibingwa,Abeid Mziba,Sahau Kambi n.k walipamba kurasa sana kipindi chao...kweli tumetoka mbali
 
Scolari alishangaa uchezaji bora wa kombe la dunia kupewa Ronaldo na si Rivaldo hiyo japan na korea..
 
Huyu Jamaa alikukuwa Tishio kwa mabeki na makipa maana alikuwa anawanyanyasa sana,Sijapata kuona Mshambuliaji wa aina yake kwa miaka ya hivi karibuni,hata wa kufananishwa nae kwa uchezaji wake!
Hasa namkumbuka mechi ya fainali kati ya Germany na Brazil nchin Korea kusini mwaka 2002, alipiga bao mbili matata sana na kuibuka mfungaji bora akiwajibu watu walioanza kuponda kwamba ameshuka kiwango.
 
Hiyo ya Kubandika Picha za wachezaji kwenye daftari nimepitia miaka ya mwisho ya Themanini,hasa timu za nyumbani....wakina Selestine Sikinde Mbunga,Faustine kibingwa,Abeid Mziba,Sahau Kambi n.k walipamba kurasa sana kipindi chao...kweli tumetoka mbali
Magazeti ya uhuru na mfanyakazi baadae ikaja motomoto mzee alikuwa ananunua gazeti la africa now lilikuwa la rangi wacha kabisa nasi tumekula tuchumvi si haba.
 
Mbona mpira wa sasa hauvutii???au ndio nazeeka wadau!!!!!

Dem boy, uliishawahi kuwa na kidaftari umebandika picha za wachezaji kutoka katika babrish???
Siku hizi hakuna wachezaji kuna masharobaro tu,Moira waliondoka nao akina De lima
 
Back
Top Bottom