Rombo: Aweso amsimamsha kazi meneja RUWASA

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,811
4,533
Waziri wa Maji nchini Tanzania, Jumaa Aweso amemsimamisha kazi Meneja wa Wakala wa Usambazaji wa Maji vijijini (Ruwasa), Mhandisi Nevard Kihaka kwa kumdanganya na kumpa taarifa za uongo juu ya upatikanaji wa maji katika vizimba 14 Kati ya 16 jambo ambalo sio kweli.

Aweso amemsimamisha kazi jana Julai 13 wakati alipotembelea baadhi ya vilula hivyo vya maji kujiridhisha na kukuta maji hayatoki.

"Kwa kuwa umenidanganya na huku ndiko mnakofanya kazi na tunafanya kazi na wewe na ndiyo tumekuamini na sisi ndio tuliokuteua uje hapa utusaidie na ukatudanganya wewe hapa hautufai. Mimi ninavyoondoka hapa leo chukua mabegi yako uondoke ,"amesema Waziri Aweso

Aidha alimpa siku moja Mhandisi aliyekuwa anasimamia Mradi wa Maji Shimbi na kuhamishwa Ileje arudi Rombo mara moja na akamtwe ili ajibu kwanini hakukamilisha Mradi huo pamoja na kujibu fedha za serikali alizipeleka wapi.

"Mhandisi aliyesimamia Mradi huu na kuhamishiwa Ileje arudi Alhamis hii na akamtwe na aeleze ni kwanini Mradi huu haujatekelezwa kama ilivyokusudiwa ilhali amechukua fedha za serikali," amesema.

"Hawezi kuharibu Rombo alafu akahamishiwa sehemu nyingine haiwezekani ,nataka Alhamis afike akiwa na mkandarasi wakamatwe na waeeleze kwanini walichukua fedha za serikali na wananchi hawana maji,mkuu wa Wilaya naomba usimamie hili," amesema Aweso

Awali Meneja huyo alimhakikishia Waziri Aweso kuwa vizimba 14 Kati ya 16 ndio vinatoa maji hali ambayo ilipelekea wananchi kuingilia Kati huku wakimweleza Waziri kuwa taarifa hizo sio za kweli ndipo Waziri alipotaka kwenda kuangalia baadhi ya vilula hivyo na kukuta havitoi maji.

Mwananchi
 
Shida ya Maji Rombo sijui kama itakwisha mapema, Jana hio hio wanasema kampuni iliyokuwa ikisambaza maji Rombo KILIWATER imevinjwa ama kusimamishwa kuendelea kutoa huduma na sasa inaundwa mamlaka ya maji safi na taka Rombo, Lakin aliyekuwa meneja/mkurugenzi wa Kiliwater ndio kateuliwa kama kaimu wa mamlaka hiyo Mpya. Yaani ni KESI YA NGEDERE UNAMPA NYANI
 
Naupenda huu mfumo alokujaga nao hayati, hakuna kubembeleza mtu, Tanzania ni kubwa kuliko mtu
 
Kwa mfumo huo tunaweza kupiga hatua.

Huu utamaduni wakuweka majukwaa nakumchora Rais anapokuja kuzindua miradi nakusifiana tu huwa inakera sana wakati miradi ovyo.

Mtu ameharibu unamhamisha kwa cheo kilekile,unazidi kumpa kiburi aendako.Peleke akawe mlinzi wa Pampu huko
 
Back
Top Bottom