HNIC
JF-Expert Member
- Sep 6, 2011
- 1,898
- 2,195
Hawa ni wadau wa soka wa mkoa wa Dar es Salaam enzi hizo . Mwaka 1986 walichangia kutuweka madarakani IDFA ya akina Mussa Shagow. Kutoka kushoto ni Margaret Bwana. Luke luhui. Afisa utamaduni wilaya ilala. Marehem Malik Chanzi. Amin Bakhressa. Chando. Hamisi Kissiwa. Abdallah Kisungura.Mstari wa pili viongozi walikuwa Saidi Kizega. Mussa Shagow. Abdallah Katungunya. Wadau wengine. Gerald Sewe Jaluo. (R.ip) Shabani Kinana(r.i.p)Shaaban Zembwela(r.i.p) Maharani Mkamba na wengineo
-Picha kwa Ihsani ya mzee wetu Mussa Shagow
Mohammed Said na wengineo
Tuaomba mtuleteee history ya namna vilabu vya soka kwenye historia ya Tanzania
Je ni kweli soka la Tanzania lilishuka baada ya Nyerere kuambiwa na Gama Abdel Nasser wa Misri awadhibiti vilabu vya soka kwa sababu za kisiasa?
Hivi ni kweli klabu ya YANGA ndio iliyozaa Klabu ya SIMBA?
Je ni kweli Yanga ilikuwa ni klabu ya the masses na simba ilikuwa na bado ni Klabu ya ma "UNCLE TOMS"? yaani Simba ni klabu ya ma middle class na watu waaliokuwa karibu na watawala wa kikoloni?
Je ni kweli Yanga ilikuwa ni klabu ya walalahoi, na watu wa hali za chini?
Je marais wetu walikuwa wanashabikia vilabu vipi?
Hebu tupatie historia ya akina ya akina Mussa Shagow, Captain Malik, Mzee Ugundo na wengineo