MoroGent
Senior Member
- Jan 10, 2018
- 146
- 460
Salaam sana Wakuu,
Leo nimewiwa kutoa muhtasari wa kitabu cha "Who Will Cry When You Die?" Kilichoandikwa na mwandishi maarufu aitwaye Robin Sharma (huyu ndo ameandika pia The monk who sold his ferrari, The leader who had no title na The 5 AM Club).
Kitabu hiki kinavutia sana kukisoma kwa sababu mada zake au chapter zake ni fupi na zina mkusanyiko wa masomo 101 mafupi ya maisha yanayokuhamasisha kuishi maisha yenye maana, utulivu na ari.
Kila sura ina ushauri wa vitendo kuhusu jinsi ya kujiendeleza binafsi na kuacha alama nzuri kwa wengine.
Kuna mambo kadhaa ambayo nimejifunza kwenye kitabu hiki ikiwemo;
1. Kusudi la Maisha: Kwanza Swali la kichwa cha kitabu linakutaka ujiulize unaishi vipi na nini utakachowaachia wengine ukiondoka.
2. Nidhamu na Tabia katika maisha: Robin anasisitiza umuhimu wa mazoea kama kuamka mapema, kuandika kumbukumbu, kutafakari, na kusoma kila siku.
3. Huruma na Wema: Kitabu kinahimiza kuwasaidia wengine, kuwa mkarimu na kuishi kwa upendo.
4. Thamani ya Muda: Anakushauri kuthamini muda, kuishi kwa urahisi na kuwa na mtazamo wa sasa.
5. Amani ya Nafsi: Anasisitiza ukuaji wa kiroho na wa kibinafsi badala ya kutafuta mali pekee.
UJUMBE MKUU wa KITABU:
Kiujumla Usiishi tu kwa mazoea, ishi kwa makusudi. Gusa maisha ya wengine, fuata ndoto zako, na uwe mtu ambaye akiondoka watu watahisi pengo lake kwa dhati.
Nawasilisha,
Hakika baadhi ya Maarifa yamefichwa kwenye Vitabu