Basi kama ndo hivi ili mtu ajae nguvu za Roho Mtakatifu halazimiki kuwa Mtristo kwanza. Anaweza kujaa roho akishakuwa anamuamini Munbu na Mungu akiwa na kusudi naye anamjaza tu kama ambavyo amekuwa akifanya tangu enzi za Mababu. Hata Sauli alikuwa anajazwa nguvu za Roho Mtakatifu na roho chafu pia.
Yakobo 3:11.,12.
11. Je! Chemchemi katika jicho moja hutoa maji matamu na maji machungu? 12. Ndugu zangu, Je! Mtini waweza kuzaa zeituni, au mzabibu kuzaa tini? Kadhalika chemchemi haiwezi kutoa maji ya chumvi na maji matamu.
Mathayo 22:29.
29. Yesu akajibu, akawaambia, Mwapotea, kwa kuwa hamyajui maandiko wala uweza wa Mungu.
Mungu ambaye ni mwema ambaye anatoa roho Mtakatifu ambaye ndio roho wake mwenyewe anaweza kutoa roho chafu? Inamaana anayo hiyo roho chafu pia???
Yoeli 2:28.
28. Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu, waume kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono;
Agano la Kale ndio walikuwa wanapewa roho kwa kazi maalum na ni kama portion lakini zama hizi ni kwa kila atakae muamini Yesu Kristo.
Ezekieli 36:26.,27.,28.,29.
26. Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama. 27. Nami nitatia roho yangu ndani yenu, na kuwaendesha katika sheria zangu, nanyi mtazishika hukumu zangu, na kuzitenda. 28. Nanyi mtakaa katika nchi ile niliyowapa baba zenu, nanyi mtakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wenu. 29. Nami nitawaokoeni na uchafu wenu wote; nitaiita ngano, na kuiongeza, wala sitaweka njaa juu yenu tena.
Hii ndio kusudi la kupewa Roho Mtakatifu