KICHUNA CHANGU
Member
- Feb 5, 2016
- 16
- 4
RIWAYA: ANGAMIZO
MWANDISHI: HALFANI SUDY
SIMU 0674 395733
WHATSAPP 0757 633010
SEHEMU YA TISA
ILIPOISHIA JANA...
Itakuwa ni kundi moja kama siyo muuaji mmoja. Lakini awe mtu kiwe kikundi nitahakikisha hafanyi mauaji mengine ya raia wema !" Alisema kwa uchungu mkubwa Daniel. Waliondoka pale Magereza wakiacha mwili wa marehemu Raiya ukipakiwa kwenye gari kupelekwa hospitali. Abdul alikuwa mwenye majonzi sana. Watu wawili waliojitolea kumsaidia kwa hali na mali walikuwa wamefariki kwa tofauti ya masaa machache sana. Ni mkosi gani huu ! Njiani alimuona Daniel Mwaseba akitabasamu. Akajua kuna kitu cha kakiona. Tena bila shaka cha hatari !
"Tunafuatwa" Alimsikia akisema kwa sauti ndogo.
"Ama zetu, ama zao ! "
Waliifuata njia iliyokuwa inaelekea Moshi mjini kutokea Arusha. Abdul roho inamdunda sana. Daniel alikuwa hana wasiwasi hata kidogo. Akiendelea na mluzi wake usioeleweka. Abdul aliangalia kwenye kioo cha pembeni naye aliona.
Gari tatu nyeusi aina ya Noah zilikuwa zinawafuata kwa kasi kubwa sana!.
Daniel alikuwa makini na usukani.
Alipofika Tengeru alikata kulia. Wakawa wanaelekea barabara ya vumbi iliyokuwa inaelekea katika Chuo cha Maendeleo ya jamii, Tengeru. Zilikuwa mbio kali sana kwenye barabara ya vumbi.
Jamaa walianza kurusha risasi!.
Daniel alikuwa dereva makini. Alihakikisha hawadhuriki na risasi zile. Na hawakudhurika!
Daniel aliingiza gari ndani ya Chuo cha Tengeru. Abdul hakutegemea kama ataiingiiza gari Chuoni kwa kasi ile. Yeye alidhani atakata kulia njia inayoelekwa chuo cha Sayansi cha Nelson Mandela.
Haikuwa hivyo lakini.
Sasa Ilikuwa patashika ndani ya Chuo cha Tengeru. Walikuta wanachuo wengi wapo nje. Baada ya kufunga breki kali! Walishuka haraka haraka na kujichanganya na kundi la wanachuo waliokuwa wanaelekea kunywa chai mgahawani. Waliziona zile Noah tatu nazo zikifunga breki kali.
Vumbi lilitimka.
Baadhi ya wanafunzi wa kike wakipiga kelele za uwoga, wa kiume walikuwa wanashangilia. Bila kujua nini kinatokea . Walishuka jumla ya watu kumi na tano toka katika Noah zile tatu. Wote na bunduki mkononi. Abdul na Daniel walikuwa washaingia Mgahawani. Lakini waliona kila kilichokuwa kinafanyika kule nje karibu na geti ya kuingilia Chuoni. Wanafunzi walianza kukimbia hovyo. Jamaa moja alipiga risasi tatu hewani. Sasa lilikuwa vurumai. Wanafunzi walikimbia hovyo huku wakipiga kelele za taharuki. Wakajigawa wale majamaa. Watano walielekea madarasani. Wawili walienda maktaba. Watatu walienda uelekeo wa ofisi za walimu, na watatu wengine walielekea vimbwetani na wawili walikuwa wanaenda Mgahawani walipokuwa kina Daniel.
Daniel aliinuka pale kwenye meza akaenda kujificha nyuma ya mlango wa Mgahawa ule. Abdul alibaki palepale mezani pamoja na wale wanafunzi. Hali ya hofu ilitawala ndani ya Mgahawa.Wote waliwashuhudia watu wale wawili wakija Mgahawani na silaha zao mkononi. Wanafunzi walikuwa na hofu kubwa, walikuwa wanalia kimya kimya. Wale watu waliingia Mgahawani kwa umakini mkubwa sana. Abdul alikuwa anasubiri hatua atakayoichukua Daniel kule nyuma ya mlango. Alikuwa na imani nae sana.
Akaingia wa kwanza.
Akaingia wa pili.
Wote wakiwa na bunduki zao mkononi, aina ya SMG.
Ghafla yule jamaa mmoja alidondoka chini. Watu wote walistuka mule Mgahawani. Abdul akamwangalia Daniel kule nyuma ya mlango alikojificha. Aliiona mdomo wa bastola yake ukiwa unafuka moshi. Akajua bastola ya Daniel imetumika. Na ilikuwa imefungwa kiwambo cha kuzuia sauti. Na bila shaka risasi ilitua mgongoni kwa yule jamaa.
Yule jamaa mwengine alibabaika sana. Hakujua nini kimempata mwenzie. Mgahawa sasa ulikuwa kimya. Kila mtu alitulia kusubiri hatma ya roho yake.Yule jambazi mwengine aligeuka nyuma kuangalia kule mlangoni.
Alikutana nayo!.
Alipigwa risasi ya utosini. Damu chache ziliwarukia baadhi ya wanafunzi waliokuwa karibu naye. Nae alielekea kuzimu bila ya kuaga. Sasa Daniel alitoka kule mlangoni. Akazivuta zile maiti mbili na kwenda kuzificha nyuma ya mlango.
Hakuwa na wasiwasi kabisa.
Alikuwa kama anavuta magunia ya mkaa tu.
"Wanafunzi wote laleni chini haraka. Atakayejifanya mjuaji tu shauri yake !!" Daniel alisema huku na yeye akilala chini.
Baada ya kama dakika kumi sauti za mlango zilisikika tena. Aliingia jambazi aliyevaa sawa na wale wenzake. Suti nzuri nyeusi na shati jeupe ndani. Na bunduki iliyotayari kuuwa wakati wowote itakapoamrishwa. Huyu aliingia bila umakini wowote. Bila shaka alitegemea Uwepo wa wenzake mule ndani. Hivyo yeye hakuwa makini sana. " Chugaaa" alianza kuita. "Naam" Aliitikiwa. Daniel aliitikia ule wito huku akinyanyuka alipokuwa amelala. Jamaa aliashangaa sana. Akiwa Kwenye mshangao Daniel aliachia risasi iliyozama katika tumbo la yule jamaa. Alikufa na mshangao wake usoni ! Daniel aliivuta ile maiti tena na kwenda kuiweka nyuma ya mlango nayo. Ulikuwa ni mchezo hatari sana lakini Daniel aliucheza bila uwoga wowote. Kosa moja tu lingesababisha kifo. Wanafunzi wengi walikuwa wameshajikojolea pale sakafuni kwa uwoga. Abdul sasa kidogo alianza kuwa mzoefu. Mzoefu wa kuona maiti. Mzoefu wa kuona watu wakiuwawa. Alianza kuupenda pia mchezo wa kifo. Watu wote walikuwa wameikumbatia sakafu kasoro Daniel pekee. Alikuwa amesimama akiangalia kule nje. Simu moja ya wale marehemu ilikuwa inaita kule nyuma ya mlango. Daniel alienda kuipokea.
" Chuga hapa " Alisema, kisha alitulia kusikiliza.
"Yah, waje wawili "
Daniel alijitambulisha kuwa yeye ni Chuga. Na kuomba watu wawili waende mgahawani.
Hawakuchelewa.
Walikuja haraka sana. Wakati Daniel akiwa bado yupo kulekule nyuma ya mlango. Alikoenda kupokea simu. Wauaji waliingia ndani huku wakimwacha Daniel kule nyuma ya mlango. Hawakufikiria kabisa kama kuna hatari!
Abdul jicho lake lilikuwa linaangalia nyuma ya mlango, kwa Daniel kuona atafanya nini?.
Alimuona akijishika kiuno.
Alitoka na visu viwili.
Kimoja amekishika kwa mkono wa kulia na kingine mkono wa kushoto. Alivirusha vyote kwa mpigo na kwa nguvu visu vile kuelekea kwa wale majamaa. Vyote vilitua shingoni. Kila mmoja na chake. Walienda chini kama mizoga. Alimuona Daniel akitabasamu. Majambazi wanne sasa alikuwa kawamaliza kimya kimya mule Mgahawani .
Mara kundi la majambazi wote kumi na moja waliobaki kule nje lilikuwa linakuja Mgahawani wakiwa wanakimbia. Bila shaka walihisi kuna kitu cha hatari!
Sasa ilikuwa hatari zaidi.
Abdul nae alianza kutetemeka mwili mzima kwa hofu. Alimwangalia Daniel kule nyuma ya mlango, alimshangaa hakuwa na hofu kabisa mwanaume yule, alikuwa anatabasamu!. Kwa hakika Daniel hakuwa binadamu wa kawaida. Kila hatari inavyomkaribia yeye anazidi kuwa mtulivu na tabasamu lisiloisha usoni mwake. Wale jamaa waliingia ndani ya Mgahawa. Pale nyuma ya mlango sasa Daniel Alikuwa ameshika bastola mbili mkononi. Ndani ya nusu dakika watu wote kumi na moja walikuwa chini. Wote walikuwa wameuwawa na bastola ya Daniel Mwaseba!
Wanafunzi wote walisimama na kumpa mkono wa pongezi Daniel. Alikuwa shujaa kwao. Alikuwa shujaa zaidi kwa Abdul. Walimhusudu sana Daniel. Abdul alimhusudu zaidi Daniel. Walitoka eneo la Chuo huku Daniel akiwapigia simu Polisi waje kutoa maiti zile. Wao walielekea moja Kwa moja kituo cha Polisi Arusha...
ANAITWA DANIEL MWASEBA, TUKUTANE TENA KESHO KUMSOMA HUYU JAMAA.....