RIWAYA

Makonyeza

Member
Joined
Feb 2, 2020
Posts
72
Reaction score
261
Taarifa ya Msiba ilimfikia Watende kama taarifa ya kawaida isiyomuhusu ikitagazwa kupitia idhaa moja ya redio mjini Iringa wakati yeye akiwa ni mmoja wa abiria katika daladala moja likitokea eneo la Kihesa kuelekea Mwangata.
Akiwa ametulia katika siti baada ya kubahatika kuipata kutokana na msongamano mkubwa wa abiria, alionekana amezama katika tafakuri juu ya jambo alilolijua yeye mwenyewe kama ambavyo kwa abiria wengine ilivyokuwa ukiachilia mbali wachache waliokuwa wakizungumza wao kwa wao.
Hakuizingatia ile taarifa ya msiba wakati ikitangazwa, hakuwahi kusikia wala kutarajia kusikia taarifa ya msiba inayomuhusu kupitia redioni, lakini kile kipande cha maneno ya mwisho ya habari ile ndicho kilimstua, tena baada ya kusikia jina analolijua.
“…..habari ziwafikie….na kaka wa marehemu bwana Zakayo Matutu wa Kijiweni Iringa, na ndugu na jamaa wote wanaohusika na msiba huo, nitarudia….”

Tangazo lilirudiwa kama ilivyo utaratibu wa kawaida kwa matangazo ya vifo, lakini kwa bahati mbaya Watende hakuweza kusikia vizuri baada ya zogo kuzuka baina ya …..

'Mchezo Mchafu' ni Kitabu kipya cha riwaya kitakachokuwa dukani hivi karibuni, usikose nakala yako kwa Tshs. 15,000/-
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…