Robertinho imebidi nikuangalie kwa makini

Edson Carrington

JF-Expert Member
Oct 30, 2022
216
634
Habari wakuu,

Kwanza naomba nitangulize pongezi zangu moja kwa moja kwenye bodi ya usajili simba kwa kusajili wachezaji wa level za juu kabisa na waliokomaa kwenye michuano na ligi kubwa barani Africa, Kiukweli hongereni sana. Na pia nishukuru mashabiki wenzangu kwa sapoti kubwa tunayoitoa kwa klabu yetu.

Lakini baada ya haya yote naomba kutoa attention kubwa kuhusiana na kocha mkuu Robertinho. Kiukweli wote tunakubaliana na ukweli kwamba toka aingie klabuni bado hajatupatia kile wanasimba tunahitaji au kuifikisha simba pale panapostahili. Matokeo yake amechangia kwa kiasi kikubwa kubadilisha falsafa za timu kiuchezaji tofauti na tuliyozoea Kwani hata ule mpira wa pasi na mipango mingi (pira biriani) sasa haupo.

Kitu kingine ni wasiwasi na jicho la Robertinho kung'amua vipaji vilivyomo ndani ya klabu. Sidhani kama kocha Robertinho ameshindwa kuiona hazina iliyomo ndani ya miguu ya Moses Phiri ambaye staili yake ya uchezaji inafanana na mganda Emmanuel Okwi.
Kibu Denis si mbaya bali ni mchezaji mwenye makosa mengi ikiwemo kupoteza mipira mara kwa mara mfano ukifuatilia mechi zake nyingi na hata kwenye mechi ya juzi.

Sitastaajabu pia Luis Miquissone akipigwa benchi la kudumu na kocha Robertinho Simba kutokana na staili yake ya uchezeshaji na wachezaji anaowataka. Kwani Ikumbukwe Pape Osman Sakho alilalamika sana kuhusiana na Robertinho juu ya maamuzi anayoyafanya.

Mechi ya juzi imeonyesha ni namna gani Simba ya siku hizi inavyotegeneza nafasi chache za mashambulizi ukifananisha na kipindi cha nyuma. Power Dynamos hawakuwa na beki imara kiasi hicho cha kuzuia Simba kutotengeneza nafasi za kutosha. Hivyo kocha Robertinho anaonekana bado hajatengeneza chemistry ya kueleweka yenye kuleta tija kwa kikosi tulicho nacho.

Yote kwa yote Simba iwe makini sana kwenye hili maana wachezaji waliobora kwa sasa wako wengi kikosini, kinachotakiwa ni umakini wa kupata kikosi cha kwanza klabuni hapo. Isitokee mambo yaende kombo kutokana tu na mapenzi ya kocha juu ya mchezaji fulani.

Hii itasaidia mwisho kumtafuta mchawi nani na pia tusije jilaumu kufanya usajili mkubwa halafu klabu kutofanya chochote cha maana mwishoni mwa msimu.

Shukrani wanasimba.
 
Nadhani tumuachie kocha kwanza, yeye achambue kikosi chake Bora na aende nacho akifeli hapo ndo tutaelewa nani mchawi .
 
Back
Top Bottom