Roma kupotea-Usalama ni somo la muhimu zaidi

jamiiyamtimkavu

JF-Expert Member
May 20, 2011
274
192
Kwanza nikiri mimi si mwana usalama hivyo sina taaluma hiyo. Pili, simhusishi yeyote na utekwaji.
Lakini ni ukweli kuwa elimu ya usalama kwa watanzania wengi ni ndogo kuliko hata elimu ya uraia. Nahisi hii imetokana na hali ya amani iliyopo katika nch yetu. Nayasemayo kwa kuwa ukifuatilia kwa makini utekaji wa Roma utabaini yafuatayo, ambayo ninaamini kiusalama Roma au wamiliki wangeweza kuufanya uma ujue nn kiliendelea japo kwa kiduchu

1. Pamoja na kuwa watekaji walikuja na gari hakuna anayejua namba ya gari hata kama ni bandia.
2. Pamoja na kuwa watekaji walifanya mahojiano na Roma hakuna anayejua waliongea ni nn na Roma?
3. track system za vyombo za mziki na studio, kwa hali ya dunia ya sasa hivi vitu havifichiki, yaani unapata mpaka GPS ya mahali vilipo.
4. Simu kuipata sio tu mnara wa simu, lakini kama device nyingine ikiwa online unajua hadi point iliko, lakini kama ikitokea watu wanaihusisha Serikali na simu ikohewani kuna njia nyingi za kumtafuta...Nadhani hapa kuna watu wananielewa

Tujiulize je tunasababu ya kukuza elimu yetu ya usalama?

moderators, hapa ni mada ya usalama naomba usiungenishe
 
Kuhusu kujua tips za usalama kama mleta mada alivyosema ni kweli wengi hawajui haya mambo na Mara nyingi watu wa namna hiyo wanapokufuata kwanza wanakuja as friend then taratiibu wanakwambia twende tukaongelee kwenye Gari....hii unaweza kuishtukia ikiwa unaelewa hayo mambo vinginevyo utakwenda
 
Back
Top Bottom