Ronaldo awajibu waandishi kwa vitendo

Primier

Member
Dec 16, 2015
86
14
160117185909_cristiano_ronaldo_512x288_getty_nocredit.jpg


Christian Ronaldo ni kama amewajibu kwa vitendo wanahabari wale ambao jumanne alikataa kuendelea kuongea nao pale alipoulizwa kuhusu ukame wa magoli ya ugenini.

Goli lake la 33 la Musimu limeisaidia Real Madrid kusogelea robo fainali ya Champions Ligi. Kikosi kilichoko chini ya Zinedine Zidane kimeichapa Roma bao mbili kwa moja.


Kabla ya Mechi hiyo Mshambuliaji huyo alikuwa ameondoka kwa hasira katika katika chumba cha mahojiano baada ya kuulizwa juu ya rekodi ya ufungaji magoli katika mechi za ugenini msimu huu.

Ronaldo mwenye miaka 31, mpaka hapo alikuwa amefunga magoli 32 msimu huu lakini hakuwa amefunga nje tangu mwezi Novemba. "Nani mwingine amefunga magoli mengi ugenini kuliko mimi tangu nimekuja Hispania?

Ronaldo mfungaji namba moja wa Championzi Ligi aliuliza kwa kukereka "Taja mchezaji mmoja ambaye amefunga kuliko mimi. Hakuna jibu? Sawa. Asante" Akaondoka.
 
Kuna ambacho napenda toka kwa uyu dogo anajiamini sana na anajua kua anajua basi burudani hakuna muda wa kuwaburudisha wehu ambao wanajipanga kukukwamisha.
 
Hana lolote uyo, gaucho na huyu jamaa siwatofautishi wamefanana everything, kujiona sana,kujisikia, ni ujinga tu usiokuwa na maana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom