Ronaldo akatia timu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ronaldo akatia timu

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by vukani, Mar 12, 2010.

 1. vukani

  vukani JF-Expert Member

  #1
  Mar 12, 2010
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 245
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Huyu jamaa, rafiki zake walikuwa wakimuita Ronaldo, sio kwa umahiri wa kucheza mpira bali kwa umahiri wa kuvichezea visichana vya shule.
  Alikuwa ni hodari sana wa kuvitokea visichana kwa maneno matamu na longo longo kibaao, kwani, kama ni suala la kuhonga hakuwa na pesa, alikuwa ni mganga njaa na kula kulala akiishi na kaka yake aliyekuwa brigedia wa jeshi maeneo ya Kijitonyama.
  Msimulizi wa stori hii ya kitaani ni shoga yangu mmoja niliye soma naye sekondari.

  Stori yenyewe iko hivi:
  Katika mtaa aliokuwa akiishi huyu kijana kulikuwa na duka la dawa ambalo muuzaji na mmiliki wake ni mama mmoja mtu mzima,. Sasa huyu kijana alikuwa kila akipata Mlupo (msichana), alikuwa na kawaida ya kununua kondom katika lile duka la dawa na ili kuwafanya watu wengine wasielewe alikuwa akiziita socket breaker. Alikuwa ni mnunuaji mzuri wa kondom pale dukani mpaka yule mama akamzoe.

  Baadae yule mama alihamishia duka lake maeneo ya Tegeta ambapo ndipo alipojenga nyumba yake, na huo ukawa ndio mwisho wa kuonana na yule kijana mnunuzi wa Condoms.

  Basi katika pilika pilika za Ronaldo kufukuzia mademu akakutana na binti mmoja aliyekuwa akisoma chuo cha Biashara pale Akiba maarufi kama CBE, na baada ya kuwa na mahusiano naye kwa takribani mwaka mmoja kijana Ronaldo alijikuta akiwa amefika Kigoma mwisho wa reli hivyo akaamua amuoe binti huyo.

  Baada ya makubaliano, binti akatoa taarifa nyumbani kwao kuwa amepata mchumba na baada ya mchakato wa taratibu kadhaa za maandalizi ya kutambulishwa kwa wakwe watarajiwa ndipo kijana akaalikwa yeye na mshenga wake na ndugu zake kwenda kujitambulisha.

  Walipofika nyumbani kwa binti walikaribishwa vizuri na wenyeji wao, Mara mama mkwe mtarajiwa alipomuona mkwe mtarajiwa, akataharuki, “Heeeee yaani huyu Saidi Makondom ndio anataka kumuoa binti yangu, haki ya mungu sikubali”

  Mama alipoulizwa na mumewe kisa cha kumdhalilisha mkwe mtarajiwa ndipo alipowapasha kwamba yule kijana alikuwa ni mnunuzi wa Kondom dukani kwake wakati duka lake lilipokuwa Kijitonyama kabla yakulihamishia Tegeta.


  Ilibidi zoezi la utambulisho lisitishwe na huo ukawa ndio mwisho wa ule uchumba….
  Said Makondom akakosa mke….duh…..
   
 2. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #2
  Mar 12, 2010
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Walipofika nyumbani kwa binti walikaribishwa vizuri na wenyeji wao, Mara mama mkwe mtarajiwa alipomuona mkwe mtarajiwa, akataharuki, “Heeeee yaani huyu Saidi Makondom ndio anataka kumuoa binti yangu, haki ya mungu sikubali”

  Mama alipoulizwa na mumewe kisa cha kumdhalilisha mkwe mtarajiwa ndipo alipowapasha kwamba yule kijana alikuwa ni mnunuzi wa Kondom dukani kwake wakati duka lake lilipokuwa Kijitonyama kabla yakulihamishia Tegeta.


  Ilibidi zoezi la utambulisho lisitishwe na huo ukawa ndio mwisho wa ule uchumba….
  Said Makondom akakosa mke….duh…..
  [/QUOTE]

  Badala kushukuru kijana anajilinda na atamlinda mwanae anamkataa kweli mwehu,
  ngoja ampate ambae hajui bei ya ndom:D
   
 3. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #3
  Mar 12, 2010
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,707
  Likes Received: 8,253
  Trophy Points: 280
  Kwani huwa ni how much,...!??
   
Loading...