FANANI MTENZI
Senior Member
- Jul 4, 2017
- 106
- 95
Kwa wapenzi wa simulizi jiandaeni kupokea ujio mpya wa riwaya ya KOMBORA KIOTANI
Kuyajua maisha ya rais bi Kilua mpenda kuchepuka anavyoweweseka akiwa madarakani itaanza rasmi jumatatu.Safiri nami katika mchirizi wa riwaya hii kujua kiti cha uongozi alichopewa bi Kilua kinavompelekesha siku ya kwanza.Hakuwa ameandaliwa kuwa rais wala hakutegemea zaidi ya kupewa ghafla kumrithi rais aliyeuawa!Je,wanawake wanaoonekana dhaifu barani Afrika wanaweza kuongoza nchi miongoni mwa wanaume simba!Mwanzo wake tayari umechapwa kwenye blog hii unaweza ipitia.
KOMBORA KIOTANI-1
BONIFACE BIRAGE
Uwanja ulipambwa kwa tabasamu za wana nchiMagwaride kadhaa yameshapita kutoa heshma zao kwa mkuu wan chi aliyekuwa jukwaa kuu. Mavazi yaliyovaliwa hapa asilimia kubwa yalikuwa yakizalendo hasa kwa rangi zilizopo kwenye bendera ya taifa. Uzalendo ulitukuka baina ya taifa hili linalokumbuka siku ya uhuru wa taifa lao kutoka kwa wakoloni waliowatawala.
Kiuhalisi taifa limeshapiga hatua kutoka kwa mkoloni.Kuimarika kiafya,elimu,ulinzi na mengine mengi.Lilikuwa taifa imara na linaendelea kuimarika japo kwa mapungufu kadhaa wa kadhaa.
Jeshi la taifa la KIOTA kwa sasa katika sherehe za uhuru lilikuwa linafanya mazoezi kuonesha wana nchi wake uimara na ukakamavu wa jeshi.Pia walikuwa wakimuhakikishia mkuu wan chi ulinzi uliotukuka. Vyama mbalimbali vya siasa vilikuwepo katika sherehe hii pamoja na viongozi wa kitaifa.
Vilevile kulikuwa na mialiko ya mataifa ya kadhaa japo wengi wao walituma udhuru na kuleta wawakilishi wao katika uwanja wa taifa.Ulinzi ulikuwa umeimarishwa katika jiji kuu la nchi ambapo taifa lilikuwa linashuhudia maadhimisho haya.
Rais Kisusi akiwa ameketi meza kuu, pembeni yake alikuwepo mkuu wa majeshi upande mmoja na upande mwingine alifuata naibu rais wake na viongozi wengine. Waliteta na mkuu wa majeshi.
“Kinachofuata ni nini jeneral maana leo sijisikii vizuri sijui kwanini?”aliuliza rais Kisusi.
“Ni mwite daktari?”aliuliza jenerali Tindikali.
“Hapana aliniambia sina tatizo.”alijibu rais Kisusi.
“Itakuwa msongo wa mawazo mkuu.Usijali nchi ipo salama.”
“Na wasiwasi na uchaguzi ujao.Lakini sio kwa hilo ni kwamba roho inanienda mbio sana.”
“Kivipi mkuu?”
Walikuwa maswaiba wakuu tangu shuleni tofauti ni majukumu ya kazi lakini wote ni wazalendo wazawa wa taifa la Kiota walioamua kuitumikia nchi yao.
“Au ni vile majirani zako hawajaja?”
“Hapana Tindikali.”
“Au tuhairishe shughuli?’”
“No!Leo ni dhifa muhimu sana sidhani kama kuna haja ya mimi kuondoka ghafla. Ngoja niimalize then tutaondoka.Unajua file namba 13.14 linanitatiza sana kiasi nakosa Amani.”alisema rais Kisusi ambapo alipitisha kitambaa kufuta kijasho kilichokuwa kina msumbua.
“Lina ufumbuzi hakuna kidudu mtu atakayesumbua.”Alijibu jenerali Tindikali.Waligutushwa na mshereheshaji aliyekuwa akielezea makundi mbalimbali ya ulinzi yaliyokuwa yanafanya mazoezi.
“Halafu Mkuu kinachofuata ni Maonesho ya ndege mpya za kijeshi tulizo tengeneza.”
Rais alipitisha ulimi kwenye papi za midomo yake nakuachia tabasamu hafifu.Akaangalia juu kusubiri maonesho ya ndege.
“Ndege inaendeshwa na Kapteni Pilipili ya kwanza kabisa kufanya onesho lake.Inatoka makao ya Msanda.Mh RAIS unasikia sauti ikizizima uwanja mzima.Haya ni mafanikio chini ya utawala wako.
Ni ndege yetu wenyewe MI fighter Jet ian uwezo wa kwenda kilomita mia tatu kwa saa.Ina beba makombora kwa kumshambulia adui.Kwa heshma mh rais Kaptein…”MC alikuwa anahutubia.
Kaptein Pilipili akiwa angani kuelekea uwanja wa taifa kuonesha ndege mbele ya rais wao.Alianza kuhisi mikono mkimtetemeka.Makao yakuongozea ndege yalikuwa yakiwasiliana naye kumpa maelekezo ya kipi cha kufanya.Lakini ghafla alipoingia kwenye anga la uwanja aliekeza ndege moja kwa moja kwenye meza kuu walimoketi Rais na watu wake.
Halafu akabonyeza kitufe cha kuachia kombora lakini hakubonyeza la kuruhusu kombora kutoka bali mlango wa kombora ulibaki wazi.Na kwa kasi atakayoenda nayo mpaka kufika kwenye jukwaa halitakuwa limeanguka kutoka kwenye eneo lakuhifadhi bali kama ndege ikiwaka moto au kulipuka bila shaka kombora lingelipuka.Kasi yake ilikuwa ya sekunde.
“Mh Rais kaptein Pilipili ndo….”hata kabla hajamaliza tayari ndege ilipigiza kwa kasi kwenye jukwaa.Kishindo kizito kilikuwa kimejiri. Lakini wakati wa butwaa lile likiendelea kuna mlipuko mwingine ulitokea pale uwanjani! Mlipuko mzito. Moto ulipanda juu na moshi mzito kufuka.Kilio kilikuwa kimesikika kikubwa sana tena cha kuogofya kiasi watu walishtuka ambao hawakupatwa na mlipuko ule.
Vikosi vya kijeshi vilivyokuwa pale uwanjani nakubahatika kukoswa na mlipuko ule vili taharuki kwa harka maana mshtuko uliotokea ni waaina yake.Vyombo vya habari kadhaa vilipoteza mawasiliano hasa kamera zilizokuwa karibu jukwaaani.Lakini kwa kamera zilizo mbali kidogo hazikupatwa na kadhaia hiyo. Mambo yote yalionekana mubashara kwenye vyombo vya habari.
Taharuki iliyokuwepo katika taifa haikuwa na maeleoz!Nchi ya Kiota ilikuwa taabani.Na kwa haraka tu ilikuwa vigumu kujua ni wangapi walikuwa wamekumbwa na kadhia hii!Ilichukua muda kwa vyombo vya habari kuanza kutangaza kinachotokea uwanjani.Waliopo studio waliona kama ni sinema wana tazama lakini ukweli ni kwamba balaa kubwa lilikuwa limetokea.
Wakati simu zikipigwa maeneo mbalimbali huku vyombo vya ulinzi vikijitahidi kujua ni ktiu ganoi kimetokea hadi ndege ilyokuwa ikirushwa kwa maonesho ikapoteza mwelekeo nakuanguka jukwaa alimokuwamo Rais Kisusi. Jukwaa ambalo serikali nzima ilikuwemo!Ilikuwa maapema mno kubashiri tukio hili ambalo bichi sana!
Nchi ya Kiota ilikuwa imesimama hakuna kilichosonga. Waliokuwa karibu na maeneo yale nje ya uwanja walianza kutimua ovyoo. Waliopo ndani walianza kutoka nje msongamano ambao ulisababisha purukushani hadi watu kubanwa chini nawengine kupoteza fahamu.
Taharuki!Taharuki kuu!
Taifa limetetemeshwa!Kiota imeanguka chini kwa kishindo!
****
Makao makuu ya jeshi!TRIANGLE
Meza kuu yahali ya hatari ilikaliwa na viongozi wa kijeshi waliokuwa wamebaki kambini.Kulikuwa taharuki.Hakuna kilichotulia kila mmoja aliongea lake.Simu ikipigwa huku na kule.
“Nimesema tuna tuna tangaza hali ya hatari nakuipeleka kwa kiwango cha DEFCON 3.”alisema kanali Rama.
“Hapana huna mamlaka yakupandisha hiyo amri.DEFCON 3 nikubwa sana wewe huoni ni mwenzetu ndokaangusha ndege.”alijibiwa na Major Kanda.
“Major huu siwakati wa mzaa Kiota imepigwa hatucheki na mtu vilevile nataka kujua ikulu nani anachukua napia nijue nani anajua hali ya rais na serikali nzima.Tukisubiri mambo yaendee kijinga tutapoteza nchi!Tuamue hapa hapa kufungulia vikosi vya kijeshi kuingia mtaani.Hivi.”
“wewe ni nani katika nchi uamuru upuuzi huuo!”
“Huna mamlaka hana mamlaka!”
“Pumbavu hujui lolote nimekufundisha kazi mimi.”
Kila mtu alikuwa na wasiwasi na hasira.Hakuna aliyejua ni uamuzi gani wakuchukua kwa wakati huo. Ilihitajika busara na amani ya hali ya juu. Nchi ilikuwa imetikiswa kwa pigo kubwa kuliko yote pona ya watu ilikuwa na wakati mgumu usio na maelezo yakuridhisha. Hali ilikuwa tete.
Hakuna aliyemuamini mwingine.Mfumo mzima wa utawala uliingia dosari ya ajabu. Utamwamini nani? Aliyetekeleza mauaji ni nani? Kwa dhamira gani? Na mpango upi? Ni ajali? Lilikuwa swali lililoshibisha meza nzima ya eneo lile.
“Jamani hebu tutulie natuwe na uvumilivu wa hali ya juu.Nchi nzima inahitaji amani.”alisema moja ya wazee wa jeshi aliye na umri mkubwa.Ni mstaafu lakini mtu mwenye busara alishashinda medani kadhaa kwa juhudi zake jeshini pamoja na ushirikiano mbalimbali alioutoa jeshini.
Vyeo Alisha vipata. Pamoja na mambo mengine,alikuwa mzalendo kwa taifa lake huru. Alilipenda. Alilijali nakulithamini kama kwa uzalendo uliotukuka. Mwili wake wenye ngozi iliyozeeka, sharubu zenye uzito halafu nyeupe pamoja na pua yenye mchongo ilimpa sura ya busara. Utuuzima dawa.
“Ni sawa nchi imepigwa pigo kuu.Hii ni ajali mbaya…”kabla hajamaliza alivamiwa kwa kauli zenye utata.
“Sio ajali!”
“Wewe mzee unazeeka vibaya utaitaje tukio hili ajali?Unaona kuna ushawishiwi wa ajali hapo?”
“Huu ni uvamizi tumepigwa na adui zetu.Haiwezekani rubani wa jeshi ambaye ni mwanajeshi aangushe ndege mahali alipo mkuu wa majeshi na amiri jeshi mkuu ambaye ni rais? Hii ni dharau kubwa sana na haivumiliki kamwe!Lile eneo lilikuwa na umma mkubwa. Kulikuwa na mazoezi ya kutosha yaliyofanyika kabla ya leo. Rubani alijua fika anachopaswa kusema sasa iweje adondoshe ndege hapo?”
Mzee Gwamaka alivuta pumzi ndefu na kuzishusha kwa muda akiangalia hali ya hewa kwa ujumla. Alifikiria kidogo kitu gani cha kufanya. Alizitafuta busara zake zilizojificha ndani ya mvi zake. Akapitisha ulimi kwenye baraza la mdomo wake kasha akasema, ”Najua tukio lililotokea ni zito.
Tena ni kubwa sana. Sio tukio la kawaida. Ni la hatari. Tumepata pigo! Kulalamika sio suluhu. Muhimu tumuombe Mungu atupe ujasiri. Hili sio jambo la mzaa kabisa. Ni jambo lenye huzuni isiyo na mipaka. Kupigwa tumepigwa kweli. Ila sio kwamba ni lazima tuanguke chini kwa pigo hili.”
Wakamsikiliza,wengine walishayaacha makoti yao purazai.
“Ni kweli serikali nzima imetikiswa hatujui nani kapona nani kafa? Bado ni maapema mno. Pamoja na umaapema wote huu hatuna budi kujipanga nakuwa tayari kukabiliana na lolote litakalo tokea. Tuchunguze kwanza,tujue ni nini halafu hali ya dharura itangazwe. Kila sekta iliyopo pale jukwaani ilikuwa na wawakilishi wake.
Wengi wao wakiwa ni viongozi wa sekta hizo. Bila kuficha kuna sekta nyingi zenye pengo hivi tunavyozungumza. Zinahitaji wasimamizi wapya ili nchi iendelee.Inaweza kuwa siyo ajali bali ni kundi la kivamizi kwa lengo lakuiadabisha serikali yetu tukufu. Ndiposa natoa tamko kwamba tufuate protokali.Uchunguzi ufanyike wa haraka sana ila tuwe na bodi maalum yakufanya uchunguzi huu pamoja na shghuli za uokoaji.
KOMBORA KIOTANI-2
BONIFACE BIRAGE
Chumba cha dharura kilifuka moshi wa wasiwasi.Hakuna aliyejua aanzie wapi.Mzee Gwamaka alikuwa akitoa maneno yake.
“Lazima tujue serikali kuu inaendeshwa na nani.Kama rais hayupo hai lazima nchi iwe na kiongozi wa mpito mpaka hapo mambo yatakapokuwa shwari.”
Ni kama walipitisha maazimio yakufuata wakati wakitaka kujua nchi inasimama upande gani kwa muda.Kwa kweli siku ya ujio wa shari ni vigumu kujua kitu gani chakufanza.Njia kuu huwa matatani na usijue ni wapi hapo uanzie.
“Sasa tukisimamia kijeshi jambo hili itaonekana ni mapinduzi hivyo bodi maalum ya sheria itashugulika kuangalia kiprotokali ni nani wakuchukua madaraka.”alieleza mzee Gwamaka.
“Nina swali mzee wangu.Hivi mpaka sasa tukiangalia vizuri ni kitengo gani kitumike kufanya uchunguzi huu?”
“KIS,Kiota Intelligence Service,hawa watatupa jibu kwa haraka.”
“Lakiini kwa nini tusiactivate Destruction Control Unit?”aliuliza Meja Kanda.
“Ndiyo hao DCU wataweza kazi mara moja.Huwa ni kitengo cha siri sana ambacho kiliundwa chini ya amri ya rais mwaka 1969.Kitengo hiki hakijulikani kwa wengi isipokuwa ikitokea hali mbaya kwa taifa.Hiki hakiendani na vitengo vyovyote vya kiusalama.Huwa kimetengwa na hutumika tu endapo kuna usaliti katika taifa.Ila nani anaweza kukipa amri ya kuingia kazini?”alijibu kaptein Utumbo.
“Kinaweza pokea amri kutoka kwa rais kama yupo.Ila rais anaweza kuamrisha DCU 1,lakini DCU 2 rais hana mamlaka kikatiba kukipa amri.Chenyewe huingia kazini ikiwa hakuna serikali nzima.Hufanya uchunguzi maana ni chombo huru.Na huwa tayari baada ya nusu saa wakati imejulikana serikali hakuna.”alieleza mzee Gwamaka.
“Tangu tukio litokee imepita muda gani?”
****
BLACK ZONE 2
Kengele ilikuwa imelia kutoa tahadhara kwa watu waliokuwa wakifanya kazi kwenye eneo hili la siri.Lilikuwa jengo lililojengwa chini ya ardhi.Askari wake wote walikuwa tayari wamejiandaa kwa kazi.Wamekusanyika nakujipanga mstari wakisubiri maagizo.
“DCU tumekutana hapa. Nadhani mpaka sasa mmejua kuitwa kwenu kuna hali ya hatari. Kilichotokea mmekisikia nakukiona kwenye vyombo vya habari. Kwa upekuzi wetu wa ghafla tumeweka nukta kwamba tukio hili linaweza kuwa limejiri kupitia mianya tofauti. Tumeshapewa taarifa na mashushu wetu waliopo uwanjani na jinsi hali ya tukio ilivyo.
Hatujaridhika kabisa na wanaotaka kutikisa taifa letu.Tuliundwa kikatiba na nijukumu letu DCU 2 KUWA ACTIVE endapo tutakuwa na uhakika kwamba hakuna rais. Lengo letu nikuweka mambo sawa. Kusimamia uchunguzi, kusimamisha serikali mpya. Kwa sasa kiongozi wetu anaelekea ikulu kusimamia ni nani anapewa urais.
Timu nyingine itasimamia uchunguzi wa pale uwanjani kwa mapana zaidi. Naomba tuwe macho nakuleta ukombozi kwenye taifa letu tukufu tulilopewa na Mungu. DCU 2 inaposimama ina maana vitengo vingine vya kiusalama havipewi mwanya mkubwa wa uchunguzi sisi tutaenda mbali kujua ni nani muhusika. Tutakuwa kama gesi ya gabon monoxide hakuna wakujua tumefikia uchunguzi gani?”
Watu wa pale walimsikiliza huyu msemaji kwa makini.Kilikuwa kitengo cha siri na hujulikana na wachache na huwa hakiruhusiwi kuingiliwa na taasisi yoyote bali chenyewe huweza kuingia popote. DCU 2 hakikuwa chini ya rais hivyo chenyewe kilikuwa na mamlaka ya upekee. Maelezo ya kushiba yalitolewa kwa hadhira ile.
Baada ya muda wahusika waliandamana kuchukua nafasi zao kwa minajili yakuirudisha Kiota katika usawa. Siku huru ilikuwa taabani. Taarifa zilianza kukusanywa kupitia vitengo mbalimbali kujua ni nini kimetokea na kipi wanatarajia kitokee. Vilio vilivyo tanda katika taifa hilo vilikuwa kama moshi wa volcano.
Nchi imetikiswa. Kujipanga ilihitajika sana. Matukio kama haya yalikuwa yakutisha na kuogofya nakulipeleka taifa kwenye hali ya kutetemesha.
***
Mamia ya waokoaji walikuwa uwanja wa taifa.Macho yalikuwa jukwaa kuu. Vifusi vikitolewa pamoja na miili kuokotwa. Zilikuwa maiti zimepandiana nakufinya wengi. Wapo waliokatika mikono wapo waliopasuliwa vichwa. Asilimia kubwa ya miili ilichomwa na moto wa mlipuko. Zilikuwa maiti zilizo tisha na kuogofya kwa sana. Ilihitaji moyo. Taifa zima liliamishia macho eneo lile.Kulikuwa na mvutano wa hali ya juu.
Maiti zilitolewa nakuwekwa kwenye mifuko yakuhifadhia.Kikosi cha DCU 2 kilikuwa kazini wao walikuwa wakikagua idadi ya viongozi waliopoteza maisha ya orodha ilikuwa ina jaa kwa haraka. Kwa kuwa ni watu waliojipanga na wakala waliopitia mafunzo waliifanya kazi ile kitaalamu. Takribani sekta zote muhimu zilikuwa zimepoteza viongozi wa orodha ilizidi kusheheni majina pamoja na picha za waliowatoka ndani ya lisaa limoja walipata uhakika wakile walichokiogopa kuliko vyote.
“Confirm! Confirm Eagle Sky is down!”huyo alikuwa ni wakala wa DCU 2 akitanabaisha upatikanaji wa Eagle Sky.Habari zikaanza kusambaa kila eneo kuhusiana na taarifa hiyo muhimu. Wakala wa DCU 2 wakaanza kuandaa taarifa nakuzipitisha kwa waliosalimika katika sekta zote za siri na wazi za taifa ili umma uandaliwe kisaikolojia kuhusiana na jambo zito. Sekta zote za kiserikali zilisimama na hakuna kilichoendelea. Vyombo vya habari vilisimamisha matangazo nakutumia muda mchache kutangaza tanzia.
Wimbo wataifa ulipigwa katika vyombo vyote vya habari.Wananchi wa Kiota walikuwa macho na masikio kupokea taarifa husika.Mioyo yenye majonzi.Habari ilianza kusomwa yenye huzuni.
“Habari zilizotufikia hivi punde,hivi leo siku ya kusheherekea uhuru wetu,katika uwanja wataifa imetokea ajali mbaya baada ya ndege ya kijeshi iliyokuwa ikifanya maonesho kupoteza mwelekeo nakugonga jukwaa kuu walimokuwamo viongozi wa taifa. Katika tukio hili lenye kutisha tumepoteza mamia ya raia,rafiki,ndugu,wazazi na viongozi wetu wazalendo waliokuwa kazini.
Viongozi wote wa serikali wamefariki na majina yao tutayatoa muda simrefu. Makiwa zaidi tunayo kwa kuondokewa na Rais wetu Mh Kisusi pamoja na makamu wake,pamoja na baraza la mawaziri wote…”mtangazaji alitaja sekta karibu zote zilizokuwa na uwakilishi katika jukwaa kuu. Lilikuwa pigo tena makiwa makuu. Kitwea kilichokumba taifa zima kilikuja na upepo mkavu uliopenya kwenye mfipa ya hisia ya nafsi nakupafanya tetemeko lenye ukiwa.
Mengi maneno yalipukuchua mbegu za maumivu kuyawakilisha kwenye gunia lenye ujazo wa kihoro. Habari za taifa la kiota zilipita kila pembe ya dunia kuhabarisha masaibu yaliyojiri siku ile ya kiama chao. Rambirambi zilianza kutangazwa pamoja na pole kutoka mataifa mbalimbali yenye ushirikiano na taifa la Kiota. Hayo yalipokelewa ikulu na wafanya kazi waliokuwepo hapo. Bila ajizi walijibu kwa heshima kupokea pole hizo. Ikulu ilikuwa bize kukiwa na malumbano wa hatua gani stahiki kuchukua. Katika mashaka haya mambo yalikuwa na ugumu wake.
Bashasha iliyokuwepo ikulu ilikuwa imekufa nakuzikwa kaburi la sahau!Familia ya Hayati rais Kisusi ilikuwa kwenye huzuni kwa kuondokewa na baba na mama pamoja na wana wao wawili ambao waliambatana na wazazi kwenye tafrija hiyo. Ukoo wa Kisusi ulikuwa kwenye maumivu makali sana. Tayari vikosi vya usalama vilienda kujumuika nao kwa heshma ya Kisusi aliyetumikia taifa lake kama rais.
Tayari kamati maalum ya jeshi iliundwa kushughulikia msiba huo mkuwa. Familia ya makamu wa rais na baraza la mawaziri waliambatana pamoja.Magavana takbribani ishirini na tano waliokuwa katika majimbo yao walisalimika hawa ndo viongozi pekee wakiserikali kisiasa walibaki. Kuna majimbo 30 katika taifa la Kiota.Magavana watano walifariki kwani walikuwemo katika tafrija ya uhuru uwanjani.
Hawa 25 walikuwa na wakati mgumu kutuliza majimbo yao maana hali ilikuwa tete.Walitakiwa kuwa na ujasiri kuliko wakati mwingine wowote ule.Walitakiwa kujipanga kwa haraka kunusuru taifa lao lililokuwa linateketea.Tayari walianza kuwasiliana kujua hatma ya tukio lote.
***
IKULU
DCU 2 walikuwa tayari wapo ikulu.Timu ya wana sheria ikiwa ikiwemo kwa mapitio ya dharura.Kiongozi wa DCU 2,DIRECTOR Masha alikuwemo kwenye chumba cha mikutano.Makaratasi mbalimbali yalikuwa mezani kwake.Walikuwemo walimsikiliza kwa makini wakisubiri kauli yake.
“Ndugu zangu kama mjuavyo taifa limepigwa pigo takatifu.Tuna hitaji mwelekeo wa haraka kujua tunaenda wapi? Katika katiba yetu inchi haitakiwi kukaa bila rais kwa sababu yoyote. Rais wetu Kisusi hayupo na hakuna wakutekeleza majukumu. Nipo hapa kuhakikisha taifa linasonga mbele tuna hitaji tujue nani anatakiwa kuchukua madaraka. Naomba mwana sheria atuelezee.”alisema bwana Masha.
Mzee Panda mwanasheria mbobezi wa serikali alitumia fursa hiyo kueleza mambo aliyuoelewa,”Kwa mujibu wa katika yetu,ikiwa rais hawezi kutekeleza majukumu yake kwa njia ugonjwa au kufa au safari basi makamu wake anachukua usukani. Lakini kwa hapa kwentu ya leo kali. Wote waliopo kwenye mnyororo wakupokea madaraka hawapo.
Makamu hayupo,waziri mkuu,spika wa bunge, na mawaziri wa wizara zote hakuna aliyepo. Hivyo katiba inaeleza zaidi kwa mabadiliko yaliyofanyika miezi sita iliyopita kwamba kama watakao kaimu kwa muda hawapo basi hakutakuwa na budi itabidi tuwatumie magavana. Katiba inasema wazi kwamba wakwanza kuchukua madaraka miongoni mwa magavana wetu ni magavana wa kwanza watano wanaoongoza majimbo makubwa.
Hawa hakuna hata mmoja walikuwepo kwenye tafrija za uhuru.Katiba inaongeza kama hawapo atachukuliwa gavana anayeongoza jimbo dogo kuliko yote.Na hapa namuhitaji gavana wa jimbo la Kibatari.”Mzee Walii Panda alisema.

- KOMBORA KIOTANI-1